SI MBAYA KUULIZAAAA NIMEWAZAA TU KAMAAA HAYA MAKAMPUNI YA SIMU YANAKOPWA NA JESCA AMA BETTY GAFLAAAAAA MM NATUMIWA MSG NA HAYA MAKAMPUNI YA KUKOPAAAA ATI NDUGU AMA MFADHILI WA BETTY UNAOMBWA KUMJULISHA TAPELI AMETAKA KUTUTTAPELI SH ..... NAWAAAMBIAA NIMESHTUKAAA SANA SANAAAA GAFLAAA...
Pesa x wamekuwa wanabambikia watu madeni hovyo hovyo huku wakitishia kuwatangaza waliotishiwa mitandaoni waziri wa fedha aziangalie hizi kampuni ni sumu kwenye uchumi wa nchi
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Moses Nnauye amesema Serikali imetoa maeleko kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuwafuatilia na kuchunguza Watu wanaotumia taarifa za waliowakopesha Mtandaoni kwa lengo la kudhalilisha wakopaji. Amesema maelekezo hayo pia...
Hao Matapeli wasifungiwe ili waendelee kufanya kazi kwa sababu Mimi nishaanza kufanya Research yangu namna ya kuwapiga na kitu kizito na wasinifanye chochote...Research ikikamilika nikaweza kuwapiga mzinga Mrefu nitawapa namna...Ila BOT na TCRA chonde chonde msiwafungie saivi.
Binafsi sio tapeli ila nikiri kwamba niliamua kuwanyoosha hawa wakopeshaji wa mtandaoni baada ya mmoja wao kunichafua, Nilikuwa mkopaji mzuri wa app fulani jina nalihifadhi nikilipa walikuwa wananiomba nikope tena na tena basi kwangu ikawa kama mazoea kopa lipa Tabu na mateso vilianza pale...
Haiingii akilini kuwa serikali impe mtu kibali cha kukopesha wananchi wake ambapo malipo yanapaswa kufanyika ndani ya siku 5, 6 au 7 tu yakiwa na riba ya 35%. Kama serikali imekubali kazi za kampuni hizi na kubariki kisa kodi basi Watanzania hatuna serikali. Au vibali vyao viko safi tu mbele ya...
Waziri wa Fedha, Dr. Mwigulu Nchemba , tunaomba kujua huyu mtu ni nani hasa na je, BOT walimpa leseni ya kufanya hii biashara kihalali hapa nchini? Na kama ana leseni, basi Waziri Mwigulu hebu chunguza leseni ya huyu bwana kama imetolewa kwa njia halali hasa kutokana na riba wanazochaji, muda...
Kwa Niaba ya Wadau wananchi wa kawaida kabisa nadhani ni wakati sahihi wa kupazia sauti kadha hii ambayo imefumbiwa macho kwa muda mrefu na vyombo vyetu husika. Week chache zilizopita niliamua kuvalia njunga swala moja la mtu ambae alikua akidaiwa na App moja ya Mtandaoni ikiitwa *SUNN LOAN...
Uchunguzi wa kijasusi uliofanywa na BBC umegundua yafuatayo.
1) Mteja mtarajiwa hutumiwa meseji akiambiwa kwamba amechaguliwa kupata mkopo wa kiasi flani, hivyo afuate link ya ‘playstore’ ili ku-‘download’ na ku-‘install’ app ya kampuni husika.
2) Wakati wa ku-‘install’, ile app inakuomba ruhusa ya kuingia kwenye ‘contact list’ yako yote, ‘Photo gallery’ yote, ‘Messages’ zote, ‘call log’ yote! Halafu ndani ya dakika chache mkopo wako unaingia.
3) Riba za kampuni husika zinaenda kinyume na matakwa ya kisheria ya nchi husika, mfano ukikopa elfu 40, unaweza kuja kuambiwa ulipe laki 2 kama jumla ya mkopo na riba, hii ni mara 5 ya pesa uliyokopa, na ni kinyume cha sheria za mikopo za BOT.
