Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu 9 wafariki dunia katika ajali iliyohusisha Hiace inayopeleka Magazeti Mbeya

Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace lenye namba za usajili T 249 BWT inayotumika kubeba magazeti iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP. Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha cha Mahenge Wilayani Kilolo Mkoani Iringa majira ya saa 10 alfajiri.

Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kupinduka.

Kwanini magazeti hayapelekwi Mbeya kwa ndege?
 
Siku hizi wanasafirisha kwa hiace Sasa Kona na speed hiace itahimili vipi zile Nissan vipii wameziacha sipati picha hizo zingekuwa pesa tusingeona karatasi happy🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
hivi haiwezekani kuweka printing house mfano Mbeya ikawa inaprint kwaajili ya mikoa ya kanda ya juu kusini? au mtaji wake ni ghari sana? haiwezekani hadi leo hii tutegemee gazeti litoke Dar ndo lije hapa Mbeya tena kwa kuchelewa.
Mkùu inawezekana ila makampuni hayataki kuwekeza kwenye teknolojia. Kuna remote printing na hata printing via satellite ambapo gazeti linapotoka Dar basi linatoka sambamba katika sehemu zote linapotakiwa litoke. Issue hapa ni kujali faida kuliko maisha ya mtu.
 
Niamini mimi,zilikua Isuzu pickup,gia sita spidi 240 kama hilux D4D,jamaa akikanyaga gia rotation inafika sita ndio anachange ingine,spidi yao ni hatari mnooo nimepanda zaidi ya mara 10,cha pekee zaidi jamaa wanajua kutunza mafuta aisee diesel wanaiuza inayobaki ndio wanatembelea gia namba 5 na 6 tuuu,ila roho mkononi,tukitoka dar saa 4 usiku mikumi anapita saa 7 kamili yaani jaribu siku 1 ikiwa bahat yako utafika salama
'Jaribu siku moja ikiwa bahati yako utafika salama'

Yani ajaribu sumu kwa kuilamba[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jeshi la Polisi wameonesha udhaifu mkubwa sana kwa kushindwa kutoa ufafanuzi wa 5Ws juu ya wahusika wa ajali hiyo.

Ina maana hakuna simuvitambulisho,nyaraka,n.k zozote ambazo zingewawezesha kutoa taarifa sahihi za wahanga wa ajali hiyo?inamaana hata majeruhi nao hawakuweza kujitambulisha?

Inasikitisha sana utoaji taarifa wa namna kwani kuna mwenzetu amefariki katika ajali hiyo lakini tumekuja kumpata baada ya siku mbili tena kwa mzazi wake kujiongeza kwa kufika Iringa hospitalini na kukuta maiti ya mwanae polisi wametulia tu.

Jeshi la polisi jirekebisheni huo siyo utoaji taarifa wa kiueledi tumewachoka!!!!!
 
Daaaaahhh wadau wamekata moto katika harakati za kutafuta ugali
 
Jana nacomment huu uzi kumbe ajali imeondoka na classmate wangu aisee, leo ndo tunapata taarifa za msiba baada ya familia yake kuanza kumtafuta maana dar hayupo na mbeya hayupo na simu yake imepigwa kapokea msamaria mwema anayeishi eneo ambalo ajali imetokea.
Duuh poleni sana mkuu
 
Kwa hyo Leo huko mbeya watu hawajasoma magazeti. Magazeti yanatengenezwa saa ngapi,yanapakiwa saa ngapi, yanatoka dar saa ngapi, na yanafika mbeya saa ngapi?
Habari zenyewe zina umuhimu huo kweli?
 
Naomba kuuliza hivi haya magari ya kubeba magazeti yanaruhusiwa kubeba abiria pia?
 
Back
Top Bottom