Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Kwanini magazeti hayapelekwi Mbeya kwa ndege?Watu tisa wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya hiace lenye namba za usajili T 249 BWT inayotumika kubeba magazeti iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Jijini Mbeya.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP. Allan Bukumbi amesema ajali hiyo imetokea katika kijiji cha cha Mahenge Wilayani Kilolo Mkoani Iringa majira ya saa 10 alfajiri.
Kamanda Bukumbi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo gari hilo lilimshinda dereva kwenye kona na kupinduka.
Ukinywa dawa ya usingizi unakufa in advanceKama huna roho usipande au ukipanda kunywa dawa za usingizi
Ina maana hata kupublish mzigo ktk Northern strip yote...Arusha, Mwanza, Kagera, KLM, bado wanapata hasara?Jamana walijaribu lake zone wakaishia kufunga ofisi
Hapa ni zone mbili tofauti northern na lakezone ukiweka plant kwa kila zone ni hasara kubwaIna maana hata kupublish mzigo ktk Northern strip yote...Arusha, Mwanza, Kagera, KLM, bado wanapata hasara?
Mkùu inawezekana ila makampuni hayataki kuwekeza kwenye teknolojia. Kuna remote printing na hata printing via satellite ambapo gazeti linapotoka Dar basi linatoka sambamba katika sehemu zote linapotakiwa litoke. Issue hapa ni kujali faida kuliko maisha ya mtu.hivi haiwezekani kuweka printing house mfano Mbeya ikawa inaprint kwaajili ya mikoa ya kanda ya juu kusini? au mtaji wake ni ghari sana? haiwezekani hadi leo hii tutegemee gazeti litoke Dar ndo lije hapa Mbeya tena kwa kuchelewa.
'Jaribu siku moja ikiwa bahati yako utafika salama'Niamini mimi,zilikua Isuzu pickup,gia sita spidi 240 kama hilux D4D,jamaa akikanyaga gia rotation inafika sita ndio anachange ingine,spidi yao ni hatari mnooo nimepanda zaidi ya mara 10,cha pekee zaidi jamaa wanajua kutunza mafuta aisee diesel wanaiuza inayobaki ndio wanatembelea gia namba 5 na 6 tuuu,ila roho mkononi,tukitoka dar saa 4 usiku mikumi anapita saa 7 kamili yaani jaribu siku 1 ikiwa bahat yako utafika salama
Duuh poleni sana mkuuJana nacomment huu uzi kumbe ajali imeondoka na classmate wangu aisee, leo ndo tunapata taarifa za msiba baada ya familia yake kuanza kumtafuta maana dar hayupo na mbeya hayupo na simu yake imepigwa kapokea msamaria mwema anayeishi eneo ambalo ajali imetokea.
Habari zenyewe zina umuhimu huo kweli?Kwa hyo Leo huko mbeya watu hawajasoma magazeti. Magazeti yanatengenezwa saa ngapi,yanapakiwa saa ngapi, yanatoka dar saa ngapi, na yanafika mbeya saa ngapi?
Kwamba abira wanachanganywa na hayo magazeti au?Hiace ina mzigo wa magazeti wakutosha na bado imebeba watu 12. Na bado inaendeshwa mwendo wa kuwahi kuzimu.
Mambo mengine tunajitakiaga wenyewe.
Wanunue zile Mercedes-Benz Sprinter au VW Crafter kutoka pale CFAO.Wanunue Van za mjerumani zenye 260 KPH hizi hiace ni nyepesi sana yani!
Kama saa 10 alfajiri alikuwa Mahenge Mbeya angefika saa 9 alasiri! Magazeti angemuuzia nani! Ni wazi aliamua kunyoosha mguu mpaka kwenye redieta.
Hapanaaa ni kosaa kubeba abiriaNaomba kuuliza hivi haya magari ya kubeba magazeti yanaruhusiwa kubeba abiria pia?
Tatizo litakuwa ubahili hapoWanunue zile Mercedes-Benz Sprinter au VW Crafter kutoka pale CFAO.