historia itabakia kuwa historia na haiwezi kubadilishwa wala kuongezwa chumvi,kama waislamu ndio walioanzisha vuguvugu la kudai uhuru basi hiyo ni historia na ilikuwa hivyo,sasa naona watu wengine wanakuja hapa na kudai mjadala umetekwa na kikundi cha watu wachache wadini,sio ukweli na tusipindishe mada
wengi wetu hapa hatuijui historia ya tanzania wakati kipindi cha vuguvugu la kudai uhuru,mengi tunayoyajua ni hadithi za kina mkwawa,carl peters na nyerere na karume tu kwani hayo ndio yaliyoandikwa sana katika vitabu tulivyotumia shule na secondary,sasa kama wapo wenye ufahamu kwa sababu wamesoma ama kuelezwa na wenye ufahamu jinsi mambo yalivyokuwa kwanini upinge bila kuweka fact zako tena kwa kusema hoja imehamia kwenye udini?
uingereza wenyewe kwenye historia yao wanasema kuwa nchi yao ilikuwa ni ya wakristo sembuse tanzania kuwa vuguvugu la kudai uhuru lilianzishwa na waislam?history ni history na itabaki kuwa history