Watu Muhimu katika Historia ya Nchi yetu

What is wrong with a short? Kwa ile weather ya Dar Es Salaam I can be comfortable wearing a short or a lob (kanzu)!!
 
Zakumi,
Nkrumah hakusoma Uingereza. Alisoma Marekani katika chuo kikuu cha Lincoln jimboni Pennyslvania. Alipokuwa Marekani alikutana na wana harakati wengi tu kutoka Black diaspora, including Guyana, Jamaica, Trinidad and Tobago, na wote hawa wakizungumzia haki ya watu weusi kujitawala. Kwa hiyo wakati Nkrumah anarudi kwao alikuwa ameshaamua kuingia katika siasa.
 

kwanza you need to get your facts right...Nyerere alikuja Dar mwaka 1952 akiwa kama mwalimu wa shule ya St. Francis College, Pugu.Alikuwa hajui mtu na alikuwa ni jamaa ambaye yupo yupo tuuuu

Nyerere alikuwa na Mwapachu huko Tabora katika mwaka 1945, na Makerere College na baadaye nchini Uingereza wakichukua masomo ya juu...nadhani walikuwa Edinburgh Inawezekana kwamba Nyerere kufuatia harakati za chama cha TAA, alisikia kuhusu Abdulwahid Sykes kupitia kwa Mwapachu alipokuwa bado yuko Uingereza. Mwapachu na Nyerere walikuwa wanafunzi katika Makerere College wakati ambapo Kasella Bantu na Nyerere walifundisha katika shule moja, St. Mary's School kule Tabora. Na hii haina ubishi ukitaka kujua mengi zaidi soma kitabu kilichoandikwa na Mwandishi maarufu wa historia ya Tanganyika, BW. MOHAMED SAID katika kitabu chake cha The Life and Times of Abdulwahiid Sykes. sasa hili la kutaka kutuambia tunapindisha Historia umelitoa wapi? Hakuna anayemkandia Nyerere ila ukweli unaelezwa kama ulivyo na si kwa kusoma tuu lakini inabidi ukae chini na wazee wa mji ambao walikuwepo enzi hizo ndio utaelewa watu wanazungumiza nini

Of course inawezekana hukuambiwa lakini unaambiwa kati ya ma RADICALS hakuna aliyekuwa kama KASELLA Bantu mwanachama wa TAA mwenye msimamo usiotetereka wa kupinga ukoloni alijiuzulu kufundisha na alikuja Dar es Salaam kujiunga na Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC)....


Na unaambiwa kwenye hotuba ya kuaga yenye kuhuzunisha ambayo Nyerere aliitoa tarehe 1985 kwa Wazee wa Dar es Salaam, kikundi cha Waislamu pekee wakazi wa mjini waliomuunga mkono tangu kuundwa kwa TANU, Nyerere aliwaambia wasikilizaji wake kwamba ilikuwa Kasella Bantu aliyemtambulisha yeye Nyerere kwa Abdulwahid.


Hii ilikuwa ni moja ya zile nyakati adimu sana ambazo Nyerere alizungumza hadharani kuhusu siku zake za mwanzo na ilikuwa mara ya kwanza kutaja jina la Abdulwahid hadharani akimhusisha na historia yake mwenyewe na ile ya chama.


sasa mnataka kubisha nini?
 
And the point is?
 

Kardinali Laurian Rugambwa kardinali wa kwanza afrika.....
 
 


Jasusi:

Ni kweli Nkrumah alisoma Marekani, lakini baadaye alikwenda kuishi Uingereza. Huko alitaka asome London School of Economics lakini baadaye aliingiza kwenye Pan Africanism. Na huko alikuwa mpiga porojo wa siasa kwenye migahawa.

Alirudi Ghana baada ya kupata mwaliko wa Joseph B. Danquah ambaye alikuwa ni kiongozi wa United Gold Coast Convention (UGCC) hili awe katibu mkuu wao.

Hivyo aliporudi Ghana alitokea Uingereza. Kwa reference zaidi soma mikutano ya Pan Africanism iliyofanyika uingereza the rest is commentary.
 
