DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kesi ya Uhaini namba 26394/2025 inayowakabili washtakiwa 38 ambao walikamatwa kutokana na matukio yaliyotokea Oktoba 29, imeahirishwa mpaka Disemba 3, 2025.
Shauri hilo leo lilikuwa linasikilizwa kwa njia ya mtandao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki ambapo washtakiwa hawakufikishwa mahakamani.
Hata hivyo upande wa Utetezi ukiwa na Mawakili 10 wakiongozwa na Sisty Massawe, Paul Kisabo na William Maduhu waliomba shauri hilo kuahirishwa na kupangiwa siku nyingine huku wakitaka washtakiwa waletwe mahakamani.
Pamoja na hayo iliibuka hoja mahakamani hapo juu ya kuongezwa kwa washtakiwa wanne katika hati ya mashtaka bila upande wa utetezi kujuzwa lakini pia mshtakiwa mmoja hakufikishwa mahakamani.
Hoja nyingine iliyohojiwa ni juu ya hali ya upelelezi ambapo jamhuri kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Baada ya majibizani ya kisheria ya pande zote mahakama imeagiza washtakiwa hao ambao wanashikiliwa katika gereza la Segerea kufikishwa mahakamani siku kesi itakakuja kwa ajili ya kutajwa.