Watu mliosoma wote kuanzia shule ya msingi, sekondari na vyuo hupotelea wapi?

Watu mliosoma wote kuanzia shule ya msingi, sekondari na vyuo hupotelea wapi?

Tuko mitandaoni tunatumia Anonymous I'd ili mliofanikiwa kwenye maisha msituchore, ila mitandaoni tumewa add ili tuone movement zenu siku mkidanja tuje kuwazika
Mkuu naulizia kwamba mbona sionani na wadau naojuana nao huko mitaani ata kama kwa nadra?? Mtandaoni sio sehemu physical master
 
Sema kua maarufu kumbe sio kitu simple, umaarufu wa halali lakn sio kama wa baltazar au amber rutty
 
Tuanze hesabu,

Primary darasani mlikua 200
Secondary daradani mlikua 200
A Level darasani mlikua 100
Chuo labda 200
Hawa jumla ni watu 700.

Tanzania ina watu jumla 70millioni approximately. So probability ya kukutana na watu Hawa 700 katika watu wote 70millioni walioko Tanzania ni 0.00001.
kama alikimbia Hesabu hawezi elewa kabisa😄
 
Habari za mapambano wakuu,

Kuna swali huwa najiuliza sana haswa wiki inapoanza Jumatatu napokuwa naelekea kwenye majukumu, hivi watu niliosoma nao primary, seco na chuo mbona asilimia zaidi ya 97% siwaoni?

Sio kwenye maofisi ya uma na binafsi, usafiri wa umma kama daladala na mwendokasi, sehemu za huduma za kijamii kama migahawani au hata za ibada (kwa mimi msikitini).

Niwe mkweli napenda sana privacy na ninafurahi kutoonana na watu naowajua ovyo ila haiondoi hilo swali kichwani!

Kwenye utafutaji nina uzoefu wa miaka 9+ kwenye ajira makampuni tofauti lakini pia nishajichanganya sehemu tofauti tofauti mikoa yote mikubwa hapa nchini cha ajabu ni nadra kukutana hata na wafanyakazi wenzangu wa zamani au wapambanaji wengine tulio hustle nao.

Maex ndio sinaga bahati ya kuonana kabisa wakati nilikuwa Lewandowski mmoja sniper sikosi, ila kwa hili nashukuru hao sina hata shauku ya kuonana nao.

Na kuna marafiki wa utotoni mliokua mtaani pamoja, sijui wameyeyukia wapi? Ubaya huwa nikikuta nimewekwa group najitoa naonaga upuuzi kukuta msg 628+ kusoma hata kujibu ni mzozo.. ila mada ni kuonana hata kwa juu juu humu mjini kwahiyo magroup sio kesi bado.

Kuna muda huwa najiuliza au watu wamekua wamebadilika labda mwingine kufutuka sana hata huwezi mjua? Kwa mimi watu wengi huniambia wajihi wangu haubadiliki tokea utotoni so ni rahisi kunijua na imenitokea mara kadhaa mtu ananikumbusha ila simkumbuki.

Hivo inawezekana napishana na watu waliobadilika kiasi cha kutokumtambua? Hili silipi uzito.

Hivi kuna member mwingine huwa anajiuliza kama mimi na ina tija kuwaza hivyo?
Labda wako kundi la Whatsapp la mliosoma pamoja wanashangaa wewe uko wapi.
 
Tuanze hesabu,

Primary darasani mlikua 200
Secondary daradani mlikua 200
A Level darasani mlikua 100
Chuo labda 200
Hawa jumla ni watu 700.

Tanzania ina watu jumla 70millioni approximately. So probability ya kukutana na watu Hawa 700 katika watu wote 70millioni walioko Tanzania ni 0.00001.
Hii hesabu ya hoja atakayeihoji na kukomaza fuvu kubishi, huyo ni kichwa ngumu wa kuzaliwa na harekebishiki.

Mkuu umetufungia mada hii kwa hesabu ya uwiano ambayo rahisi sana.
 
Wengi wapo facebook huko. Wewe jaribu kuvaa suti mpya kisha post "Asante mama kwa kuniteua kuwa mkuu wa wilaya ya Lushoto", Lazima uone watakavyotiririka inbox na kwenye comment.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nyakati zote wakati nasoma nikimaliza mitihani yangu ya mwisho toka shule ya msingi hadi chuo kikuu, naondoka kimya kimya bila kuwaaga marafiki. Sikuwahi mahafali, ni hulka ya ubinafsi

me ni mcheshi napenda marafiki ila wakati wa kuondoka nawaacha na maswali mengi mpaka sasa niliosoma nao wengi wanahamu ya kujua wapi nilipo

nishakutana na marafiki zangu wengi niliosoma nao masokoni, stendi za mabasi, usafiri wa umma, mimi nikiwaona navunga pengine nabadili mwelekeo wasinione.....

napenda kuvaa kofia na miwani ya macho kuficha id yangu niwapo mikusanyikoni
 
Back
Top Bottom