Watu sita wa familia moja wanusurika kwa ajali ya gari wakitoka Dar kuelekea Mwanza

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Gari aina ya Toyota Harrier lililobeba watu sita wa familia moja limepinduka baada ya kuacha njia na kuingia kwenye mtaro.

Ajali hiyo imetokea leo Desemba 20, 2024 eneo la Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga, saa 9 mchana.

Mmoja ya waathirika wa ajali hiyo, Diana Willibard amesema gari hilo ilianza kupata shida wakiwa Tinde.

"Tulikua tunatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza tulivyofika Tinde gari likapata shida na kuzima, hivyo tukaomba msaada wa gari lingine aina ya Toyota Noah kutuvuta ili kutusogeza eneo ambalo tutapata msaada.

“Tulipofika eneo la Kivumbi bomba lililofungwa kutuvuta likakatika na gari likapinduka na kuingia kwenye mtaro,” amesema Diana.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba, askari wamekwenda eneo la tukio.
Screenshot 2024-12-20 183108.png
 
si vyema sana kusafiri usafiri mmoja watu wa familia moja!, kama mkiwa wengi heri mjigawe tu.
pole kwa wahanga.
kipindi kama hiki famili husafiri kwenda mikoani kwa private car zao
 
Gari zenyewe tukinunua haziendi service Wala Nini, ni roho mkononi.
 
Gari aina ya Toyota Harrier lililobeba watu sita wa familia moja limepinduka baada ya kuacha njia na kuingia kwenye mtaro.

Ajali hiyo imetokea leo Desemba 20, 2024 eneo la Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga, saa 9 mchana.

Mmoja ya waathirika wa ajali hiyo, Diana Willibard amesema gari hilo ilianza kupata shida wakiwa Tinde.

"Tulikua tunatoka Dar es Salaam kwenda Mwanza tulivyofika Tinde gari likapata shida na kuzima, hivyo tukaomba msaada wa gari lingine aina ya Toyota Noah kutuvuta ili kutusogeza eneo ambalo tutapata msaada.

“Tulipofika eneo la Kivumbi bomba lililofungwa kutuvuta likakatika na gari likapinduka na kuingia kwenye mtaro,” amesema Diana.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kwamba, askari wamekwenda eneo la tukio.
View attachment 3181013
Hii ni habari nzuri na njema. Mungu awajaliekutokuwa na hofu wakati huu mgumu wakikumbuka.
 
Back
Top Bottom