Watu Muhimu katika Historia ya Nchi yetu

Zakumi,
Alichofanya Nyerere ni kuunganisha pamoja juhudi zote za kupigania uhuru kote nchini chini ya TANU. That was no small feat, Karl Peters notwithstanding.
 

Tunakwenda taratibu mzeee haraka ya nini BANGUSILO keshaleta hotuba ya Nyerere kwa wazee...sasa kwenye hili la kumdiscredit Nyerer ambalo unataka niliharakishe sitolileta kwa sasa kwani bado tunatazama matukio ya hapo awali


Kwa kuanza tuuu uongozi wa TAA ulimpendekeza Nyerere ili kukiimarisha chama kwa kuwani Mwafrika aliyesoma sana. Ilibakia kwa Nyerere kulikubali au kulikataa shauri hilo; kabla yake Chifu Kidaha Makwaia kama ushawahi kumsikia alishauriwa kuchukua uongozi wa TAA ili kuchukua urais lakini alilikataa shauri hilo.


Ilikuwa jambo moja kujadili siasa na jambo jingine kabisa kuongoza chama cha kisiasa kinachokusudia kunyakua madaraka ya serikali ya kikoloni na mtu ilibidi ajitayarishe kwa lolote linaloweza kutokea.

Nyerere alikuwa mwalimu aliyefundishwa na Wakatoliki wa Roma na alipitia mfumo huo ambao huwafanya wale walioupitia wawe watiifu na waaminifu kwa vyote viwili kanisa na serikali.

Vile vile Nyerere alikuwa chini ya ushawishi wa Padri Richard Walsh aliyepanga nafasi yake ya masomo ya juu nchini Scotland...sidhani unahitaji kufundihswa ukaelewa kuwa Kanisa na mamlaka za kikoloni zote zilikuwa adui wa siasa za kiafrika. Na inaasemekana kwamba Padri Walsh alikuwa na "ushawishi wa kutosha juu ya maisha na fikra" za Nyerere. Alimlea Nyerere na alimfanya ajiunge Edinburgh University na hiyo haikuwa sababu kwamba arudi kuipinga serikali. ....Kanisa lilimtarajia Nyerere abakie kwenye kazi ya Ualimu katika shule yoyote ya misheni nchini Tanganyika...na hilo lipo kwenye hiyo hotuba aliyooitoa BANGUSILO hapo juuu Mwenyewe Nyerere alilisema wazi hilo

Nyerere alikuwa ndio kwanza amerudi toka masomoni nchini Uingereza mwaka uliopita na alikuwa anataka kutulia aanze maisha.....wale vijana wa mjini aliowakuta wakicheza katika siasa mjini Dar es Salaam kama Abdulwahid na mdogo wake Ally, na Dossa Aziz walikuwa matajiri wakiishi ndani ya mazingira yao wenyewe.

Nyerere alijua yeye kama kamwe asingeweza kujenga msingi wa kisiasa katika mazingira ya Dar es Salaam ya miaka ya 1950 ambako siasa ilichukua tabia za Waislamu(jambo ambalo baadhi ya posters humu ndani hawataki lisemwe lakini ndio hali halisi ilivyokuwa Dar ya 1950's) anyway mwanzoni Nyerere hakutaka kulikubali shauri hilo.

Uongozi na busara wa chama cha TAA ulielewa na kutambua thamani ya elimu ya Nyerere na uwezo wake kwa uongozi wa baadaye wa chama na nchi yenyewe....si hivyo tuuu Abdulwahid pamoja na watendaji wa TAA waliamini kwamba kuwa na Mwafrika aliyeelimka sana nchini kama rais wa chama kungeimarisha uongozi wake na kutoa sura nzuri machoni pa serikali ya kikoloni.

Nyerere alipata kusema kwamba, ilikuwa dhahiri yake kufundisha kwa muda kisha aingie kwenye siasa. Hatimaye Nyerere alifanywa kuukubali ule uongozi ambao TAA ilimpa....na shindano baina ya aliyekuwa rais, Abdulwahid na Mwalimu wa shule asiyefahamika, Julius Nyerere, lilifanyika kwenye Arnatouglo Hall 1953(Hivi ule ukumbi sijui wameufanya nini MAFISADI sintoshangaa kusikia kauziwa mtu) mind you hii ilikuwa nje ya duara la uongozi wa TAA ambao ulimpendekeza kugombea, Nyerere alikuwa mgeni kabisa kwa wote waliokuwa na haki ya kupiga kura.

