Watu saba wakamatwa kwa tuhuma za kuteka na kumuuwa mfanyabiashara, Morogoro

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watu saba wanaodaiwa kuhusika na tukio la utekaji na mauaji ya Bernad Masaka (43), mfanyabiashara wa maduka ya nyama na Katibu wa Wachinjaji wa Nyama mkoani humo Juni 1, 2025

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Alex Mkama amesema mnamo Juni 1, 2025 Masaka alitekwa na Stanley Ng’ambi maarufu Jaja (31) mfanyabiashara mkazi wa Mkundi aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Premio

Ng’ambi, akiwa na watu wengine walimlaghai masaka enzi za uhai wake kuwa wanakwenda eneo la Makunganya kwa lengo la kununua Ng’ombe wa biashara, baada ya kuingia ndani ya gari ndipo walimuua kwa kutumia vitu vyenye makali kisha kuubeba mwili wake na kwenda kuutupa huko eneo la majengo, Kijiji cha Manga, Kata ya Mkata Wilaya ya Handeni mkoani Tanga

Mkama amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa biashara, baada ya kukamatwa watuhumiwa hao waliwaongoza Polisi hadi mahali walipotupa mwili wa marehemu, pia wamefanikisha kupatikana kwa gari hiyo Toyota Premio lililotumika katika uhalifu huo na pikipiki ya marehemu aina ya Boxer

Kamanda Mkama amewataja watuhumiwa hao ni Stanley Ng’ambi maarufu Jaja (31), Bahati John (44), Japhet Michael (29), Yusuph Mkamba (27), Nickson Ibrahim (43), Robson Rite (47) na Ernest Msiet (37)

​
Chanzo: Mwananchi_official
 
So sad namfaham vzr Benard Masaka niliiwahi kufanya nae kazi mahala fulani hapo Morogoro, alijitafuta akakaa sawa leo hii amepotezwa kizembe na watu kwa tamaa ya biashara. Binadamu tumekuwa wanyama halisi. RIP Masaka!!
 
Attachments

  • Screenshot_20250703_133953_Instagram.jpg
    Screenshot_20250703_133953_Instagram.jpg
    781.4 KB · Views: 46
Yani wivu wa kibiashara unauwawa hivi hivi kisa unapiga pesa kwenye biashara tutakimbilia wapi kwa Sasa yani ata biashara yako mwenyewe unauwawa😢
 
So sad namfaham vzr Benard Masaka niliiwahi kufanya nae kazi mahala fulani hapo Morogoro, alijitafuta akakaa sawa leo hii amepotezwa kizembe na watu kwa tamaa ya biashara. Binadamu tumekuwa wanyama halisi. RIP Masaka!!
Nifahamishe vizuri, maana nami nimewahi kufanya biashara ya nyama Moro miaka ya nyuma.
 
Yani wivu wa kibiashara unauwawa hivi hivi kisa unapiga pesa kwenye biashara tutakimbilia wapi kwa Sasa yani ata biashara yako mwenyewe unauwawa😢
Kifo hakikosi sababu

Ova
 
Nifahamishe vizuri, maana nami nimewahi kufanya biashara ya nyama Moro miaka ya nyuma.
Huyu jamaa alikuwa ni mlinzi kwenye media moja pale Morogoro, baadae aliachishwa kazi, akaanza kujitafuta kwa kuanza biashara ya bucha moja ya nyama pale maeneo ya sabasaba. Baadae akakaa sawa na kuwa na mabucha mengi, kifupi alijipata kiasi chake na hakuwa na tamaa na maisha ya kuonekana.
 
Hata kama amepinda ndo umuue?
Why?
Siku zote tunapinga haya mambo ya kuchukuliana,kupotezana uhai
Kifalafala
Mtu anakosoa unamtoa uhai
Mtu una dhulumiana nk mnatoana uhai,sema ni mambo ambayo huwezi kumzuia mwanadam maana hakuna kiumbe katili kama mwanadam,
Siku zote kifo hakikosi sababu

Bongo sahvi no kuishi kwa timing tu

Ova
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limewakamata watu saba wanaodaiwa kuhusika na tukio la utekaji na mauaji ya Bernad Masaka (43), mfanyabiashara wa maduka ya nyama na Katibu wa Wachinjaji wa Nyama mkoani humo Juni 1, 2025

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 3, 2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Alex Mkama amesema mnamo Juni 1, 2025 Masaka alitekwa na Stanley Ng’ambi maarufu Jaja (31) mfanyabiashara mkazi wa Mkundi aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Premio

Ng’ambi, akiwa na watu wengine walimlaghai masaka enzi za uhai wake kuwa wanakwenda eneo la Makunganya kwa lengo la kununua Ng’ombe wa biashara, baada ya kuingia ndani ya gari ndipo walimuua kwa kutumia vitu vyenye makali kisha kuubeba mwili wake na kwenda kuutupa huko eneo la majengo, Kijiji cha Manga, Kata ya Mkata Wilaya ya Handeni mkoani Tanga

Mkama amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa biashara, baada ya kukamatwa watuhumiwa hao waliwaongoza Polisi hadi mahali walipotupa mwili wa marehemu, pia wamefanikisha kupatikana kwa gari hiyo Toyota Premio lililotumika katika uhalifu huo na pikipiki ya marehemu aina ya Boxer

Kamanda Mkama amewataja watuhumiwa hao ni Stanley Ng’ambi maarufu Jaja (31), Bahati John (44), Japhet Michael (29), Yusuph Mkamba (27), Nickson Ibrahim (43), Robson Rite (47) na Ernest Msiet (37)

Chanzo: Mwananchi_official

Wmempigia simu, then wakamuua, akili za hovyo sana hizi,
 
Back
Top Bottom