Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Awa madereva wanakuwa wazima kweli
Wanakuwaga wamefyatuka kidizaini yani af wengi ni vidingi vya makamo. Mzee wa kichaga sikuhio kampa chuma utingo wake ye akalala anamwambia endesha gari dogo alikuwa analemba jamaa alipoamka akarudi mtamboni akaanza kuendesha kweli sasa!
 
Kuna siku nilikua natoka Dar kuelekea Makambako usiku kama saa 5 hivi.Nilitafuta it pale Chang'ombe nikakosa kuna jamaa akanipeleka pale Keko kwenye magazeti nidandie chuma zao hadi Makambako,,bahati nzuri karibia zote zilikua zimejaa so sikufanikiwa nikarudi kubahatisha it pale mataa ya Chang'ombe.

Tuko wawili tu mimi na dereva,jamaa kaanza kusinzia toka Tazara nikaona hapa leo kuna kifo.Huwezi amini saa 11 alfajiri tumeingia Makambako na hapo njia nzima alikua anasinzia,pale Kitonga kuna roli ilikuja mbele yetu speed na jamaa wa it kaipeleka kule kule kahama upande wetu nikamstua ndio akarudi upande wake.Tulikua tunaiva siku ile sitosahau
 
Wangeanza kuacha njia za kijima za kusafirisha magazeti ruti ndefu. Wenye magazeti mbalimbali wakishirikiana wanaweza kuwa na printing presses kila kanda.
Haya ndiyo tunaita mawazo mbadala ambayo waafrika wengi hawataki kuyatumia. Tena angweza kuwepo mtu binafsi anaprint hayo magazeti ktk hizo kanda.
 
Mimi nilipandaga moja ilikuwa inaelekea mbeya
Tulipanda na mwenzangu tulikuwa tunawahi
Boda tunduma,mwenzangu alishuka moro
Mm nlimaliza safari lkn cha moto nlikiona
Nkasema sipandi tena
Bora ucheleww lkn ufike safari yako

Ova
Mimi sijawahi kusogelea hizo gari, nilijitahidi tu kupanda fuso la Posta... nalo linatembea balaa lakini sio kama hao vichaa
 
Ilikuwa mchana au usiku?
Ilikua mchana baada ya kupigiwa simu ya mchongo huku dar

Jamaa alikua anapiga gia za kibabe, overtake za hatari hatari lakini yeye ndio kwanza wala hajari
Nikasema lolote na liwe kwani kufa kitu gani, uzuri likipiga mziga hakuna kiumbe kitachotoka hai. Acha tufe tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu hapo mbona wameendesha mwendo wa kistaarabu

Unaambiwa chombo kikiwa kinapeleka magazeti, ndio unaweza kuomba poo ata msitu wa mdaula wakushushe tu[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Eti msitu wa mdaula wakushushe[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hio distance hapana yani saa 4 usiku ufike mbeya saa 12.30am? Hio gari inatembea speed gani ?
Niamini mimi,zilikua Isuzu pickup,gia sita spidi 240 kama hilux D4D,jamaa akikanyaga gia rotation inafika sita ndio anachange ingine,spidi yao ni hatari mnooo nimepanda zaidi ya mara 10,cha pekee zaidi jamaa wanajua kutunza mafuta aisee diesel wanaiuza inayobaki ndio wanatembelea gia namba 5 na 6 tuuu,ila roho mkononi,tukitoka dar saa 4 usiku mikumi anapita saa 7 kamili yaani jaribu siku 1 ikiwa bahat yako utafika salama
 
Hio siamini mkuu mbeya mbali bana we! Labda kama wanalazaga mshale 180kph safari nzima
Sasa unadhan wanatembea ngapi?? Mda mwingi mshale upo kwenye 200 km/h hizi nazungumzia zile Isuzu za Mwananchi tena iyo ni mwaka 2013 na 2012 ukooo
 
Inashangaza kwa sababu mtu hata uwe na speed kiasi gani huwezi toka dar to arusha bila masaa 5! Hapo brake ni za matuta tu full kibati lazma uta average kwenye 130KPH

Distance: 624.3km
Average Speed: 130Kph
Time. ?
Formula: Time =Distance/speed


Ans: 4.8hrs ~ 5hrs

Dar-Chuga on average speed of 130KPH takes 5hrs.
Mzeee hujakutana na wehu wa magazeti bado,zamaniii nilikua napenda sana racing kuna mtu tuliwekeana dau kutoka ubungo mataa kabla ya hilo daraja to mwenge 25 seconds nikabisha haiwezekani aisee nikaambiwa ingia kwenye gari saa 5 usiku racing ikaanza hatari na nusu jamaa nililia kwa kihoro cha kufa kabisaaa na alitumia 23 seconds.
Hela yangu alikula na akaenda chini ya muda alioahidi sitak hata kusikia kujaribu tenaaa baada ya washikaj zangu kadhaa kufariki kwa maajali haswa alteza ziliwamaliza sanaaa
 
Ina maana Dar walitoka saa ngapi hawa jamaa? [emoji41]

Nahisi hii ajali ni aidha dereva alisinzia tokana na uchovu! Kuna wakati mwili unakataa kabisa sema alijitahidi kufosi afike point ambayo hakuweza kuifikia.
Magazeti yanatoka saa 4 usiku.

Saa 5 wanaanza safari. Kufika iringa muda huo ni reasonable.
 
Back
Top Bottom