To be fair ilivyoonekana Mwalimu Nyerere alimuona Abdulwahid Sykes kuwa ni mtu mwenye akili sana, asiye na choyo na mtu wa kupendeka. Kwa upande mwaingine Abdulwahid alimwona Nyerere kuwa ni mtu aliyeelimika sana na mwenye ustadi wa kupendeza wa kujadiliana.

kilichokuja kumkumba Nyerer baada ya uhuru anakijua Mwenyezi Mungu tuu
 
kilichokuja kumkumba Nyerer baada ya uhuru anakijua Mwenyezi Mungu tuu

Please go on kipi?
 
kilichokuja kumkumba Nyerer baada ya uhuru anakijua Mwenyezi Mungu tuu

Please go on kipi?

hatuwezi kuenda mbele bila kujua huko nyuma ilikuwaje..unajua historia ukitaka kuenjoy basi inabidi uwe na subra...kwanza ni muhimu kujua yaliyotokea huko nyuma au unasemje ?
 

Unajiita Atheist na baadaye unasema anakijua Mwenyezi Mungu. Hapo umeondoka kwenye u-Atheist.

Anyway. Baada ya uhuru viongozi wengi wa Africa walikuwa kwenye ideaological battles na kusahau walichopigania uhuru. Na matokeo yake vyama vya kupigania uhuru vikawa vimejaa makada wa kisiasa na ambao ndio walioandika historia za nchi.
 
Kwa kuanza tuu ni muhimu kujua kuwa Nyerere hakuwa na uzoefu wa ujuzi wowote wa kisiasa uliostahiki kutajwa wakati huo wa kulinganisha na ule wa Abdulwahid.


Chama cha African Association huko Tabora kiliposhiriki katika ule mgomo wa jumla in the late 40's Nyerere hakujihusisha na chama hiki cha wafanyakazi ingawa alikuwa katibu wa chama

sasa je hii ilikuwa ni calculated risk au nini? sijui labda nitamuuliza Mohammed Said anifafanulie zaidi maana alipata bahati ya kuongea na wazee ambao walimpa insight zaidi

Anyway, kutokana na sababu hiyo kuheshimiana kulitokea baina ya Abdulwahid na Nyerere, Kila Jumapili Nyerere alikuwa akisafiri toka Pugu hadi Dar es Salaam kuhudhuria mikutano hii isiyokuwa ya kawaida na baada ya mikutano ama Dossa Aziz au Dunstan Omar alimrudisha Nyerere kwa gari hadi Pugu....so hivi ndivyo ndivyo Nyerere alivyokuja kuingia ndani ya duru za ndani zaidi za TAA katika makao makuu na hatimaye akajapendekezwa kugombea cheo cha juu kabisa cha uongozi wa cham in 1953.
 

issue ilipo inhand in historia ya nchi yetu unless una lako jambo

au imekuudhi Abdulwahid Sykes na Kasela Bantu kumwonyesha Nyerere njia?
 
Hotuba mnayoizungumzia nimeipata toka kwa jamaa wa Tanzania Daima.

*******************************************************************


Katika kumuenzi Baba wa Taifa, leo tunawachapishia moja ya hotiba zake zilizowakuna wengi. Hii ni sehemu ya hotuba ya Julius Nyerere alipokutana na Baraza la Wazee wa Dar es Salaam, kuagana nao kabla hajastaafu urais. Ilichapishwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la Radi, Toleo Na. 2 la mwaka 1986 lililokuwa likimilikiwa na Ndimara Tegambwage. Gazeti hili lilifutwa na serikali kwa madai kuwa lilikuwa halitoki kwa muda mrefu – Mhariri Tanzania Daima.

MIMI nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.

Niliporudi nikakubaliana na wamisionari hapo Pugu (sekondari), nifundishe shuleni kwao. Lakini nikiwa shuleni – Chuo Kikuu – nilijua. Niliishaamua kwamba maisha yangu yatakuwa ya siasa. Niliamua hivyo: Nitafundisha kwa muda wa miaka mitatu, nione hali inavyokwenda na kuzoeana na wenzangu kabla ya kuanza maisha ya siasa.

Niliporejea nchini hapo Oktoba, nikaenda Butiama. Januari nikarudi Dar es Salaam. Nikaanza kazi. Nikataka kujua habari za African Association. Mzee Mwangosi anakumbuka. Yeye ndiye aliniambia habari za African Association. Aliisha niambia habari hizo tangu nikiwa Makerere – Chuo Kikuu – nikiwa mwanafunzi.

Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao. Hapa tukaona mambo yanakwenda vizuri kidogo.

