Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace lenye namba za usajili T 249 BWT inayotumika kubeba magazeti iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP. Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha cha Mahenge Wilayani Kilolo Mkoani Iringa majira ya saa 10 alfajiri.

Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kupinduka.

Kama saa 10 alfajiri alikuwa Mahenge Mbeya angefika saa 9 alasiri! Magazeti angemuuzia nani! Ni wazi aliamua kunyoosha mguu mpaka kwenye redieta.
 
Miaka ya nyuma nimepanda gari ya gazeti toka mbeya tupo kitonga dereva ananiambia nimpigishe stori usingizi usimpitie......wapumzike salama walotangulia
Weee acha hizo! Naona unakwenda kinyumenyume, gari za magazeti hutoka Dar kwenda Mbeya.
 
Kama saa 10 alfajiri alikuwa Mahenge Mbeya angefika saa 9 alasiri! Magazeti angemuuzia nani! Ni wazi aliamua kunyoosha mguu mpaka kwenye redieta.
Kutoka Dar hadi hapo Mahenge ni 413Km kama hilo gari lilitoka saa 6 usiku jamaa ametumia roughly masaa 4, na kutoka hapo Mahenge hadi Mbeya ni 403 Km saa mbili asubuhi jamaa alikua anafika Mbeya.. ila alikua spidi kali sana
 
Bado kuna watu wanapanda hizo chinja chinja wakati siku hizi kuna new force ya usiku
Sio kweli bhana New Force hana gari ya usiku,zaidi zaidi kuna coaster za hakuna kulala tu
 
Kama saa 10 alfajiri alikuwa Mahenge Mbeya angefika saa 9 alasiri! Magazeti angemuuzia nani! Ni wazi aliamua kunyoosha mguu mpaka kwenye redieta.
Iringa wanapita kuanzia saa 11 mpaka saa1 asubuhi. Mbeya saa around saa 3 hv.
 
Hiace ina mzigo wa magazeti wakutosha na bado imebeba watu 12. Na bado inaendeshwa mwendo wa kuwahi kuzimu.

Mambo mengine tunajitakiaga wenyewe.
[emoji23][emoji23][emoji23]
Usinichekeshe bwana wakati habari ni ya huzuri.

Mungu awaponye majeruhi
Na azipumzishe roho za marehemu mahali pema[emoji120]
 
Back
Top Bottom