Shughuli za kisiasa za Nyerere zinaanza tangu siku hii. Hapa alikuwepo Nyerere, mgeni na mtu aliyekuwa hana historia ya kuongoza mapambano ya watu dhidi ya serkali ya kikoloni....nadhani kuna umuhimu MOHAMMED SAID akakitoa kile kitabu kwa kiswahili ili watu wengi wakipate na kukisoma
 
-bwa haa haa ha huko ndiko ulikotaka kufika toka mwanzo ulikuwa unapinda pinda kona.......hii thread ni nzuri sana ila mkiendelea kuingiza mambo kama haya tutabishana na mwishowe itahamishiwa kwa akina x-paster na maxshimba....

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee.
sawa kabisa......
 

mambo ya kumkoma Nyani GILADI ndio haya

Nyerere anasema alikuwa nakuja Dar na Baskeli lakini baadae akina Sykes wakawa wanamrudisha na gari
 
 
anyway wakija watu serious nitajadiliana nao


naona watoto washaanza kuingia humu
 
 
anyway wakija watu serious nitajadiliana nao


naona watoto washaanza kuingia humu
Halfu sijaona mahali popote ulipomtaja John Rupia alivyotoa zile pesa 1200 kumlipia Nyerere faini maana alibidi afungwe. Sasa kwako wewe John hayupo akilini mwako?
 
ndugu zangu someni makala ya mmisionari wa MARYKNOLL. wanadai walimsaidia Mwalimu Nyerere kwa namna mbalimbali ktk harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. kilichoandikwa ktk makala hii ni kipya kabisa katika duru za siasa zetu na kimenishangaza sana.




 
Last edited:
Mada hii utawaona waislam na lawama zao kama ambavyo wamesha zuka akina GT mh haya .
 
Kwanza kasome histoia ya TAA ya 1950's kisha lete listi ya uongozi halafu nitajie wakristo wangapi walikuwepo mle
sijabisha woote walikuwa waislamu......unayoyasema sibishi hata chembe......

BTW hivi mzee mchumikiate bado yupo hai?
kuna kitu wakuu inabidi tufanye tafiti zaidi hii thread inahitaji tafiti......nuimetoka kumsikia mohamed said sasa hivi

PodOmatic Player

nilishawahi kumskia sana na nitaendelea kumsikia....

Kuna habari weqwe ndio umeanzisha ile ZE UTAMU mpya ni kweli?
ni kweli mkuu.....
 
anyway wakija watu serious nitajadiliana nao naona watoto washaanza kuingia humu

Mkuu Gt nafikiri kinacholeta utata hapa ni miaka na hiyo hotuba ya Mwalimu bahati mbaya haikuingia kwenye detail kuhusu miaka.

Mwalimu alisoma Makerere mwaka 1943 hadi 1945 na kupata cheti. Ni huo mwaka 1945 yeye na wanafunzi wenzake walipoanzisha chama kilichoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; yeye akiwa katibu. Wakati huo kulikuwa na chama cha wasomi nchini kilichoanzishwa 1929 kilichojulikana kama African Association, AA, lakini hakikuwa cha siasa.

Baada ya kumaliza masomo alirudi Tanganyika na kuwa Mwalimu shule ya Kikatoliki Saint Mary's Tabora. Hata hivyo mwaka 1949 aliondoka nchini tena kwenda Uingereza kuchukua masomo ya Uchumi University ya Edinburgh na kurudi nchini mwaka 1952. Hivyo alikuwa mwanafunzi wa kuanza kusoma hicho chuo na kupata degree.

Ninachotaka kusema ni kuwa tunachotakiwa kuangalia ni hii miaka 1945 hadi 1952, je ni harakati zipi zilizokuwepo kuhamasisha Watanganyika kudai uhuru. African Association ilibadilika na kuwa Tanganyika African Association, TAA, mwaka 1948 lakini haikuhusika na kudai uhuru - sana sana kutetea haki za wafanya kazi na ndio maana ilivumiliwa na wakoloni.

GT, unao umri gani ?
 
Zakumi,
Alichofanya Nyerere ni kuunganisha pamoja juhudi zote za kupigania uhuru kote nchini chini ya TANU. That was no small feat, Karl Peters notwithstanding.

Jasusi:

Mada inasema watu muhimu katika historia yetu. Kama mwanzilishi angesema watu watakatifu au watu weusi katika historia ya nchi yetu basi Karl Peters asingekuwemo.

Kazi ya kuunganisha makabila yote na kuyaweka kwenye utawala mmoja. Na kuanzisha central government was not a small feat either.

Karl Peters angekuwa mtu mweusi, alichofanya hakitofautiana na alichofanya Shaka Zulu.
 
