Interested Observer
JF-Expert Member
- Mar 27, 2006
- 3,384
- 4,428
What is wrong with a short? Kwa ile weather ya Dar Es Salaam I can be comfortable wearing a short or a lob (kanzu)!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kawaida yako. Ukibanwa na hoja unarudi baadaye na more info.
Zakumi,Mama Ntilie:
Huu uzoefu wako hauko ukamili. Wakati TAA inabadilika na kuwa TANU 1954, wimbi la kudai uhuru tayari lilikuwepo barani Africa. Na haitawezekana kwa watanzania kuanza kudai uhuru mwaka 1954, hii itakuwa ni kutotendea haki struggle za wananchi zilizokuwepo kabla.
Phenomena unayoiona hapa, imetokea karibu katika nchi zote za kiafrika. Wananchi walianzisha vyama, lakini baadaye waliwapa nafasi vijana waliotoka masomoni Ulaya.
Kwa mfano Kwame Nkrumah alikuwa yupo uingereza hana mpango wowote. Lakini kwa sababu alikuwa amesoma watu walimrudisha Ghana na kumpa madaraka.
Nkrumah hakusoma Uingereza. Alisoma Marekani katika chuo kikuu cha Lincoln jimboni Pennyslvania. Alipokuwa Marekani alikutana na wana harakati wengi tu kutoka Black diaspora, including Guyana, Jamaica, Trinidad and Tobago, na wote hawa wakizungumzia haki ya watu weusi kujitawala. Kwa huyo wakati Nkrumah anarudi kwao alikuwa ameshaamua kuingia katika siasa.
Kamuzu Banda, Jomo Kenyatta na wengine wengi tu walikuta watu wameweka misingi mizuri ya vyama vya kudai uhuru. Na hawa ndio walioandikwa kwenye historia.
Nia ya Mhe. Mkandara ni njema kabisa lakini ndugu yetu Junius naona umeenda nje ya mstari. Unamlaumu Baba wa Taifa eti alijali umaarufu wake tu wengine aaa! You are being very unfair to him! Did you expect him kusimama jukwaani na kutoa orodha ya wale alioshirikiana nao katika kupigania Uhuru? Ama ulitaka pamoja na makujumu mazito ya kuliongoza taifa basi aketi chini awaandikie historia. Kazi hiyo ni yenu wasomi na hata wale wasio wasomi kuandika historia ya nchi hii kwa kuwafuata wanasiasa na wananchi ambao bado wako hai wanaojua kilichotokea miaka hiyo. Hata hivyo Mwalimu did justice to his fellow wapiganaji kwa sababu amewahi mara kadhaa kuwataja watu kama akina Mzee Tambaza, Sykes, Rupia na wengine wengi tu katika hotuba zake wakati akisimulia juu ya harakati za kupigania Uhuru. And for your information baada ya kustaafu wapo Watanzania waliokuwa wakionana naye na na kupata simulizi na mengi yaliyotokea katika historia ya nchi hii. I assure you, he wasn't all that mean kama unavyotaka kutuaminisha Junius!
Kwa uzoefu wangu, naona wengi wanaomkandia Mwalimu na kumshutumu kwa namna moja ama nyingine ni wale ambao kama si wao basi 'ancestors' wao waliguswa na 'fimbo' ya Mwalimu katika mambo kadha wa kadha.
And the point is?kwanza you need to get your facts right...Nyerere alikuja Dar mwaka 1952 akiwa kama mwalimu wa shule ya St. Francis College, Pugu.Alikuwa hajui mtu na alikuwa ni jamaa ambaye yupo yupo tuuuu
Nyerere alikuwa na Mwapachu huko Tabora katika mwaka 1945, na Makerere College na baadaye nchini Uingereza wakichukua masomo ya juu...nadhani walikuwa Edinburgh Inawezekana kwamba Nyerere kufuatia harakati za chama cha TAA, alisikia kuhusu Abdulwahid Sykes kupitia kwa Mwapachu alipokuwa bado yuko Uingereza. Mwapachu na Nyerere walikuwa wanafunzi katika Makerere College wakati ambapo Kasella Bantu na Nyerere walifundisha katika shule moja, St. Mary's School kule Tabora. Na hii haina ubishi ukitaka kujua mengi zaidi soma kitabu kilichoandikwa na Mwandishi maarufu wa historia ya Tanganyika, BW. MOHAMED SAID katika kitabu chake cha The Life and Times of Abdulwahiid Sykes. sasa hili la kutaka kutuambia tunapindisha Historia umelitoa wapi? Hakuna anayemkandia Nyerere ila ukweli unaelezwa kama ulivyo na si kwa kusoma tuu lakini inabidi ukae chini na wazee wa mji ambao walikuwepo enzi hizo ndio utaelewa watu wanazungumiza nini
Of course inawezekana hukuambiwa lakini unaambiwa kati ya ma RADICALS hakuna aliyekuwa kama KASELLA Bantu mwanachama wa TAA mwenye msimamo usiotetereka wa kupinga ukoloni alijiuzulu kufundisha na alikuja Dar es Salaam kujiunga na Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC)....
Na unaambiwa kwenye hotuba ya kuaga yenye kuhuzunisha ambayo Nyerere aliitoa tarehe 1985 kwa Wazee wa Dar es Salaam, kikundi cha Waislamu pekee wakazi wa mjini waliomuunga mkono tangu kuundwa kwa TANU, Nyerere aliwaambia wasikilizaji wake kwamba ilikuwa Kasella Bantu aliyemtambulisha yeye Nyerere kwa Abdulwahid.
