Watu wa JamiiForums ni wagumu sana kutoa like

Mkuu, ni vyema ukajifunza juu ya consumption habits za watu... Wachangiaji wengi wanapenda ile 'michambo' au comments anazopewa mtoa mada. Nilishawahi kuleta lalamiko kama lako siku za nyuma coz unakuta mleta mada ana likes mbili wakati aliyechangia kwenye mada yake ana likes kumi...
 
Huku kuna like za aina nyingi.
Za point nzito na zenye maana
Za kuchekesha
Za kujuana
Za kutafuta vipoozeo
Za kurudisha fadhila
N.k, we ukichunguza kwa makini utagundua hilo. Ukipata like moja we yakutosha kwani wapeleka wapi nazo hizo!!
Hahah za vipoozeo hizo lazima upate like tu
 
Mimi zangu mods wanazichukua zipo zaidi ya alfu lakini kila siku ni 600 ingekuwa chakula kingeeleweka lakini like wachukue tu
 
Mpaka tumeanza kulilia like ni Hali ngumu au ni kutafuta umarufu kuwa kila ninacho post kinaeleweka
 
Kwani usipopata hizo likes nini kinaharibika?
 
C kwel mkuu watu huwa wana Like sana tu kama mada ni nzuri, sema nilichogundua kwamba system ya jamii forum like huwa hazizidi tano, namaanisha hata wa like watu 1000 like zinazoonekana ni tano tuu, chunguza hiyo kitu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…