Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Shirika la Save the Children limeonya kuwa watu milioni 33 kutoka nchi kumi za Afrika Mashariki na Kusini wako kwenye hatari ya kukumbwa na njaa kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
Shirika hilo limetoa ripoti hiyo katika siku ya kwanza ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa (COP25) uliofunguliwa jana huko Madrid, Hispania.
Ripoti hiyo imesema, mwaka huu baadhi ya sehemu za Mashariki na Kusini barani Afrika zilikumbwa na mafuriko, maporomoko ya udongo, ukame na vimbunga, zaidi ya watu milioni 33 wako kwenye hali ya dharura ya ukosefu wa chakula au hali mbaya zaidi.
Ripoti pia imesema, kwa kuwa watu milioni 162 kwenye eneo hilo wana umri wa chini ya miaka 18, zaidi ya watoto milioni 16 wako kwenye msukosuko au hali ya dharura ya njaa.