Watu 7 wapoteza maisha na 10 wajeruhiwa kufuatia ajali ya gari Wilaya ya Handeni. Msando atoa onyo kwa madereva wazembe!

Watu 7 wapoteza maisha na 10 wajeruhiwa kufuatia ajali ya gari Wilaya ya Handeni. Msando atoa onyo kwa madereva wazembe!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando, amethibitisha kutokea kwa ajali leo asubuhi, saa 12, katika eneo la Michungwani, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni. Ajali hiyo, iliyohusisha lori na Coaster, imesababisha vifo vya watu 7 na kujeruhi wengine 10.

segera.png

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Wilaya amesema: "Naendelea kuwasisitiza sana madereva kuwa makini na kuchukua tahadhari. Ajali hii sababu ni UZEMBE WA DEREVA."

Msando.png

Kutokana na uzembe unaojirudia, Msando amesema: "Nimemuelekeza OCD atakayekiuka sheria ya barabarani eneo la Handeni tutampandisha Mahakamani na kuomba adhabu ya kifungo."

Ameongeza kuwa wale wanaopiga simu kuomba msaada kwa madereva wao wakikiuka sheria wasitegemee msaada wowote. "Hakuna msaada zaidi ya kukaa lock up kwa mujibu wa sheria na kupandishwa kizimbani," alisema.

Msando pia ametoa onyo kali kwa madereva: "Ukifika kijiji cha Manga, Wilaya ya Handeni, ewe dereva usipofuata sheria za usalama barabarani usitulaumu. Ajali nyingi zinaepukika."

Kwa upande wa abiria, Mkuu wa Wilaya amewahimiza kuchukua hatua wanapogundua dereva anaendesha kiholela. "Acheni kukaa kimya wakati dereva anaendesha hovyo aidha shuka, utarejeshewa nauli yako na toa taarifa kwa Jeshi la Polisi tudhibiti huu uzembe,"

 
Barabara kutoka Tanga mjini Mheza - korogwe - handeni ni nyembamba sana...... Maboresho yanahitajika
 
Jinamizi la ajali zinazochukua uhai wa watu wengi nchini Tanzania kuelekea mwishoni mwa mwaka linazidi kushika kasi ambapo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, DC Alberto Msando hii leo Desemba 24, 2024 anaripoti.

“Leo asubuhi mida ya saa 12 imetokea ajali iliyohusisha Lori na Coaster. Ajali hiyo imetokea eneo la Michungwani, Kata ya Segera, Wilaya ya Handeni. Watu 7 wamepoteza maisha na 10 wamejeruhiwa. Naendelea kuwasisitiza sana madereva kuwa makini na kuchukua tahadhari.

Ajali hii sababu ni uzembe wa dereva. kwa sababu ya kujirudia rudia kwa uzembe nimemuelekeza OCD atakayekiuka sheria ya barabarani eneo la Handeni tutampandisha Mahakamani na kuomba adhabu ya kifungo.

Kwa ambao mmekuwa mkipiga simu kusaidiwa madereva wenu wakikiuka sheria za barabarani wala msisumbuke: hakuna msaada zaidi ya kukaa lock up kwa mujibu wa sheria na kupanda kizimbani Ukifika kijiji cha Manga Wilaya ya Handeni ewe Dereva usipofuata sheria za usalama barabarani usitulaumu. Ajali nyingi zinaepukika.

Na abiria, acheni kukaa kimya wakati dereva anaendesha hovyo aidha SHUKA utarejeshewa nauli yako na toa taarifa kwa Jeshi la Polisi tudhibiti huu uzembe

segera.png

Watu wanane wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea alfajiri ya leo kwenye kwenye Barabara Kuu ya Segera - Chalinze katika kitongoji cha Kwachuma wilayani Handeni.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi ajali hiyo imehusisha lori lenye namba za usajili T.780DRL aina ya Sharkman lililokuwa likielekea Dar es Salaam na gari aina ya Toyota Coaster lenye namba za usajili T.906 DPJ lililokuwa likielekea mkoani Kilimanjaro.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Toyota Coaster kushindwa kulimudu gari lake na kusababisha gari kuhamia upande wa pili wa barabara na kugongana na lori hilo.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Magunga, wilayani Korogwe kwa ajili ya matibabu na miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.
 
Madereva wa hizi coaster za special hire huwa hawalali,

Hiyo ajali sababu itakuwa uchovu na usingizi
 
Kwenye gari binafsi ajali ikitokea watu wana sema hawana uzoefu wa safari ndefu
Anyways RIP
 
Back
Top Bottom