Hii ilikuwa ni moja ya zile nyakati adimu sana ambazo Nyerere alizungumza hadharani kuhusu siku zake za mwanzo na ilikuwa mara ya kwanza kutaja jina la Abdulwahid hadharani akimhusisha na historia yake mwenyewe na ile ya chama.
sasa mnataka kubisha nini?
Waliopigania uhuru ni Waswahili bwana,kwa maana ya wasilamu na wakristo maskini.Mwazna alikuwapo Huseni Majaliwa,Bukoba alkuwapo Ali Migeyo,Kahama Ali Saidi Maswanya,Paulo Bomani,Mwananyolo na Gerevas waliokubali mseto na kuitwa wapumbavu.Lakini wale waliokuwa wamejikita katika Misheni na kuwa karibu sana na wakoloni walikuja kurukia tu kama Lyanyantika Masha na wengineo walikuja kupewa kazi na nyerere.
Kule darisalam ambako ndiko kulikuwako na vuguvugu kubwa ni wale wazee wa kipwani walikuwa wanampelekesha mkoloni.Nyererr yeye alilpelewka na kapputula yake na kasela bantu hadi kwa kina sykes na kutambulishwa huko.[/QUOTE]
Maneno yako ni mazima kabisa
Infact Nyerere alikuwa mgeni kabisa mjini Dar es Salaam na kama ilivyokuwa mazoea, Kasella Bantu alimchukua Nyerere kwa Abdulwahid kukamilisha kufahamiana na kukutana na watu maarufu wa pale mjini. Mbali na Dossa Aziz aliyekutana na Nyerere kwa muda mfupi katika mkutano mkuu wa TAA , ilikuwa ni Mid 40's, Kasella Bantu mwenyewe na Denis Phombeah, hakuna mtu mwingine katika makao makuu ya TAA aliyewahi kusikia habari za Nyerere...infact Nyerer was a NO BODY
Wakati huo, Abdulwahid na mdogo wake Ally, walikuwa na mawasiliano na International Union of Socialist Youth iliyokuwa Austria na mipango ya kupeleka mjumbe Umoja wa Mataifa, NewYork ilikuwa mbioni. Nyerere na baaadaye Mwapachu walirudi toka Uingereza wakiwa wameshawishika na mawazo ya Fabian Society, kikundi cha wasomi cha mrengo wa kushoto cha Labour Party ya Uingereza. (Btw mimi ni member wa Fabian Society)
Ukikaa na wakee kama akina Mzee Katungunya pale nje ya msikiti wa Manyema watakuwambia kuwa Abdulwahid, Nyerere, Ally, Dossa Aziz, Mhando, Rupia, Dunstan Omari na wengine walizoea kukutana kila Jumapili kwa ajili ya baraza ama nyumbani kwa Dossa Aziz mtaa wa Congo au nyumbani kwa Abdulwahid mtaa wa Stanley. Sehemu hizi ndizo ambazo wazalendo hawa walikuwa wakikutana kujadili mustakabali wa Tanganyika....ambayo siku hizi mnaiita Tanzania ya MAFISADI
Zakumi,
Nkrumah hakusoma Uingereza. Alisoma Marekani katika chuo kikuu cha Lincoln jimboni Pennyslvania. Alipokuwa Marekani alikutana na wana harakati wengi tu kutoka Black diaspora, including Guyana, Jamaica, Trinidad and Tobago, na wote hawa wakizungumzia haki ya watu weusi kujitawala. Kwa hiyo wakati Nkrumah anarudi kwao alikuwa ameshaamua kuingia katika siasa.
kilichokuja kumkumba Nyerer baada ya uhuru anakijua Mwenyezi Mungu tuuTo be fair ilivyoonekana Mwalimu Nyerere alimuona Abdulwahid Sykes kuwa ni mtu mwenye akili sana, asiye na choyo na mtu wa kupendeka. Kwa upande mwaingine Abdulwahid alimwona Nyerere kuwa ni mtu aliyeelimika sana na mwenye ustadi wa kupendeza wa kujadiliana.
kilichokuja kumkumba Nyerer baada ya uhuru anakijua Mwenyezi Mungu tuu
kilichokuja kumkumba Nyerer baada ya uhuru anakijua Mwenyezi Mungu tuu
Please go on kipi?
To be fair ilivyoonekana Mwalimu Nyerere alimuona Abdulwahid Sykes kuwa ni mtu mwenye akili sana, asiye na choyo na mtu wa kupendeka. Kwa upande mwaingine Abdulwahid alimwona Nyerere kuwa ni mtu aliyeelimika sana na mwenye ustadi wa kupendeza wa kujadiliana.
kilichokuja kumkumba Nyerer baada ya uhuru anakijua Mwenyezi Mungu tuu
Unajiita Atheist na baadaye unasema anakijua Mwenyezi Mungu. Hapo umeondoka kwenye u-Atheist.
Anyway. Baada ya uhuru viongozi wengi wa Africa walikuwa kwenye ideaological battles na kusahau walichopigania uhuru. Na matokeo yake vyama vya kupigania uhuru vikawa vimejaa makada wa kisiasa na ambao ndio walioandika historia za nchi.
Hizo point zote ulizoongea, are you trying to discredit that Nyerere ni katika "Watu Muhimu ktk Historia ya Nchi yetu?".hatuwezi kuenda mbele bila kujua huko nyuma ilikuwaje..unajua historia ukitaka kuenjoy basi inabidi uwe na subra...kwanza ni muhimu kujua yaliyotokea huko nyuma au unasemje ?
issue ilipo inhand in historia ya nchi yetu unless una lako jambo
au imekuudhi Abdulwahid Sykes na Kasela Bantu kumwonyesha Nyerere njia?