Watu tunajisahau sana, mambo gani ya msingi inabidi tukumbushane July hii?

Watu tunajisahau sana, mambo gani ya msingi inabidi tukumbushane July hii?

Pesa si tatizo ila usimamizi ndio tatizo.

Kabla hujapigania kipato kikubwa, jifunze kusimamia kidogo kilichopo.

Usisubiri kuwa tajiri ndipo ujifunze nidhamu.
 
Mindsets is everything Haijalishi unaishi wapi au wewe ni nani

Ukiwa na poor mindset huwezi kufikia 1% ya watu bora bali utakua 99% ya watu wa kawaida

Unatakiwa kufanya vitu vya utofauti na kufanya kwa ubora wa hali ya juu

Akili yako ndo kila kitu

Ukiyumba mindset UMEKWISHA
 
Kuna jamaa mmoja anajikuta ni askari hodari wa ku push agenda ya NoreNoel ila ikifika usiku kwenye magroup ya watsap yeye ndiye kinara wa kutuma ma video ya porn. Huwa nabaki kujiuliza ana matatizo ya kisaikolojia au ndio mmoja ya wahuni aliowasema Polepole.
Porn addiction ni tatizo la kisaikolojia, kuna watu hawawezi kulala au kwenda makazini bila kuangalia porn na kujichua.
 
Kuna jamaa mmoja anajikuta ni askari hodari wa ku push agenda ya NoreNoel ila ikifika usiku kwenye magroup ya watsap yeye ndiye kinara wa kutuma ma video ya porn. Huwa nabaki kujiuliza ana matatizo ya kisaikolojia au ndio mmoja ya wahuni aliowasema Polepole.
Ni huzuni kwa kweli
 
Tujali na kutunza afya zetu kwa kula mlo kamili na kukumbuka kutumia kinga kwani mtu ni Afya😎
2025 mambo yamekua mengi sana, haya tukumbushane.

Naanza:
  1. Tafuta hela nyingine zote ni stori tu.

  2. Acha roho mbaya, chochote kibaya utakachofanya kwa mwingine kitakurudia.

  3. Usikimbie wanao na majukumu ya malezi kisa umegombana na mzazi mwenzako.

  4. Usiendekeze ulevi (pombe, mihadarati, ngono n.k).

  5. Haki na wajibu kwanza, ila siasa siyo vita, kuna maisha baada ya uchaguzi.

  6. Akiba haiozi (hasa kwenu wanawake, ukipewa hizo sapampa mnazopigia kelele, zielekeze kwenye mambo ya msingi na siyo kununua mawigi.)
Endeleza mengine ya msingi ya kuwakumbusha wanajukwaa!
 
Back
Top Bottom