Watu umri wangu tuliokua wote wana maisha mazuri sana, sijui mimi nineteleza wapi

Watu umri wangu tuliokua wote wana maisha mazuri sana, sijui mimi nineteleza wapi

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Yaani kuna muda napata mawazo nimeteleza wapi yaani kila nikikutana na wenzangu tumekuwa wote wengine umri mmoja tu ila wako vizuri sana kimaisha.

Sasa mimi sijui nilikosea wapi kuchanga karata zangu maana mpaka sasa napanga wenzangu wana mijengo ya maana magari ya kifahari mimi nipo Manzese kwa mfuga mbwa huku nimepanga vyumba viwili daaah.
 
1
IMG_20210703_125151.jpg
 
Huo ndo uchawi wenyewe.. basi roho inakuuma mno [emoji28][emoji28]
 
Tanzania Ni Tajiri!!!!😂😁😀😃😄😄😄😅😅😆😄😄
 
Ndugu yangu unatamani kujenga nyumba kwani utaishi milele hapa duniani?

Mfalme Suleimani alijenga majumba na mahekalu ya kifahari. Je, leo hii Suleimani yupo wapi na mahekalu yake???

Ishi maisha yako, ridhika na kile ulichonacho, tumia muda wako kumtafuta MUNGU na ujifunze "MUNGU anataka nini kwako".
Yashike kwa bidii yale yote MUNGU anayotaka. Siku zako za kuisbi zikiisha, pumzika kwa amani maana utakuwa na tumaini la kuishi tena.
 
Yesu Mwenyewe mpaka anainua kwa Sir God alikua hajajenga.

We unazungumzia kujenga kwani ulikuja kulinda dunia mkuu!!!!?

Kula bata kufa sio ubaki unateseka na kujenga😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Kweli kabisa. Watu wanajenga hapa kana kwamba watakaa hapa milele. Chukulia km mwendazake vile, yale majengo aliyoyaacha anayafaidi vipi huko aliko?
Acha ujinga ujenge kwani umeskia hapa Duniani Ni makao yetu ya kudumu..mji wetu uko mbinguni Hapa kikubwa tafuta hela ule maisha/matunda
 
Maisha yana siri nyingi ndugu.

Jifanyie tathmini ya mwenendo wako, ya watu yaache tu.

Wakati tuko chuo kuna jamaa kila mtu alikuwa anamtamani, hakuna siku ameishiwa; simu kali yeye, mademu wakali yeye... watu tunapambana na mikopo, mwenzetu anakula bata kama zoooote. Siri ya mafanikio wote tulikuwa tunajua ni graphic designer. Siku moja, news zinakuja kauawa kwenye mapambano na polisi.... tukabaki tunashangaa. Kumbe mwenzetu shughuli nyingine alikuwa dereva wa wazee wa kazi(majambazi), sometimes anapotea tunajua ni bata, kumbe yuko kazini. Tangu hapo nimejifunza ku-mind my own business, vya watu viache tu; vina siri sana, ingawa haimaanishi kila mwenye mafanikio ni magumashi, ila usijipime sana na wenzako. Kuna siri nyingi sana
 
Back
Top Bottom