Tukaona kwanini TAWA iwe ya wanafunzi peke yao na siyo Tanganyika nzima. Kwa hiyo nikawaandikia baadhi ya watu Tanganyika. Nikasema, jamani ee, tumeanzisha chama, kwanini msianzishe huko matawi ya chama hicho?

Ndugu Mwangosi akapata barua hiyo. Alikuwa miongoni mwa waliopata barua hiyo. Akaniandikia – nikiwa Makerere – akasema: Wewe kwanini unataka kuanzisha chama kipya? Kipo chama. Kipo Chama cha TAA (Tanganyika African Association).

Kwa hiyo la maana si kuanzisha matawi, maana chama kipo na matawi yameenea; la maana ni kwamba hicho chama chenu mfute, na muanzishe tawi la Tanganyika African Association.

KUVUNJWA KWA TAA

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Mary's (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.

Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.

Nilipelekwa na Kasela Bantu - ambaye naye aliteleza-teleza na hatunaye hapa (kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo. Nilipokuja Dar es Salaam, nikakuta anafanya kazi Radio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Sykes.

Wakati huo mambo yalikuwa yanasinzia kidogo. Kwa muda mfupi mwaka ule, tukafufua-fufua, hasa kutoka Januari. Kufika Aprili, TAA ikafufuka. Tukafanya mkutano hapo Anautouglou. Kwenye mkutano huu wakanichagua kuwa rais wao – wa TAA.

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana – cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana – katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na kina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

WAZEE NA MSIMAMO

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU. Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa! Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao, waliogopa kuvipoteza.

Nalo jambo lenyewe ni la hatari – la kuzungumzia uhuru! Unaweza ukakosa kazi; na wapo waliopoteza kazi; wengine wakaacha kazi. Kina Rashid (Kawawa) waliona watoke kwenye shughuli hizo tuje tuungane katika chama.

Wazee wa Dar es Salaam, na baadaye wa nchi nzima, wakatuunga mkono, na kila nilipokwenda, watu wa kwanza walionielewa, walikuwa wazee.

Nilikwenda Songea mwaka 1955 mara baada ya kujiuzulu. Huko wazee walinipokea na kunielewa. Nilianza safari za kuitembelea Tanganyika nzima. Nilikwenda Mbeya. Mkutano wangu niliufanya na wazee; kikundi kidogo cha wazee, ndani ya nyumba ya mtu.

Kwa mkutano huu wa Mbeya, wazee wakauliza: Unatafuta nini? Nikawaambia natafuta uhuru. Wale wazee, kwa sababu ya vita vya Maji Maji, na wanakumbuka, kabisa, wakaona mimi ninatafuta jambo la hatari. Tulifanya mkutano wa makini kweli. Wakauliza: Wewe unawezaje kuleta uhuru? Wewe una njia gani kudai uhuru na usitiwe kitanzi na Waingereza?

WAINGEREZA WAONGO
Tulielezana. Nikawaambia ninyi wazee, Waingereza wanawadanganya, Waingereza wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa (League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari, watuachie tukajitawale.

Waingereza wanafanya ujanja; hawasemi. Vita vimekwisha (vya Pili) na Umoja wa Mataifa mwingine – mpya (United Nations Organisation – UNO) umewakabidhi Tanganyika kwa shabaha ileile. Sisi siyo koloni lao. Wamepewa dhamana tu.

Kwa hiyo nikawaambia wazee, hakuna haja ya kumwaga damu. Tuwaseme tu! Tuwashitaki kwa waliowaleta hapa kwamba hawafanyi kazi yao; wamesahau kabisa!

Wazee wakauliza: Eh, inawezekana? Nikasema inawezekana. Kazi yetu ya kwanza ilikuwa kuwaambia watu kwamba uwezekano wa kujitawala upo. Hilo lilikuwa la kwanza. Wazee walijua maana ya kujitawala. Walitamani kujitawala, lakini hawakujua waanzie wapi.

Vijana hawakuwa na habari kwamba kujitawala kunawezekana. Kwa hiyo kwa wazee sikuwa na matatizo. Wao hawakuwa na kazi; hawakumwogopa Mwingereza. Hawakuogopa kufukuzwa kazi. Baadhi walikuwa wafanyabiashara.


