Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Kama unafuatilia mtandaoni account za CAF champions league, tangia Simba imeanza kufanya vizuri mashindano ya kimataifa, ni kama CAF au wanaoendesha account za CAF wana ushabiki fulani kwa Simba na kama wanaumia hivi inapotolewa
Siongei kishabiki, Hata Yanga nafikiri itakuwa hivyo hivyo wakianza kuzoeleka kwenye mashindano haya
Sababu unajua ni nini? Zipo 3
1. katika timu zote zinazoshiriki mashindano ya CAF, Simba ndio ina mashabiki wengi zaidi mtandaoni, na post za CAF zinazoihusu Simba hupata engagement kubwa kuliko post za timu nyingine
Kuwa na mashabiki wengi kunaifanya mashindano kuwa na uhai, au kuwa na moto 🔥🔥, na nadhani husadia pia kuvutia sponsors zaidi, kumbuka kati ya changamoto zinazokabili mashindano mengi ya Afrika ni kukosa mashabiki (tofauti na UEFA au South America)
2. Kingine ni mashindano haya yamekuwa dominated sana na timu za kiarabu na kuyafanya yaonekana kama mashindano ya Waarabu badala ya Waafrika kiujumla, kuwepo kwa timu kama Simba husaidia kuleta diversity
4. Pia katika club za Sub Sahara zinazoshiriki, nyingi huwa hazina mashabiki wengi uwanjani, achilia mtandaoni, isipokuwa kwa Simba, tuliona jinsi viwanja vya timu kama Horoya, Vipers, Cotton Sports, Mamelodi, hata timu za Shirikisho kama zinazotoka Sub Sahara kama Rivers huwa hazina mashabiki wengi kama timu za Tanzania