Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace lenye namba za usajili T 249 BWT inayotumika kubeba magazeti iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP. Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha cha Mahenge Wilayani Kilolo Mkoani Iringa majira ya saa 10 alfajiri.

Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kupinduka.

Gari limepata ajali Iringa iweje uandike Mbeya ili ionekane mbeya ajali nyingi zinatokea huko
 
Ifikie mahala jamaa wangebadili mfumo tu kusafirisha gazeti kwenye hiace sio safe kabisa. Bora hata wangenunua wagons za kijerumani au gari za chini ambazo ziko stable zaidi with powerful engines!
Ubahili na kutaka faida kubwa ndio kinasababisha hayo yote, usikute gari yenyewe ilikuwa mkangafu
 
Gazeti likishakamilika linatakiwa kutumwa kwenye printing machine.......
ambapo kimsingi kila mkoa zinapaswa kuwepo
haya mambo ya kusafirisha magazeti yamepitwa na wakati kwa kweli

yaani mtu kama musiba awe na mashine kila mkoa!!!kwa hela ipi!!

ujue tatizo la tz ni,urasimu na ukiritimba.
hatupendi sana kuwa waaminifu katika miongozo tunayojiwekea,ukute kanuni ziko wazi,kwamba hakuna kuanzisha kampuni ya kuchapa magazeti kama huna uwezo moja na mbili,lakini watu wanafungua kampuni hizi ili ndipo wapate hela.
yale yale kama katika kampuni za ulinzi,matokeo yake kampuni isipolipwa mwezi mmoja wafanyakazi wanakosa mishahara miezi mitatu.
 
Kuna siku nimepata dharula inabidi niende Mbeya. Nimefika Kibo mida ya saaa 3 usiku nakutana na Noah ya magazeti. Dereva anavuta bangi na ana konyagi mkononi. Nikagoma kupanda, kifo hakizuiliki lakini kuchagua kifo siko tayari.
 
Poleni sana Mbeya na viunga vyake. Mungu awafute machozi na kuwaponya majeruhi
 
Ifikie mahala jamaa wangebadili mfumo tu kusafirisha gazeti kwenye hiace sio safe kabisa. Bora hata wangenunua wagons za kijerumani au gari za chini ambazo ziko stable zaidi with powerful engines!
Unasema?!
 
Kwa hyo Leo huko mbeya watu hawajasoma magazeti. Magazeti yanatengenezwa saa ngapi,yanapakiwa saa ngapi, yanatoka dar saa ngapi, na yanafika mbeya saa ngapi?
Hata mimi hii hunipa kuzunguzungu sana. Gazeti huwa tayari saa 5 usiku lakini Mbeya hadi saa 12-1 asubuhi tayari watu wanasoma gazeti. Huo mwendo ndiyo Mungu nisaidie
 
That could have been me in that car. Nimezipanda sana hizi gari. Sana. Nimeshakaa kwenye buti la hizi hiace mara mbili kutoka Mbeya kurudi Dar. Nina namba za simu za madereva 6 tofauti wa hizi Gari. Naogopa hata kuwauliza, si ajabu mmoja wao alikuwa humo.

Mungu ni mwema kwakweli, maana tunapotoka ni mbali.
 
Daresalamaa mpaka mbeya ni takribani masaa 13.
Hata mimi hii hunipa kuzunguzungu sana. Gazeti huwa tayari saa 5 usiku lakini Mbeya hadi saa 12-1 asubuhi tayari watu wanasoma gazeti. Huo mwendo ndiyo Mungu nisaidie
Screenshot_20211213-190245.jpg
 
Ifikie mahala jamaa wangebadili mfumo tu kusafirisha gazeti kwenye hiace sio safe kabisa. Bora hata wangenunua wagons za kijerumani au gari za chini ambazo ziko stable zaidi with powerful engines!
Zamaniii nilikua napanda gari za magazeti ya mwananchi,aiseee jamaa wanakimbiaaaaaa hakuna mfano, dar mnaondoka saa 4 au 5 usiku mbeya mnafika saa 12.30 asubuhi,saa 5 wanageuza saa 3 wapo dar saa 5 wanageuza mbeya tena
 
That could have been me in that car. Nimezipanda sana hizi gari. Sana. Nimeshakaa kwenye buti la hizi hiace mara mbili kutoka Mbeya kurudi Dar. Nina namba za simu za madereva 6 tofauti wa hizi Gari. Naogopa hata kuwauliza, si ajabu mmoja wao alikuwa humo.

Mungu ni mwema kwakweli, maana tunapotoka ni mbali.
Mi namba za madereva nilizonazo nmecheki online wote last seen ni mchana wa leo so wote wapo hai
 
Back
Top Bottom