Mzee John Rupia (marehemu) alikuwa mfanyabiashara na kaidi (mkaidi) kidogo. Aliwahi kutishwa na kunyang'anywa leseni yake ya biashara. Akaambiwa akiendelea kushirikiana na kijana mwenda wazimu (Julius Nyerere), atanyang'anywa leseni moja kwa moja. Rupia aliwajibu: Potelea mbali!

Nasema yote haya ikiwa njia ya kutoa shukrani kwa wazee na imani yao kwa vijana wakati huo.

Imani hujenga imani. Na mambo haya makubwa ya nchi, kama hayana baraka za wazee hayaendi. Magumu sana. Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee tangu zamani. Tangu awali kabisa.

TWINING AMEKWISHA

Siku moja, Dosa akanifuata Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka. Wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja. Nikaenda. Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu. Wakaniombea dua za ubani. Tukamaliza.

Tulipomaliza wakasema kuna dua pia za wazee wao. Basi wakanitoa nje. Tukatoka. Zilipomalizika zilikuwa za Kurani; sasa zikaja dua za wazee – za jadi.

Walikuwa na beberu la mbuzi. Wamechimba shimo. Wakaniambia simama. Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, "Twining (Twainingi) umekwisha!" (Edward Twining alikuwa gavana wakati huo). Ndipo nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo Twining amekwisha!

Sasa mimi Mkristo; hao Waislamu. Na mimi mkorofi-korofi katika mambo haya (ya kutambika). Lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao. Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa: Nenda nyumbani salama. Twining hawezi tena!

Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa kina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa mzee Mohammed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: Bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee.
 
hatuwezi kuenda mbele bila kujua huko nyuma ilikuwaje..unajua historia ukitaka kuenjoy basi inabidi uwe na subra...kwanza ni muhimu kujua yaliyotokea huko nyuma au unasemje ?
Hizo point zote ulizoongea, are you trying to discredit that Nyerere ni katika "Watu Muhimu ktk Historia ya Nchi yetu?".

Umeongelea kuwa Nyerere admired Sykes and this other guy admired Nyerere, sasa sielewi, unataka kusema Nyerere ali-exploit wema wa hawa watu wa - Pwani; au siyo kuwa hawa watu - Wa-Pwani (Dalisalamu) walikuwa na expectation kubwa mno baada ya Uhuru. Ulivyoongea hapo juu inaonekana kuwa Nyerere alifanya dhuluma kubwa sana kwa baadhi ya watu wa Dalialamu na itikadi zao hasa wale WaIslamu, huoni kuwa, inawezekna kuwa Nyie pamoja na wewe mlikuwa minority on those people who were in struggle for the liberation of the motherland.

How can Mr. Nyerere alone triumph to such higher stage and have such powers without the majority at the core?
 
Balozi Paul Bomani alikuwa architect muhimu wa vyama vya ushirika kanda ya ziwa, vyama vilivyoleta matumaini na mwanga wa ukombozi kwa wakulima wa kiafrika kutoka unyonywaji wa wakoloni kwa kupitia vibaraka wao wa kihindi waliokuwa na monopoly ya vinu vya kuchambua pamba (ginneries) kuanzia sehemu za Nasa, Kwimba, Musoma na pande zote za mashariki na kusini mwa ziwa Victoria Tanzania.
 
issue ilipo inhand in historia ya nchi yetu unless una lako jambo

au imekuudhi Abdulwahid Sykes na Kasela Bantu kumwonyesha Nyerere njia?

Mimi historia ya Tanzania sijuhi vizuri lakini naichambua kwa vigezo vyangu.

Historia ya nchi nyingi za kiafrika zimepikwa na kuwakuza watu pale isivyo. Nyerere amechukua uongozi wa TAA akiwa na miaka 31 au 32. Ndio kwanza amerudi na hajajijenga. Na zaidi ya hapo alikuwa na familia changa.

Ukichukua umri aliyokuwa nayo na mazingira ya wakati utaona kuwa historia ya Tanzania nayo imepikwa.

Ukienda upande wa Kaskazini ya Tanzania, watu wa mwanzo kuanzisha chama cha ushirika barani Africa, utaona kuwa Tanzania haikusubiri mpaka TANU ianze ili wadai uhuru wao.

Vilevile mapambano ya kudai uhuru Tanganyika yanakuwa Exaggerated. Mwingereza hakuwa na faida yoyote ya kukaa Tanganyika.
 
Bangusule,
Naona umemaliza somo. Ngoja sasa waje akina Junius watuambie jinsi Nyerere alivyoua babu zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…