Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mtuhumiwa
Upande wa Jamhuri katika kesi namba Cc 32444/24 inayomkabili Saleh Ayoub (39) mkazi wa Salasala Jijini Dar es Salaam ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Green Acres iliyopo maeneo ya Mbezi Beach Africana, Dar anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake (11) umesema kuwa unatarajia kuwa na mashahidi sita na kielezo kimoja kwenye kesi hiyo.
Kesi hiyo imesikilizwa Novemba 26, 2024, ambapo upande wa Jamhuri umewasilisha hoja kupitia Wakili Jaquline mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hawa Magesa.
Hata hivyo Mshtakiwa ameendelea kukana shtaka linalomkabili ikiwa ni baada ya Jamhuri kuiomba Mahakama kufanya marekebisho ya Hati ya Mashtaka iliyodaiwa kuwa na kasoro.
Kesi hiyo dhidi ya Mtuhumiwa Saleh anatetewa na Wakili Faraja Mangula ilianza kusikilizwa majira ya saa kumi na moja Jioni kuelekea saa 12 Jioni licha ya kuwa awali Mahakama ilitoa maelekezo kuwa itasomwa Saa tano asubuhi.
Kesi hiyo inayosikilizwa kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imeahirishwa mpaka Desemba 10, 2024 Saa 4:00 Asubuhi, ambapo kesi itakuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi.
Itakumbukwa mshtakiwa huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza siku moja baada ya mdau wa Jamiiforum.com kuhoji sababu za kutofikishwa mahakamani kwa watuhumiwa aliodai wanahusika na ukatili katika Shule ya Green Acres iliyopo Dar es Salaam.
Kujua ilipoanzia kesi hii, bofya hizi link:
~ Dar: Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti Mwanafunzi wake afikishwa Mahakamani
~ Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?
~ Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres anayetuhumiwa kulawiti Mwanafunzi yaahirishwa Mwezi mzima, Hakimu apata hudhuru
~ Watu 6 kutoa ushahidi Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake
~ Ushahidi wa Kesi ya Shule ya Msingi Green Acres, Saleh Ayoub anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake kuanza kutolewa Februari 6, 2025
~ Kesi inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti mtoto yaahirishwa hadi Machi 24, 2025