Watu kulala hovyo kwenye madaldala ni dalili ya njaa kali!

Tatizo ni kula ugali mkubwa au mihogo asubuhi.
 
Huwezi kupata usingizi na njaa ,wameshia hao acha walale
 
Uwe na njaa ulale we kweli poyoyo. Hiyo ni shibe km hujui.
 
Kulala au kupata usingizi ni majaliwa ya ulevi wa SHIBE.
Kuwa na njaa uone kama utasinzia.
N. B, Mama lishe na wapishi mbalimbali acheni kuweka hamira kwenye ubwabwa mnasababisha haya.
Ahsante mkuu waeleze ukweli wengine ni wajinga hata Yesu akirudi hawatamwelewa
 
Kuna mmoja jana alitakiwa kushuka itv ,kutokana na kusinzia akashtuka gari likiwa mataa yakuingiaa makumbusho stend aisee alimtukana kondaa utafikirii konda ndio alimwambia alale
Kisheria konda anatakiwa kutangaza kila kituo
 
Bei ya vyakula iko juu na sio rafiki kwa mlaji,
Tatizo unamaneno mengi yasiokua na tija kwenye uandishi wako
 
Mbona mimi nikishiba napata usingizi kwahiyo hili nalo unasemaje mleta mada?

Japo kweli huyu maza kuna mambo haendi sawa ila sio kila lawama abebeshwe kukaa na njaa hapa bongo ni ujinga wako sio kila kitu ulaumu raisi.

Hiko kipindi cha magu chenyewe watu walikua na njaa kama kawaida mbona hamkuongea japo naye ana yake alizingua ila alipofanya vyema tulisifia alipozingua tulisema
 
Nadhani katika utafiti wako ungejaribu hata kuonana na wataalam wa lishe uweze kupata uelewa na tofauti za njaa na uchovu.....

Stress ni tatizo kubwa sana na seems hii post yako ni zao la msongo wa mawazo
 
Huo mchele wa 4000 kilo uko wapi?

Korie mwenyewe anauza 18000/5KG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…