Watu Maskini huongozwa na Maoni ya Watu zaidi kuliko Sheria ndio maana wanazidi kuwa Fukara

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Na, Robert Heriel

Moja ya dalili ya MTU Maskini na mjinga ni suala la kuongozwa na Maoni na mitazamo ya Watu wengine zaidi kuliko kuongozwa na Sheria na Kanuni.

MTU Maskini na mjinga Kabla hajafanya lolote hufikiria kuwa Watu watasemaje na kumuonaje, au watamchukuliaje.

Unajua umaskini na ujinga siku zote ni utumwa wa utajiri na Werevu. Badala MTU afikiri kuwa nikifanya Jambo hilo nitavunja sheria ipi iwe ya nchi au sheria za kidini au kiutamaduni ndipo afanye. MTU anawaza mambo ya Maoni ya Watu. Maisha yako hayapaswi kuongozwa na hisia, Maoni na mitazamo ya Watu. Huo ni utumwa.

Unakuta MTU anataka kuanzisha biashara lakini kitu cha Kwanza anachotanguliza ni kusikiliza Watu wanasemaje, Mama yake, Baba yake, Ndugu zake, marafiki, au jamii. Alafu mbaya zaidi hao anaowasikiliza wenyewe hawajawahi hata kufanya biashara. Lakini ndio wakwanza kutoa Maoni na mitazamo Yao utadhani wanakitu cha maana wanachojua. Vijana acheni kuongozwa na kile Watu wanachosema au wanavyowachukulia.

Wewe kama unataka kuanzisha biashara, Achana na Maoni, Fanya biashara mengine utajulia mbele Kwa mbele. Fuatilia sheria na Kanuni za biashara unayotaka kuifanya na sio Maoni ya Watu kuhusu hiyo biashara.

Unakuta MTU anaenda kuoa, lakini ni jitu linaondeshwa na Maoni na mitazamo ya Watu wengine. Huwezi fanikiwa Jambo lolote ukiwa MTU wa kushikiwa Akili na watu wengine. Ndoa itakushinda mapema.

Kwa vile Watu wanasema ndoa ngumu nawe hata hujawahi kuingia kwenye ndoa unaanza kuropoka kama mwendawazimu, ndoa ngumu, ndoa ngumu! Kama popoma flani! Ingia kwenye ndoa fuata Kanuni na sheria za mahusiano uone huo ugumu wa ndoa utatoka wapi.

Wakati tunasoma Enzo zile ilikuwa kawaida kusikia mtu akisema, Darasa la tano gumu, sijui Darasa la sita gumu, au Form Two pagumu, alafu ukifika Darasa Hilo unaona kawaida tuu. Watajitokeza tena watasema; Subiri uingie form Three hapo kuna mziki mnene, wanataja na baadhi ya topics wakikutisha. Ujinga mtupu!

Sisi kina Taikon sio Watu wa kuendeshwa na Maoni na mitazamo ya Watu. Kitu kama kilikuwa kigumu ni kwako kutokana uwezo wako kuwa mdogo.

Sisi tunachozingatia ni Kanuni na sheria. Hivyo ndio tunavipa kipaombele zaidi. Ingawaje Maoni na mitazamo ya Watu inatufanya tujue pande nyingi za Jambo tunalolifuatilia.

Maskini na wajinga wengi wanakosa uthubutu Kwa sababu ya hofu waliyojengewa na Maoni ya Watu wengine. Hofu za kipumbavu tu.

Zingatia Maoni mengi ya Watu yamejawa na ubinafsi. Watu wanaweza kukupa Maoni na mitazamo Yao ili wakukatishe tamaa.

Utasikia, hiyo biashara pasua kichwa, au alishindwa Fulani wewe ndio utaweza. Basi MTU akisikia hivyo anajaa upepo. Mwisho anaamua kuacha. Usiongozwe na Maoni na mitazamo ya Watu. Utakatishwa tamaa. Utashindwa.

Unakuta MTU anakuambia usifanye hivi au vile alafu ukimuuliza Kwa nini anakuwa Hana sababu ya maana. Yaani ujinga ujinga tu. Unamuuliza, nikifanya hivi nitapata madhara gani? Nitamdhuru yeyote? Nitavunja sheria za nchi au sheria za dini au sheria za utamaduni. Jibu Hana la maana. Kazi kufanyana watumwa Kwa mambo yasiyo na mantiki.

Sijasema usisikilize Maoni na mitazamo ya Watu wengine. Ila nimesema usiongozwe na Maoni na mitazamo ya Watu wengine. Huko ni kujitafutia utumwa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kweli kuna uhusiano wa kisayansi kati ya ujinga na umasikini wa pesa au utajili na kua na akili?
 
Umaskini Kwa kiasi kikubwa unachangiwa na ujinga. Kisayansi.
Kiimani, umaskini chanzo chake ni Laana
 
barikiwa
 
Back
Top Bottom