Tusifanye ajizi - baadhi ya Mataifa ya Ulaya yameanza kupiga marufuku ndege za kutoka Uigereza na Afrika Kusini, wanasema COVID-19 ya kutoka mataifa hayo mawili imethibitika kwamba hiyo ni STRAIN mpya!! What does that tell us as a Nation, it means itakuwa more virulent kuliko strain ya mwanzo, ndio maana Waziri Mkuu wa Uingereza alionekana ana wasi wasi sana wakati alipo kuwa anawaonya raia wa Uingereza wasitoke nje ya nyumba zao ovyo ovyo na wa avoid mikusanyiko.
Binafsi naona Taifa letu lina paswa kuiga Mataifa ya Ulaya yaliyo piga marufuku ndege zinazo toka Uingereza na Afrika kusini,ila tatizo hatujui ndege za barani Afrika zinazo kwenda na kutoka Afrika kusini wamiliki wake wanatoka mataifa yapi ya Afrika, mfano: tusije kuruhusu ndege za Malawi,Zambia,Zimbabwe na Rwanda nk huku kumbe na zenyewe usafiri kwenda na kurudi kutoka Afrika Kusini possibly na Uingereza - hapo kuna changa moto jinsi ya kuzidhibiti zisije kikawa ni chanzo cha vector wa kueneza ugonjwa.