Watu umri wangu tuliokua wote wana maisha mazuri sana, sijui mimi nineteleza wapi

Watu mnapuuza kujenga nyumba na kujivunia nyumba za kupanga kwamba hi dunia tunayoishi si mahali pa kudumu,hao watoto na mke ukifariki umewajengea uchumi gani wajitegemee?mfano ukifa una umri wa miaka 25 na una watoto wawili wadogo umewaacha na mke kwenye nyumba ya kupanga umewaachia mateso tu.Umaskini ulioacha na akili ya uvivu uliyokuwa naye inabaki kwa watoto na wajukuu,familia inawaza ni laana na kujikatia tamaa kumbe baba alikuwa mvivu na kucheza bao kijiweni
 
Hakikisha ungafanya kila unachokitaka kabla hujafa.
Kama unachotaka ni kujenga nyumba kubwa basi jenga.

Trust me kukaa kwenye nyumba kubwa nzuri yenye kila kitu tena na familia yako tu na kukaa kwenye mifupa ya mbwa ni vitu viwili tofauti hasa ukiwa umepanga.

Usisikilize hawa wanaosema utakufa utaviacha kwani nani hafi.
Na hii ni akili ya kibinafsi, kijinga na kimasikini kwani ukifa si utawaachia watoto wako.
Au ni vizuri kuwaacha watoto kwenye mifupa ya mbwa?

Au una uhakika utakufa peke yako tu?

Mambo ya ajabu sana haya.
 
Yesu Mwenyewe mpaka anainua kwa Sir God alikua hajajenga.

We unazungumzia kujenga kwani ulikuja kulinda dunia mkuu!!!!?

Kula bata kufa sio ubaki unateseka na kujenga😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Ina maana wewe hutokuja kuwa na familia mkuu?

Au bado hujakua kuanza kufikiria familia yako ya baadae utaiacha vipi?

I mean ingekuaje wazazi wako wangekuwa na mawazo kama haya?
 
Shida tunaangalia walio tuzid badilisha mtazamo angalia uliowazid kisha mshukuru aliekuumba kisha endeleza mapambano
 
Mbona hujilinganishi na wale wa umri wako waliokufa kabisa ? Pambana kwa uwezo wako. Wakati mwingine kuwa hai ni mafanikio pia mkuu tena mshukuru Mungu.

Sent from my SM-G9250 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo umechanganya wivu na umaskini
 
Jitahidi kuwa bora zaidi ya Jana!
Jilinganoshe na wengine kupata motivation tu kuona kuwa mambo yanawezekana na sio kukudharau Mkuu!!
 
Hii dunia tunapita mwisho wa siku maua hunyauka,kumbukumbu husaulika na Historia zinafutika.

Unadhani Watoto watakaozaliwa 2300 Watamujua Magufuli???.relax siku ukifukiwa na Mchanga hamna atakaye kukumbuka wala kukumbuka uliacha nini.
Hizi ndio kauli zenu za kujipa matumaini!!?
 
Acha ujinga ujenge kwani umeskia hapa Duniani Ni makao yetu ya kudumu..mji wetu uko mbinguni Hapa kikubwa tafuta hela ule maisha/matunda
Asante kwa ujumbe mzuri hapa sipo kwetu ndio tufanye kazi kwa bidii Mungu akikubariki zaidi utajenga na kununua gari ila sasa mkuu ishi kana kwamba Mungu amekupatia siku ya leo ifanyie kazi kwa bidii siku ya leo kana kwamba kesho hutafika halafu upatapo riziki toa zaka yaani pato lako mtolee Mungu au mshukuru yeye kwa kukuwezesha kukupatia riziki na penda sana kuwasaidia wasiojiweza na Mungu atakuwezesha na kukulinda kwa kuwa wewe unawajali wengine kwa kile kidogo unachopata!!!
Na Mungu hatakuacha jinsi ulivyo atakubariki zaidi na zaidi katika maisha yako ya kila siku na kusikia kilio chako kila umwitapo!!
Fanya Hivyo Mkuu!!!!
 
Je ulikataa shule wakati wenzako wanasoma?
 
Hii ni kweli na asilimia kubwa ya mafanikio ya watu behind the scene Kuna uhalifu mkubwa sana uwe wa damu or wizi
 
Chumba na sebule!! Mbona wewe umetusua mzee...mimi jirani yako hapa chumba kimoja nasumbuana na mwenyenyumba.
Leo zamu yako kununua umeme mkuu
 
Mkuu bila shaka wewe ni graduate hauko peke yako.Kikubwa dua mbona mzee mpili katoboa uzeeni,you never know ipo siku utaiangalia hii thread(Uzi).
Alafu utajichekaa sana your time will come ila husle mkuu hata mimi niko kama wewe.Ipo siku!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…