Sio kweli, Ayatollah khomeini tu ilihudhuhuriwa na watu million 10.2 na hiyo ni miaka ya 80 huko na hii ni according to guiness world record.
www.guinnessworldrecords.com
Ndio sembuse 2026? Kumbuka Iran ina watu zaidi ya 100m so hata 5% pekee ikihudhuria hiyo tayari ni zaidi ya hiyo million 2 uliyoandika.
Punguzeni chuki
Nipunguze chuki, kwani nina chuki gani? Hivi huyo aliyekwishakufa, maziko yake yakihudhuriwa na watu milioni 100 au milioni 1 au laki 1, inabadilisha kitu gani? Ingekuwa maziko yakihudhuriwa na watu wengi sana, anaamka, hapo tungekuwa na sababu ya kuweka idadi ya wahudhuriaji ni jambo la muhimu.
Record ya Dunia ni kuwa viongozi madikteta ndio maziko yao huhudhuriwa na watu wengi zaidi. Record ya mtawala ambaye maziko yake yalihudhuriwa na watu wengi zaidi Duniani, kabla ya huyo Ayatollah, ni Dikteta Stallin wa Russia, ambaye kutokana na uwingi wa watu, siku ya msiba wake, watu zaidi ya elfu 2 walikufa kutokana na kukanyagana. Na ndiye dikteta anayeshikilia record ya kuwaua raia wake wengi zaidi kuliko dikteta yeyote Duninai. Sababu kubwa ya dikteta, msiba wake kuhudhuriwa na watu wengi zaidi, ni pamoja na serikali yake ya kidikteta kuwalazimisha watu wahudhurie ili kuhadaa kuwa alikuwa anapendwa sana, na sababu nyingine ni baadhi ya watu ambao hawakuwa wanampenda kabisa, kushuhudia kuwa huyo mbaya wao, naye ameondoka. Hivyo huwezi kuwa na uhakika kiongozi dikteta msiba wake unapohudhuriwa na watu weni ni kwa sababu ya upendo, kulazimishwa au chuki.
Halafu hiyo idadi ya wairan milioni 100, ufahamu kuwa theluthi 2 ni watoto. Hivyo watu wazima unaongelea ni watu wasiozidi milioni 40. Hata kama hao milioni 40, wote wakahudhuria, haibadilishi chochote. Huyo amekwishaondoka katika Ulimwengu huu. Mtoto wake anachechemea huku akiwa amejawa na hofu ya kuuawa, kiasi cha kushindwa hata kuhudhuria maziko ya baba yake mzazi. Kuondoa mazingira yanayomfanya hata mtawala aishi kwa hofu, aishi kwenye mashimo kama panya, ni jambo muhimu na lenye msaada mkubwa zaidi kwa Wairan wote, kuliko hata idadi ya wahudhuriaji maziko ya mtawala aliyekwishauawa.
Jambo muhimu lingekuwa kuondoa mazingira yanayosababisha watawala kuuawa, wananchi kunyongwa hovyo. Ikumbukwe Iran ndiyo nchi inayoongoza Duniani kuwanyonga raia wake. Na hakuna mtawala wa Iran aliyewahi kuwanyonga wananchi wengi wa Iran zaidi ya huyo Ayatollah. Sasa alikowatanguliza wenzake, na yeye amefuata. Wenzake aliwatanguliza kwa kuwaua, na yeye amefuata kwa kuuawa.
Utimilifu wa yale maneno:
"Auaye kwa upanga hufa kwa upanga".