Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Miaka ya nyuma nimepanda gari ya gazeti toka mbeya tupo kitonga dereva ananiambia nimpigishe stori usingizi usimpitie......wapumzike salama walotangulia
Italy siku jamaa wamenichukua Airport Fiumicino twende Rome tunaenda dereva analala njiani tunamzindua.
Story zote lakini unaona kabisa huyu kazidiwa ikabidi tusimame shell japo apige kahawa.
Tumeondoka kuna msela katupita na Ferrari moto bati ,jamaa kataka amfukuzie nikamwambia tulia twende taratibu tutamkuta tu huko mbele.
Baada ya sa 1 tu tumekuta Ferrari ile nyanganyanga ambulance kibao na maiti zinafungwa kwenye mabegi.
Alikua na demu yule jamaa.
Tukapita nikamwambia si nilisema tutawakuta.
Jamaa "duh kweli aisee ila washakufa"
Ikawa ndo hivyo tembea polepole tutafika tu.
Sasa alikua tu anawai kuzimu.
 
Kuna siku nimepata dharula inabidi niende Mbeya. Nimefika Kibo mida ya saaa 3 usiku nakutana na Noah ya magazeti. Dereva anavuta bangi na ana konyagi mkononi. Nikagoma kupanda, kifo hakizuiliki lakini kuchagua kifo siko tayari.
Mimi nilipandaga moja ilikuwa inaelekea mbeya
Tulipanda na mwenzangu tulikuwa tunawahi
Boda tunduma,mwenzangu alishuka moro
Mm nlimaliza safari lkn cha moto nlikiona
Nkasema sipandi tena
Bora ucheleww lkn ufike safari yako

Ova
 
Ifikie mahala jamaa wangebadili mfumo tu kusafirisha gazeti kwenye hiace sio safe kabisa. Bora hata wangenunua wagons za kijerumani au gari za chini ambazo ziko stable zaidi with powerful engines!
Mkuu unatafuta kesi na manazi wa kijapan ,wakina mr Toyota watakuuliza TOYOTA HANA MAGARI yenye stability kuliko mjerumani[emoji848] ngoja waje sasa na land cruiser mkonga
 
Hiace ina watu 12 na mzigo wa magazeti.

Kwa nini wasitumie gari dogo tu kama mzigo wenyewe ni mdogo au hao abiria ni sehemu ya biashara ya kampuni yenyewe?

Watumie hata brevis au Crown Athletes.
 
Zamaniii nilikua napanda gari za magazeti ya mwananchi,aiseee jamaa wanakimbiaaaaaa hakuna mfano, dar mnaondoka saa 4 au 5 usiku mbeya mnafika saa 12.30 asubuhi,saa 5 wanageuza saa 3 wapo dar saa 5 wanageuza mbeya tena
Hayo magari haunipandishi hata kwa bakora
 
Sio kweli bhana New Force hana gari ya usiku,zaidi zaidi kuna coaster za hakuna kulala tu
Ipo mkuu..inatoka shekilango sati na nusu jion tunduma wanafika saa kumi alfajiri..mimi nimepanda wiki iliyopita.tena usiku kuna abiria wengi sana
 
Hizi gari mwendo wake ni hatari. Nimeshapanda mara kadhaa kutoka dar kwenda mbeya. Mara ya mwisho nimepanda mwezi wa 9 tulitoka kibo saa 5 na nusu usiku saa 1 tupo uyole.
 
Zamaniii nilikua napanda gari za magazeti ya mwananchi,aiseee jamaa wanakimbiaaaaaa hakuna mfano, dar mnaondoka saa 4 au 5 usiku mbeya mnafika saa 12.30 asubuhi,saa 5 wanageuza saa 3 wapo dar saa 5 wanageuza mbeya tena
Hio distance hapana yani saa 4 usiku ufike mbeya saa 12.30am? Hio gari inatembea speed gani ?
 
Zamaniii nilikua napanda gari za magazeti ya mwananchi,aiseee jamaa wanakimbiaaaaaa hakuna mfano, dar mnaondoka saa 4 au 5 usiku mbeya mnafika saa 12.30 asubuhi,saa 5 wanageuza saa 3 wapo dar saa 5 wanageuza mbeya tena
Sasa wanalala saa ngp
 
Hizi gari mwendo wake ni hatari. Nimeshapanda mara kadhaa kutoka dar kwenda mbeya. Mara ya mwisho nimepanda mwezi wa 9 tulitoka kibo saa 5 na nusu usiku saa 1 tupo uyole.
Yaani hata MTU wa anayekwenda Arusha mmempita.nyie mmeshafika mbeya.[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom