Maisha yana siri nyingi ndugu.
Jifanyie tathmini ya mwenendo wako, ya watu yaache tu.
Wakati tuko chuo kuna jamaa kila mtu alikuwa anamtamani, hakuna siku ameishiwa; simu kali yeye, mademu wakali yeye... watu tunapambana na mikopo, mwenzetu anakula bata kama zoooote. Siri ya mafanikio wote tulikuwa tunajua ni graphic designer. Siku moja, news zinakuja kauawa kwenye mapambano na polisi.... tukabaki tunashangaa. Kumbe mwenzetu shughuli nyingine alikuwa dereva wa wazee wa kazi(majambazi), sometimes anapotea tunajua ni bata, kumbe yuko kazini. Tangu hapo nimejifunza ku-mind my own business, vya watu viache tu; vina siri sana, ingawa haimaanishi kila mwenye mafanikio ni magumashi, ila usijipime sana na wenzako. Kuna siri nyingi sana