Martine Tibe
Ngoja nikupe ushauri wa kitalaam.
Mazoezi yana nidhamu zake na kuna aina mbalimbali ya mazoezi kuendana na matakwa ya mfanyaji.
1. Kuna mazoezi ya kujenga misuli (muscles) kujenga mwili /body building
2. Kuna wanyanyua vitu vizito weight lifter hawa hujali uzito wa hayo mazoezi
3. Kuna ya kupunguza mwili/kukata mafuta.
Namba moja 1.
Hayo ya kujenga misuli yana kanuni zake.na kanuni moja ya kwanza ni ulaji wa chakula sahihi. Ya pili ufanyaji sahihi wa mazoezi. Routine.
Kama unataka kujenga na uone mabadiliko unatakiwa ule vyakula vya kuongeza nguvu na vya kujenga mwili(protein)
Then uwe na ratiba nzuri ya ufanyaji mazoezi husika.na pia ufanye kwa kufuata sets za zoezi husika kila Reps kadhaa (8-12) zinatengeneza set moja ya mazoezi.
Hivyo zingatia uzito sahihi wa dumbell au barbell. Au kama unatumia machine.
Unapaswa upate muda wa mapumziko usiopungua 8 hrs. Usitumie sana pombe,usiwe mtu wa mabinti sana/masturbation. Kula matunda,maziwa.nyama mbogamboga n.k
Train siku 5-6 kwa week.acha siku moja au mbili ya mwili kupumzika. Then njoo unambie kama hakuna mabadiliko.ntakuangalia ntakwambia nini tatizo. Mimi ni mtalaamu wa mambo hayo. Asante.