Chifu mkuu
JF-Expert Member
- Jan 6, 2025
- 857
- 926
Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, wamewakamata watu nane kwa kujihusisha na kilimo cha bangi akiwemo Linus Nazalius
Mhagama maarufu Malifedha ambaye ndiye aliyegawa mbegu za bangi katika Kijiji cha Limamu na kuwashawishi wenzake kuwa bangi inalipa ambapo kwa mujibu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, bangi inayolimwa kijijini hapo ni kali kuliko ile ya Arusha (cha Arusha).
Wengine waliokamatwa kwa kulima bangi ni Abeli Mhagama, Jenista Mhagama (sio Waziri
wa Afya), Kaspari John Pili, Makarius Mhagama, Anodi Alois Mhagama na Hassan Rashid Haule.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Malenya, amefanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho na kuwaonya kuacha kilimo cha bangi kwakuwa ni hatari kwa ustawi wa Taifa na ni kosa kwa sheria no 5 ya 2015 ya kudhibiti
na kupambana na dawa za kulevya akiwakumbusha kuwa kwa yeyote anayezalisha bangi hukumu yake ni miaka isiyopungua 30.
#EastAfricaTV