Watu 33 wanusurika Kifo kwa kula nyama iliyouzwa Tsh 2000 kwa kilo

Watu 33 wanusurika Kifo kwa kula nyama iliyouzwa Tsh 2000 kwa kilo

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Watu 33 wa kijiji cha Kazingumu kata ya Namelock wilayani Kiteto mkoani Manyara wamenusurika kifo baada ya kula mzoga wa ng'ombe aliyekuwa anapatiwa matibabu ambapo nyama hiyo walinunua kwa shilingi 2000 kwa kilo badala ya bei ya kawaida ya 8000.

Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mbaraka Al Haji Batenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo watu wote wanaendelea vizuri kiafya.

Chanzo: East Africa Radio
 
Watu wamekuwa ni walafi wa kula nyama, nimeponea sana mara nyingi kulishwa nyama za ajabu ajabu ikiwemo nyama za wanyama wasioliwa
 
Hayo maeneo ya kiteto, simanjiro na moshi vijijini kule chini TPC ng'ombe akifa haachwi, anashambuliwa fasta. Kuna dume la ng'ombe lilijifia wenye ng'ombe wakaliacha machungani, wenyeji baada siku moja kuona wenye ng'ombe hawana taimu nalo wakalivamia na kuanza kujikatia nyama kwa kadiri walivyoweza kubeba. Wakarundika nyama majumbani mwao zikawaozea
 
Back
Top Bottom