sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Tanzania tuna makabila zaidi ya 120 na yote yana asili yake yalipotoka na mkataa kwao ni mtumwa.
Kumekuwa na ongezeko la watu siku hizi ambao wanazaliwa mjini na vijijini kwao hawakujui kabisa, mtu unaweza kumuuliza wewe ni mhaya, mnyakyusa, n.k wa wapi, anakwambia yeye ni mngoni, msukuma, n.k wa karakoo.
Je kwa watu wa mjini wanalichukuliaje swala la mjini kuwa asili yao bila kujua mizizi yao viijini?
Mfano mimi ni mtu naeishi mkoa flani wa nyanda za juu kusini na nimezaliwa huku lakini asili yangu ni mkoa wa Mara (mkoa huu unaongozea kwa makabila mengi hawapo wakuria pekee), siijui kikamilifu lugha lakini tangu zamani nikiwa mtoto tulikuwa tunaenda na mzee kila mwaka, hali hii menifanya nijuane kwa karibu na ndugu zangu, kujua mila na tamaduni kadhaa, ngoma, matambiko (kila kabila lina matambiko) n.k.
Kila mtu ana asili yake na mkoa wake.....na hao ndio wanaosumbua kutaja kabila zao. Hakuna mngoni, mkurya,mchaga,muhaya wa Arusha,Mbeya,Dar au Mwanza.
Mjenge utamadunu wa kurudi vijijni kwenu na mjuane na ndugu wa ukoo wako. Usijivunie mahali pasipo asili yako.
Muhimu: Hii inawahusu wale ambao makabila yao hayana sana changamoto ya kutupiana makombora ( guided missles ), hawa tunaweza kuwaelewa kwa kiasi