Watu wa kipato cha kati wengi wanaishi kwa hofu za kurogwa na ndugu na marafiki waliowazidi

Watu wa kipato cha kati wengi wanaishi kwa hofu za kurogwa na ndugu na marafiki waliowazidi

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Mtu akioata kazi nzuri au biashara ya kueleweka, akajenga Nyumba, Akawa na shamba, na gari la kusafiria au akamuongezea mkewe kadogo ka kutembelea wengi wanaona aliowazidi wanamuonea wivu au wanamvizia wamloge.

Hasahasa wale waliokulia kwenye umasikini mkali, na akapata mwanga kuliko wenzake. Wahamasishaji wakuu ni wanawake, nao kwa kuwa wengi ni wafuasi wa wajasiriagospo wanajazwa huo ujinga madhabahuni.

Matokeo yake, hofu hii inasababisha watu wengi wanakuwa na hofu nyingi ambazo zinawafanya wasisogee zaidi ya hapo.
China ndio nchi yenye mamilionea wengi vijana maana watu walipopata maisha ya kati kwao ulikuwa mtaji kwa kuwavusha kuwaweka tabaka la juu.

Hofu za kurigwa huleta kupararaizi kwa mifumo yako ya maendeleo.
Ndio maana wengi wanafikiria kustaafu na sio kuvuka hiyo levo.

Kumbuka kanuni ya Mfalme Suleiman " Ajionavyo mtu ndivyo alivyo". Kama unamuamini Mungu, uchawi ndio unatakiwa ukuogope wewe. Ishi kana kwamba haupo. Hiyo nguvu iingize katika uzalishaji na possibility thinking.

Ni hayo tu

.Barikiwa
Mtumishi Matunduizi
 
Makanisa mengi ya kilokole ya natumia kutibu uchawi, husda mizimu kama chanzo cha kupata wateja wengi, baada ya kugundua kwamba wengi wana Imani hiyo ya kurogwa, wanatoa sadaka ili wapakwe mafuta ya upako kuzuia kurogwa na kulinda mali zao,....... shit, hilo ni kwasbabu kufanikiwa kiuchumi Africa nikama muujiza wengi inakua kama 'surprise' kutajirika kwao, mpaka waenda kwa mganga (mrozi) kulinda nyumba gari na duka lao.
 
Kijana akishafika miaka 50+ na awe hana lolote mara nyingi anakuwa hatari sana kwa Jamii, hasa anapoona vijana wadogo wakifanya mambo mazito, nashauri wawe watulivu, kwani hakuna la maana sana hapa duniani, kila kitu ni cha muda tu, historia inasema hata kilwa ilikuwa kama dubai, lakini leo Pana nini?
 
Makanisa mengi ya kilokole ya natumia kutibu uchawi, husda mizimu kama chazo cha kupata wateja wengi, baada ya kugundua kwamba wengi wana Imani hiyo ya kurogwa, wanatoa sadaka ili wapakwe mafuta ya upako kuzuia kurogwa na kulinda mali zao,....... shit hilo ni kwasbabu kufanikiwa kiuchumi Africa nikama mujiza
Nadhani Tuishie Hapa
 
Jamii forum mnajifanyaga kama mnaishi mbinguni,
Mkubali mkatae kuna baadhi ya jamii bila kujikinga hutoboi
 
Jamii forum mnajifanyaga kama mnaishi mbinguni,
Mkubali mkatae kuna baadhi ya jamii bila kujikinga hutoboi
Kuna jamaa kasaidiwa kuja mjini, kaanza , kapewa connection ya ufundi simu,kaanza kapata wateja, baada ya mwaka kaanza kuona nuru, amebambaniwa hadi kasimama ndio anaanza kuhisi anarogwa, mara waganga kila weekend. Hawasalimii waliomleta mjini, wakimuongelesha hajibu kisa maelekezo ya vilingeni.

Kwa huu ujinga, utasema jamii flani haimpendi?
 
Back
Top Bottom