Wakuu, mmeona nyerere aliyofanya sio sahihi, hawa jamaa wenzake ndo sahihi eti.Wanashinda wanatembea na kuomba omba wakati mali wanazo zinaondoka tu.
 

Ni nani anasema kuwa AA haikuwa ni chama cha kisiasa??? Hapa ndipo mnaleta mapungufu katika mijadala kwa kutokuwa na objectives za uchambuzi.
 
halfu sijaona mahali popote ulipomtaja john rupia alivyotoa zile pesa 1200 kumlipia nyerere faini maana alibidi afungwe. Sasa kwako wewe john hayupo akilini mwako?

tatizo lako husomi post zangu rudi nyuma utaona nimetaja listi ya watu zaidi ya 10 na rupia wasa mong them
 
Mada hii utawaona waislam na lawama zao kama ambavyo wamesha zuka akina GT mh haya .

Right on,

wanachotaka wao kusema hapa ni kuwa watu muhimu katika historia yetu ni waislam au watu wa pwani pekee
 
Unaambiwa kwenye uchaguzi ule wa TAA Phombeah ndiye aliyekuwa mfawidhi wa Arnatouglo Hall alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo.

Siku ile ya uchaguzi Phombeah aliwaomba wote wawili Abdulwahid na Nyerere kutoka nje ya ukumbi ili uchaguzi uanze....na ukizungumza na wazee pale nje ya msitiki wa Manyema watakuambia kuwa wiki nzima kabla ya uchaguzi Phombeah alikuwa akizunguuka huku na kule akimfanyia kampeni Nyerere....lakinii hakukuwa na haja ya kufanya hivyo, duara la ndani kabisa la TAA la Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz na Rupia lilikuwa tayari limekwishaamua kumfanya Nyerere awe rais wa chama....Uchaguzi ilikuwa kutimiza utaratibu tu.


Baada ya Abdulwahid na Nyerere kutoka nje upigaji kura ulianza Abdulwahid "alishindwa" uchaguzi - kushindwa kwa mara ya kwanza katika maisha yake yote ya kisiasa....yap Nyerere alishinda uchaguzi huo dhidi ya Abdulwahid aliyekuwa rais wakati huo kwa kura chache sana....lakini sijui ni kura ngapoi labda mwenye dataz zaidi anaweza kuzileta

Huu ulikuwa ndio mwanzo na mwisho kwa ushawishi wa familia ya Sykes katika chama cha TAA na mwanzo wa shughuli za kisiasa za bwana Juliasi kambarage Nyerere aka Babu wa Taifa na unaambiwa tangu siku ile historia ya kisiasa ya Tanganyika kamwe haikuwa ile ile tena.

Inastaajabisha kitu kama hiki cha masafa ya maisha ya Nyerere hakijaandikwa au kupewa umuhimu na waandishi wa vitabu vya historia ya Tanganyika...lakini uzuri wa zama hizi za internet hawawezi kufunika huu ukweli

Na nNyerere mwenyewe alikiri kuwa katika kazi yake yote ya kisiasa Nyerere katu hajapambana na mpinzani mgumu kuliko Abdulwahid. Shindano hili baina ya Abdulwahid na Nyerere limekuwa hekaya...miongoni mwa wazee wetu na baadhi ya taarifa zinasema kuwa Abdulwahid alishinda uchaguzi ule, wengine wanasema Nyerere alishinda kwa kura moja; taarifa nyingine inasema kwamba wanachama wa TAA ilibidi wapige kura mara tatu ili kupata mshindi kwa kuwa zilikuwa zikifungana. Kutokana na kitabu cha Mohammed Said MMOJA KATI YA INSIDERS waliokuwepo pale AnaToglo Dossa Aziz alisema kwamba Abdulwahid hakushindwa katika uchaguzi ule .

Ili kuweka mashaka yaliyowakabili Abdulwahid, Nyerere na uongozi wa TAA, hususani ile duara la ndani zaidi, mtu lazima atambue kwamba Waislamu ndio waliokuwa wengi mjini Dar es Salaam na walikuwa wamedhibiti siasa za mtaani(JAMBO AMBALO WATOTO WENGI HUMU HAWATAKI KULISIKIA LAKINI NDIKO TULIKO TOKANA NDIO UKWELI WENYEWE HUO)

Waislamu wachache sana walikuwa na imani na wale Wakristo walioelimishwa na Wamishonari.... wakristo walionekana kuwa wako karibu na serikali ya kikoloni kupita kiasi kuweza kushika nafasi za uongozi katika harakati za kugombea uhuru. Na watu waliutumia uchaguzi ule kuonesha pingamizi lao kwa Nyerere.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…