#COVID19 Watu karibu 700 wafariki kwa COVID-19 Ujerumani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Watu 698 wamekufa kutokana na ugonjwa wa COVID-19 kwa muda wa saa 24 zilizopita nchini Ujerumani, hii ikiwa ni kulingana na taasisi ya Robert Koch inayoshughulikia magonjwa ya kuambukiza nchini humu.

Idadi hiyo ni ya pili kwa ukubwa kurekodiwa kwa siku moja tangu mripuko wa maradhi hayo kuwasili Ujerumani. Ujerumani pia imerekodi visa vipya vya maambukizi ya corona 26,923 katika muda wa saa 24 zilizopita, ilikiwa ongezeko la visa 48 ikilinganishwa na siku iliyotangulia. Kwa ujumla, Ujerumani ambayo tangu Jumatano imeimarisha masharti ya kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya corona, imepoteza watu 24,125 kwa maradhi ya COVID-19.

Huku hayo yakiarifiwa, mawaziri wa afya katika majimbo yote 16 ya Ujerumani wanakutana kukamilisha mipango ya kuanza kutoa chanjo ya ugonjwa huo kote Ujerumani kuanzia tarehe 27 mwezi huu wa Desemba.Wakati huo huo, taarifa za hivi punde zimearifu kuwa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutwa na mambukizi ya virusi vya corona.
 
inamaana mpaka sasa wazungu hawataki kutoa chanjo tu duh
[emoji1787][emoji1787]naona awam hii kimewarudia sio Kama walivo fanya kwa HIV enzi hizo

giphy.gif
 
Taifa letu linajifunza nini kutokana kupamba moto wa Corona huko Ulaya na Merikani katika majira haya ya baridi katika Mataifa hayo - mambo yanavyo elekea Dunia inakumbwa na COVID-19 katika phase ya pili - je,Serikali yetu pamoja na wizara ya afya na wizata ya utalii wamejipangaje kukabiriana na phase two ya COVID-19 ambayo italetwa na watalii na wagine kutoka mataifa ya Ulaya na Merikani - tusipo kuwa makini ungonjwa huu utalikumba Taifa letu kwa mara ya pili, this time around could be worse - God forbid.
 
Acha woga wewe,Mungu yuko pamoja nasi...
 
Huku sisi ni majira ya joto...moto mchubuyu kila mtu ashinde mechi zake
 
Taifa letu linajifunza nini kutokana kupamba moto wa Corona huko Ulaya na Merikani katika majira haya ya baridi katika Mataifa hayo - mambo yanavyo elekea Dunia inakumbwa na COVID-19 katika phase ya pili - je,Serikali yetu pamoja na wizara ya afya na wizata ya utalii wamejipangaje kukabiriana na phase two ya COVID-19 ambayo italetwa na watalii na wagine kutoka mataifa ya Ulaya na Merikani - tusipo kuwa makini ungonjwa huu utalikumba Taifa letu kwa mara ya pili, this time around could be worse - God forbid.
Unazungumzia watalii kuja na kutuletea corona kwani ile corona iliyoletwa na yule mdada wa kitanzania akitokea nje huko iliishia wapi?
 
kabla ya covid ujerumani walikua wanakufa watu wangapi kwa siku?? hospitali zote
Mambo hayo ndio nilikuwa nayaona huku Tz kipindi kile wanatangaza vifo vya corona unakuta kila aliyekufa na corona utasikia marehemu alikuwa na maradhi mengine pia,naukiangalia hayo maradhi mengine ndio yale yale ambayo hutuondoa kwa wingi kila siku.
 
kabla ya covid ujerumani walikua wanakufa watu wangapi kwa siku?? hospitali zote
Huenda walikua wanakufa zaidi ya hao, ila si kwa sababu ya ugonjwa mmoja kama Corona. Hapo ndio hofu inapokuja
 
Poleni sana wazungu!! Huku kwetu futa limegonga mwamba baada ya kutunyoosha mwezi wa nne mpaka wa sita 2020.
 
Huenda walikua wanakufa zaidi ya hao, ila si kwa sababu ya ugonjwa mmoja kama Corona. Hapo ndio hofu inapokuja
Hao wanaokufa na corona wengi ni wale wenye magonjwa ambayo ndio kila siku huwauwa.
 
Taifa letu linajifunza nini kutokana kupamba moto wa Corona huko Ulaya na Merikani katika majira haya ya baridi katika Mataifa hayo - mambo yanavyo elekea Dunia inakumbwa na COVID-19 katika phase ya pili - je,Serikali yetu pamoja na wizara ya afya na wizata ya utalii wamejipangaje kukabiriana na phase two ya COVID-19 ambayo italetwa na watalii na wagine kutoka mataifa ya Ulaya na Merikani - tusipo kuwa makini ungonjwa huu utalikumba Taifa letu kwa mara ya pili, this time around could be worse - God forbid.
Mwezi kama huu mwaka jana ilikuaje?,,piga flushback afu ukae mkao wa wary transgresor
 
Wanakufa ila sio kwa rate hii ,hii rate ni kama ile ya April-June 2020!! Yaani hawa maarufu ndio wanareflect ambao sio maarufu(ambao hawajulikani wanakufa wengi).
Tatizo hapo hao ni maarufu na kwa sababu kuna hicho kinachoitwa corona basi ndio tunaingizia humo humo,watu wangekuwa wanakufa wengi kuzidi kipindi cha kabla ya corona basi hali hiyo ingeonekana.

Kinachoendelea sasa hivi ni kusingizia marehemu kuwa wamekufa kwa corona,kila kifo tunataka kukihusisha na corona.
 
Unazungumzia watalii kuja na kutuletea corona kwani ile corona iliyoletwa na yule mdada wa kitanzania akitokea nje huko iliishia wapi?

Tusifanye ajizi - baadhi ya Mataifa ya Ulaya yameanza kupiga marufuku ndege za kutoka Uigereza na Afrika Kusini, wanasema COVID-19 ya kutoka mataifa hayo mawili imethibitika kwamba hiyo ni STRAIN mpya!! What does that tell us as a Nation, it means itakuwa more virulent kuliko strain ya mwanzo, ndio maana Waziri Mkuu wa Uingereza alionekana ana wasi wasi sana wakati alipo kuwa anawaonya raia wa Uingereza wasitoke nje ya nyumba zao ovyo ovyo na wa avoid mikusanyiko.

Binafsi naona Taifa letu lina paswa kuiga Mataifa ya Ulaya yaliyo piga marufuku ndege zinazo toka Uingereza na Afrika kusini,ila tatizo hatujui ndege za barani Afrika zinazo kwenda na kutoka Afrika kusini wamiliki wake wanatoka mataifa yapi ya Afrika, mfano: tusije kuruhusu ndege za Malawi,Zambia,Zimbabwe na Rwanda nk huku kumbe na zenyewe usafiri kwenda na kurudi kutoka Afrika Kusini possibly na Uingereza - hapo kuna changa moto jinsi ya kuzidhibiti zisije kikawa ni chanzo cha vector wa kueneza ugonjwa.
 
Back
Top Bottom