Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace lenye namba za usajili T 249 BWT inayotumika kubeba magazeti iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP. Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha cha Mahenge Wilayani Kilolo Mkoani Iringa majira ya saa 10 alfajiri.

Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kupinduka.

Mbeya.jpg
 
Ina maana Dar walitoka saa ngapi hawa jamaa? 😎

Nahisi hii ajali ni aidha dereva alisinzia tokana na uchovu! Kuna wakati mwili unakataa kabisa sema alijitahidi kufosi afike point ambayo hakuweza kuifikia.
 
Hawa watu wa magazeti na posta wanajionaga wajanja sana kwenye mwendo kasi na huwa wanajisifia....
Wasipobadilika watakwisha.
Halafu hii staili ya usafirishaji wa magazeti mbona ya kizamani sana...?....
Mkuu waambie njia mpya wapate kujua
 
Back
Top Bottom