Watu elfu 95 wanakadiriwa kuishi na VVU Geita

Watu elfu 95 wanakadiriwa kuishi na VVU Geita

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkoa wa Geita unakadiriwa kuwa na watu elfu 95 wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU), huku wananchi wakihimizwa kupima afya zao mara kwa mara ili kufahamu hali zao.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Geita, Lucy Beda,i akimwakilisha Mkuu wa Wilaya katika maadhimisho ya Siku ya Afya Geita yaliyoandaliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).

Beda amesema upimaji wa afya unasaidia wananchi kutambua hali zao na kuchangia juhudi za kujikinga na maambukizi ya VVU.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita, Dkt. Omary Sukari, amesema takribani asilimia 80 ya wanaokadiriwa kuishi na VVU mkoani humo wamejitokeza kupima na kufahamu hali zao.

Naye , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, SACP Safia Jongo, amewahimiza wananchi kujitokeza kupima afya, huku GGML ikieleza kuendelea kushiriki katika shughuli za kusaidia watu wanaoishi na VVU na kampeni za uelimishaji.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU (NECOPHA), Leticia Molice, ameitaka sekta binafsi kuendelea kushirikiana katika mapambano dhidi ya VVU.

 
Miaka fulani nyuma mererani watu walipukutika
Sana,mpaka kuja kupewa elimu kuwekwa vituo vya afya huko,ndiko angalau kukatulia
Sehemu zenye madini wadada wengi huwa wanaenda kujiuza
Msumbiji yenyewe montepuez kulipofumuka huko ruby wauza nyapu wengi walitoka huku na kwenda huko,aiseee ngwengwee ilitembea huko na wengine walirudi nayo huku

Ova
 
Back
Top Bottom