Watu hawa watalia kwa uchungu kama watoto wadogo!

Watu hawa watalia kwa uchungu kama watoto wadogo!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Siku inakuja, siku mbaya ya kutisha, isiyofanana na siku nyingine yoyote. Siku ambayo ukweli wote utawekwa wazi, na kila mtu atasimama mbele ya kiti cha hukumu. Wachache watashangilia lakini wengi watalia kwa uchungu usioelezeka.

Watu hawa watalia na kusaga meno:

Wanaotenda maovu kwa siri wakidhani hakuna aonae
Wanaokataa kusamehe wengine
Wanaofurahia ulevi, uzinzi, uongo
Wasiotaka kutubu uovu wao na kuuacha

Wanaowachukia na kuwadhihaki watu wa Mungu
Wanaopenda pesa na mali kuliko kumpenda Mungu
Wanaoidharau Biblia na kupinga Neno la Mungu
Wanaodhani kifo ndio mwisho wa yote

Wanaokataa kuamini kuwa Yesu ni Mungu
Hata wanaosoma bandiko hili na kusema ni "ujinga"

Orodha ni ndefu, nisaidieni kuijazia...

Mathayo 13:47
"Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuri ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno."
 
Watu hao, wasipotubu sasa,
Watatengwa milele na uwepo wa Mungu
Watatupwa katika tanuru la moto
Watalia milele ne milele na kusaga meno kwa uchungu
Watajuta na kujilaumu kwanini walikataa kuokoka
 
Bado hujachelewa
Ukitubu dhambi zako na kuamini kuwa Yesu Kristo alikufa msalabani ili sisi tuokoke; na ukimpokea moyoni mwako na kukubali ayatawale maisha yako, utasamehewa na kuiepuka hukumu hiyo.(1 Yoh 1:9-10)

Fanya haraka, maana wakati huo umekaribia.
Ufunuo 22:10-12
“Akaniambia, Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, kwa maana wakati huo umekaribia. Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu sawasawa na alivyotenda."
 
Ukifuatisha sala hii ya toba kwa moyo wako wa dhati, utaokoka sasa hivi na kuikwepa hukumu ya moto wa milele. Omba hivi:
"Ee Mungu Baba, nimetambua mimi ni mwenye dhambi. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na nimeamua kuziacha kabisa. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuishi maisha ya utakatifu. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu, ujiunge nalo, watakupa msaada zaidi wa jinsi ya kuendelea kiroho. Ubarikiwe sana
 
Ulevi kumbe umo cc min -me

Sasa mama mchunga vipi kuhusu kufa mara ya pili Huwa selewagi mm kijukuu cha baba paroko cc secretarybird
Kufa mara ya pili ni hukumu ya mwisho ambapo mtu atatupwa katika ziwa la moto baada ya hukumu ya Mungu. Ni adhabu ya milele kwa wale wanaokataa kutubu na kuokoka.
Ufunuo 20:14-15
“Kisha mauti na kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hiyo ndiyo mauti ya pili, yaani, ziwa la moto. Na mtu ye yote asiyeonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika ziwa la moto.”
 
Siku inakuja, siku mbaya ya kutisha, isiyofanana na siku nyingine yoyote. Siku ambayo ukweli wote utawekwa wazi, na kila mtu atasimama mbele ya kiti cha hukumu. Wachache watashangilia lakini wengi watalia kwa uchungu usioelezeka.
Kwa nini walie na kusaga meno wakati walichagua kuwa walivyo? Wewe umechagua fungu lako, waache wakae na mafungu yao kama ndilo chaguo lao
 
Siku inakuja, siku mbaya ya kutisha, isiyofanana na siku nyingine yoyote. Siku ambayo ukweli wote utawekwa wazi, na kila mtu atasimama mbele ya kiti cha hukumu. Wachache watashangilia lakini wengi watalia kwa uchungu usioelezeka.

Watu hawa watalia na kusaga meno:

Wanaotenda maovu kwa siri wakidhani hakuna aonae
Wanaokataa kusamehe wengine
Wanaofurahia ulevi, uzinzi, uongo
Wasiotaka kutubu uovu wao na kuuacha

Wanaowachukia na kuwadhihaki watu wa Mungu
Wanaopenda pesa na mali kuliko kumpenda Mungu
Wanaoidharau Biblia na kupinga Neno la Mungu
Wanaodhani kifo ndio mwisho wa yote

Wanaokataa kuamini kuwa Yesu ni Mungu
Hata wanaosoma bandiko hili na kusema ni "ujinga"

Orodha ni ndefu, nisaidieni kuijazia...

Mathayo 13:47
"Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya samaki wa kila namna; hata lilipojaa, walilivuta pwani; wakaketi, wakakusanya walio wema vyomboni, bali walio wabaya wakawatupa. Ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia; malaika watatokea, watawatenga waovu mbali na wenye haki, na kuwatupa katika tanuri ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno."
Wezi wa kura
Wauaji na watekaji
Wafiraji
Orodh ni ndefu kwa kweli mtumishi.
 
Wezi wa kura
Wauaji na watekaji
Wafiraji
Orodh ni ndefu kwa kweli mtumishi.
Kwakuwa neema bado ipo, tusichoke kuwaambia hivi: ""Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache."
(Mt 7:13-14)

Yamkini baadhi yao watachomoka kutoka katika orodha hiyo ndefu.
 
napenda sana kusikia neno la MUNGU na mahubiri ya watumishi wa MUNGU.
Ombi: Setfree Mchungaji wa kondoo wa bwana, naomba uwe unatuhubiria kila siku asubuhi.
Hongera sana, ndugu yangu Emily magnus kwa kuchagua fungu jema. Kuhubiri kila siku naweza. Hata hivyo agizo la Yesu ni kwamba tunatakiwa kuhubiri ulimwenguni pote. Nikihubiri hapa hapa JF tu, ni vigumu kuufikia ulimwengu wote. Hivyo nahitajika kwenda maeneo mengine ili wengine nao wasikie habari njema.

Je, umeokoka au bado? Je, unayatendea kazi mahubiri uliyosikia kwangu?
Yakobo 1:22-25
"Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo. Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake."
 
Back
Top Bottom