Watu wa Kigoma kuna salamu zenu huku

Watu wa Kigoma kuna salamu zenu huku

Kulupango

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2020
Posts
288
Reaction score
535
NIMEINUKUU PAHALA

1- Kupanda treni mpaka uwe na Kitambulisho au barua ya serekali ya mtaa

2- Kupanda treni mpaka ulale station ndio upate tiketi

3- Ukijifanya unapanda usafiri wa basi ujue utakumbana na barrier ya uhamiaji na mtakaguliwa kama wakimbizi

4- Meli yenu MV Liemba haifanyi kazi tangu 2017, na ikifanya kazi mkifika Kigoma saa moja jioni hamtoki hapo bandarini mpaka saa mbili asubuhi ili maafisa uhamiaji waje mkaguliwe kama wakimbizi (hivyo ukiwa na mgonjwa atafia hapo), Muda mwingine hufika saa nne asubuhi

5- Mkumbuke nyinyi ndio mnakasumbu ya ukimbizi kuliko mikoa yote iliyopo mipakani (Mamlaka zimewapachika kasumba za ukimbizi ili mkose pakujitetea haswa ukionekana mtu wa haki na mfuata sheria. Cc Abdul Nondo, Zitto Kabwe, Askof Kakobe, shekh ponda, n.k

6 - Kumbukeni mpaka leo wengi wenu hamna vitambulisho vya NIDA kwa kasumba mliyovishwa ya Ukimbizi na watu wenye mamlaka

7 - Nadra sana kumkuta MMANYEMA na MUHA wameajiriwa na jeshi la Tanzania, kidogo Waha lakini siyo Wamanyema kina Zitto, wengi wao hukimbilia usanii ili kupata tonge, ndio hao kina Dia, Kiba, Chege n.k

8 - Kigoma mmepigwa pigo la Udini na Ukabila, hivyo mnashambuliana wenyewe kwa wenyewe bila kujijua, msako wa wakimbizi ukija mnaanza kusakiziana Waha na Wamanyema. Mmanyema auchawi wa Tongwe na Muha uchawi wa Kibondo

9 - Mamlaka zinawasakama kwasababu mnauwezo kiakili kutokana na migebuka mnayokula, hivyo mkiachiwa nafasi itakuwa hatari

10 - Zunguka Dar es salaam nzima kila kijana muuza madafu ni MUHA, (hii inadhihirisha namna mlivyonyimwa elimu na mamlaka husika tangu enzi na enzi) . Vijana wenu wanatembeza madafu kwa Baisikeli kutoka Gongo la mboto hadi posta

11 - Leo Kigoma hakuna tena wale matajiri WAKASAI kutoka Lubumbashi mliokuwa mkiwategemea kwa ajili ya biashara zenu, kutokana na mfumo uliojengwa na mamlaka inabidi WAKASAI wakimbilie Mwanza kuchukua dagaa wa mwanza.

12 - Huku kwetu Arusha ni kawaida sana kumkuta Mkenya akiishi kwenye nyumba zetu na hata kupanga, lakini sio Kigoma: nyumba ikikutwa na Mkongomani au Mrundi hatakama kaingia kwa halali wenyeji hawakosi presha ya kuvamiwa na mamlaka.

13 - Huku kwetu sisi wamakonde tuna ndugu zetu Mozambique na wala hatufichi wala hatubabaiki, lakini huko Kigoma hakuna mtu anaweza akakubali kama ana ndugu nchini CONGO au BURUNDI.

Kwa leo naishia hapo wanakigoma: Kumbukeni vikwazo vyote hivyo vimeletwa na serekali za CCM tangu enzi na enzi, na hii ni kwasababu Jimbo la Kigoma mjini mnawapa wapinzani kila uchao ndio maana mamlaka zinaendelea kuwanyanyapaa na kuwanyanyasa. Ni aibu sana tena ushamba uliopindukia kwa mwana Kigoma kuishabikia CCM.

Kigoma
118779480_2807429939476036_2342212669361274156_o.jpg
 
Nimezaliwa kigoma nimesomea kigoma nimeajiriwa mwanza na nina mashamba makubwa kigoma asilimia 98 na ulivyoandika ni UONGO
 
Kwahiyo hata madame Joyce na mzee Mpango Ni wauza madafu,daah!basi sawa.
 
Tanzania ni moja kati ya The Poorest Countries in the World (MASIKINI ZAIDI DUNIANI) inashika nafasi ya 8 kutoka chini. ( Focus economy 2019- 23)

CCM imetufikisha hapa
 
Kigoma ni watu wakudanganywa kila inapofika wakati wa uchaguzi! Barabara kuu kutoka nyakanazi imeanza kujengwa tangu 2017 hadi sasa km 20 ndoo zimejengwa ( nyanza construction company LTD) Kigoma ni mkoa viongozi hupita kuomba kura tu wakishapata wanasahau! Umeme wa grid ya taifa umekuwa kizungumti ukija barabara kuu imekuwa shida kila mwaka masika tope kiangazi vumbi! Viongiz wakati wanapita barabara humwagiliwa ili kutoa vumbi baada ya hapo mambo yanakuwa hivohivo
 
Hiyo picha ya mwaka 2020 au 2015,nataka nimpelekee Magufuli akaichambue na kuona maendeleo yaliyoletwa na serikali tukufu ya ccm.
 
Back
Top Bottom