4) Kampuni husika huwa hazina ofisi popote zaidi ya kuwepo mtandaoni tu, ila huwa inaajiri recovery unit huko vichochoroni na kuwapa training jinsi ya kufanya unyanyasaji/harassment kwa watu waliopitiliza kulipa.
- Hapa wanapitia contact zako zote na kuwatumia meseji kwamba wewe ni tapeli na kukuaibisha na kukufanya usiaminike tena kwao.
- Pia wanapitia meseji zako na kutafuta zile unazotumiana na mchepuko wako, kisha wanatishia kutuma namba ya mchepuko wako kwa mke wako, ambapo hutishia kuharibu na kusambaratisha maisha yako na kuvuruga familia yako. Hapa wanaweza kukublack mail uwalipe hata milioni 2 badala ya laki 2, ni ‘Extortion’ na ‘Intimidation’. Na hakuna kitu BOT wanaweza kufanya, ni TCRA ndio anaweza kufungua App hizo, ila nahisi wana mgao, kwahiyo wanagawana hizi ‘Extortions’.
- Wanapitia picha zako zote za Photo gallery yako na kutafuta zile ulizopiga ukiwa uchi, ukiwa na michepuko, au kama ni shoga unafanya kwa siri na wakakuta picha zako ukiliwa ndio umekwisha kabisa, maana watatuma hizo picha kwenye whatsapp ya baba mkwe, mama mkwe, baba, mama, dada, ndugu, marafiki nk. Huko India watu 60 wameshajiua, hapa Tanzania sijui, mwenye takwimu azilete. Ukitaka wasizitume picha unaweza ukaambiwa lipa milioni 10, wengi wamelipa kunusuru kuaibishwa. Imagine unalipa milioni 10 kwa mkopo wa elfu 20.
Uchunguzi umebaini kwamba muhusika mkuu yupo Hongkong, ambapo ofisi yake inajina lingine kabisa, na hupokea mapato ya ‘unyonyaji’ ambayo hugawana na mamlaka ya usimamizi wa nchi husika, mfano kwa hapo bongo kuna TCRA.
MWISHO.
- Wote mliokopa kaeni kwa akili sana, usije ukapiga picha ya ajabu hata baada ya kuwa umekopa wakati hiyo app bado ipo, au ukatuma meseji kwa mchepuko, au ukaweka simu karibu wakati wa tendo, maana wana hadi live access ya Camera yako bila wewe kujua, wanakusikiliza na wanakurekodi mwanzo mwisho.
- Hizi kampuni hazina uwezo wala eligibility ya kukupeleka mahakamani au popote pale endapo hutolipa, bali wanatumia tu tactics za kukuaibisha na kukudhalilisha hadi ulipe, usipo lipa ndio basi, hawana cha kufanya zaidi ya kuharass ndugu na marafiki zako.
Serikali imetoa wito kwa watoa huduma za kifedha nchini kufuata sheria na taratibu za huduma za Fedha ikiwemo kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ili kuhakikisha huduma hizo zinatolewa kwa ufanisi bila kuwaumiza na kuwadhalilisha wanufaika na hatimaye kukuza uchumi wa nchi. Akizungumza...
Kwa ufupi ni mambo ya hovyo sana, watu wanaweza kuchukua taarifa zako na kuzisambaza mtandaoni!. Watu wanasema dawa ya deni kulipa ila si kwa kudhalilishana pale mtu anaposhindwa kulipa. Ndugu yangu amefadhaika sana baada ya kampuni moja ya mtandaoni kumsambazia jumbe za kumdhalilisha. Kweli...
Hiyo inawezekana, ila playstore au itunes wakigundua coding yako ina kitu kama hicho, wanaiondoa app yako dukani muda huo huo, issue ni kuireport vya kutosha
Wiki iliyopita si ni li kopa pesa x ikawa natakiwa nirejeshe pesa nusu mara mbili ndani ya siku 14 yani kila baada ya siku Saba nirejeshe. Sasa rejesho la kwanza lilikuwa jana ila cha moto nakipata! Aloo najuta, sio kwa meseji hizo ninazotumiwa! Kwani nisipolipa watanifanya nini tofauti na...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.