kanda2 said:
Muongo mkubwa,wapare aliyewasaidia ni Cleopa Msuya kama uchifu apewe msuya.ni kabila dhariri sana mbele ya wachagga,kutokana na manyanyaso hayo ndio Msuya akawasukuma kimaendeleo.labda history hii umetunga wewe.
kanda2,
Wachaga,Wazigua,na Wasambaa, walitunyanyasa sana Wapare kabla hatujawa na mfumo madhubuti wa utawala. kwa asili Wapare walikuwa vikundi vidogo vidogo vya wahamiaji toka maeneo ya Utaita, na Ukamba. baadaye wamekuja kuchanganyika na Wachaga,Wazigua,Wasambaa, Wagweno,Wambugu etc etc. usishangae leo ukisikia kuna Minja Wachaga na wengine Wapare. pia wako kina Tenga Wachanga wengine Wapare. Kilonzo wanapatikana Ukambani na Upareni. Mwanzia wako Utaita na Upareni. kwa hiyo ni kweli kabisa katika kuhama hama kwetu tulikuwa dhalili sana mbele ya Wachaga waliokuwa wakipora mali zetu, na Wasambaa na Wazigua waliokuwa wakituuza utumwani. pia tuliwahi kutawaliwa na maakida wa Kizigua na Kisambaa waliosimikwa na Wajerumani.
CHAANGAJA Cleopa David MSUYA asili yake ni North Pare. sasa huko uchifu wao ni ulikuwa kwenye koo za Wasangi na Wambaga. kuna historia ya vita kati ya clan hizo mbili, lakini Mfumwa wa maarufu wa mwisho wa North Pare alikuwa Mfumwa Sabuni ambaye ni Mmbaga ambao kwa asili walihamia toka South Pare.
Msuya ameendeleza pale walipoachia wale waliomtangulia kama hao Machifu niliowataja, na marehemu
Chediel Mgonja "kaghembe" ambaye ni mbunge wa kwanza wa wilaya ya Pare baada ya uhuru. barabara za Ugweno na Usangi kuunganisha na mji wa Mwanga zilijengwa kwa nguvu ya wananchi kuanzia kuanzia 1922 mpaka 1936. wakati huo Chaangaja Cleopa Msuya alikuwa ama hajazaliwa au ni mtoto mdogo.
napenda kukueleza kuwa wazee wetu walikuwa na makini sana katika shughuli za kujitolea MSARAGAMBO. waliweza kutunga sheria na faini za kuwadhibiti watega kazi na watoro.
kanda2, siyo kosa lako kwamba historia ya Upare unaoijua wewe inaanzia na Cleopa Msuya. pia inajumuisha wakati wilaya zetu zikiwa ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. wilaya ya Pare, sasa Mwanga na Same, miaka ya michache kabla na baada ya uhuru ilikuwa chini ya jimbo la Tanga. kabla ya hapo kulikuwa na North Pare iliyokuwa chini ya North Province na South Pare iliyokuwa chini ya Tanga Province.
harakati zetu za kujiamulia mambo yetu wenyewe zilianza na mashujaa kama Mavura wa Mbaga aliyebigana na Wazigua na Wasambaa waliokuwa wakituteka utumwa. inaendelea mpaka karibu na Uhuru ambapo wanachama wa
WAPARE ASSOCIATION waliunganisha nguvu zao na
TAA na
TANU. viongozi wa Wapare Association kama
MANASE KANIKI, SAMUEL MSHOTE na
ELIAS KISENGE walikuwa mstari wa mbele kuhamasisha kwa niaba ya TANU katika maeneo ya Upare na Tanga Province.
Elias Kisenge alikuwa Executive Secretary wa Pare Council, katibu wa Tanu na Wapare Association. baadaye alipanda ngazi na kuwa Katibu wa Tanu jimbo la Tanga, kabla hajahamishiwa makao makuu ya Tanu kuwa Katibu Mwenezi.
pia kuna kipindi Wapare walitaka kuanzishwa mfumo kama wa Wachaga wa kuwa na Paramount Chief. Elias Kisenge alikuwa kati wa wananchi waliofikiriwa kuchukua nafasi hiyo.