Watu wa Mbeya, badala ya kujichubua na kuwa kama vishetani, kwa nini msitumie mafuta ya kujikinga na jua?

Watu wa Mbeya, badala ya kujichubua na kuwa kama vishetani, kwa nini msitumie mafuta ya kujikinga na jua?

Chief, umeniacha kidogo hapo, jua dar lilivo kali kiasi kile kuliko mbeya then useme mionzi ya jua ukiwa mbeya ni mikali zaid? Baridi na ubichi wote wa mbeya na iringa na njombe afu useme dar kuna hali ya unyevu unyevu kuliko kusini?
dadavua mkuu
Kwa sababu ya bahari. Miji kama Dar au Tanga, na hata Mwanza inakuwa na unyevu hewani mwingi kuliko sehemu kama Mbeya na Iringa. Na jua la Mbeya na Iringa huwa kali kwa sababu kuna kama kilomita moja na nusu ya atmophere(angahewa) hawana kwa kuwa kwao juu.

Ukiwa juu mionzi inakuwa mikali zaidi. Ndiyo maana unaonaga mapilot wakivaa ile miwani myeusi. Siyo urembo, ni kukinga macho na mionzi.

Sababu hizi mbili zinafanya jua huko kuwa kali sana. Kuna joto na kuna jua la kuchoma.
 
Pwani kuna moisture kubwa, ndio maana hata jasho linatoka jingi,
Iringa unaweza ukakaa week nzima hujatoka jasho lile la kutiririka
Huku jua likichoma kama vile upo chini ya zile magnifying lenses.
 
Tz hii sidhani kama kuna mkoa unaongoza kwa watu kujichubua kama Mbeya. Ukikuta mwanamke aliyejichubua kikweli anatisha. Sura inakuwa kama kokaragosi au kashetani hivi.

Lakini si wakulaumu. Habari ya kujichubua ipo duniani pote. Wazungu walifanikiwa kuteka akili za watu kuwa weupe ndiyo urembo. Nchi kama Korea, India, na nchi nyingine za Asia wanajichubua WaCongo na Watu wa Mbeya cha mtoto. Mafuta ya kujichubua ya Fair and Lovely yalianzia huko India. Jamaa imani yao kuwa kuwa mweupe ni urembo ni kali sana.
Sasa basi, ni nini kinasababisha watu kuwa weusi? Ni kemikali inayoitwa melanin. Hii hutengenezwa na ngozi ili kujikinga na mionzi mikali ya jua. Ni kemikali muhimu sana. Sasa hii hutengenezwa kwa wingi mtu anapochomwa na jua kali.

Sasa tuje huko Mbeya. Watu huwa wana dhana potofu kuwa baridi la Mbeya na mikoa mingine ya nyanda za juu kusini ndiyo husababisha weusi. Si kweli hata kidogo. Weusi ule unasababishwa na jua kali linalowachoma. Sehemu hizi zipo umbali kama wa wastani wa kilomita moja na nusu kutoka usawa wa bahari. Maana yake mtu wa sehemu kama Dar ana layer kubwa zaidi ya hewa inayopunguza nguvu za mionzi na kulinda ngozi yake kuliko yule wa sehemu kama Mbeya au Iringa.

Jambo jingine ni kuwa unyevunyevu(humidity) kwenye hewa kwenye mikoa hii ni mdogo kuliko sehemu kama Dar, Tanga nk. Unyevunyevu husaidia kupunguza ukali wa mionzi.

Utaona kuwa mtu wa nyanda za juu jua linampiga sana kuliko watu wa pwani. Na wengi wakienda pwani utaona ule weusi wao mzito unaanza kupungua.

Sasa basi, kwa vile tatizo ni jua kali(kama kuwa na weusi wa mkaa ni tatizo)basi hata solution iwe kuzuia kupigwa na jua kali. Moja ya njia nzuri ya kufanya hivyo ni kutumia mafuta, lotion na cream zinazosaidia kupunguza madhara ya miale ya jua kwenye ngozi.
Utaona madukani lotions zimeandikwa SPF-yaani sun protection factor- unakuta kuna za SPF-30. Ambayo inazuia zaidi ya 90% percent ya mionzi. Na zingine za juu kama SPF 40, 50 na kuendelea.

Nashauri watu wa Mbeya, Iringa, Njombe nk mnaojichubua na kuwa kama vishetani, mtumie hizi lotion, zitasaidia kwa kiasi kuweka ngozi zenu sawa.
Bro uko close-minded. Hivi ukiulizwa sample size yako ilikuwa ngapi utajibu? Una maana ukikutana na mwanamke wa Mbeya chances za yeye kuwa amejibua itakuwa asilimia ngapi? Na ni kubwa kuliko mwanamke wa mkoa upi?

Hiyo kiongozi ndio huwa inaitwa generalization au stereotyping. They often say generalizations are easy to make and don't require much brain effort which reflects the limitations of a person's intellect. Si vyema, kusema population yote iko hivyo kutokana na experience ndogo uliyonayo. Badirika kiongozi.
 
Suala la wanawake Kujikoboa lipo sehem nyingi.... ila kuna kitu watu wa mbeya wamekukosea ndo maana ukaamua ukomae nao... ukawaitwa vishetaniiii....
 
Bahati nzuri sio wengi humu ndani
 
Chief, umeniacha kidogo hapo, jua dar lilivo kali kiasi kile kuliko mbeya then useme mionzi ya jua ukiwa mbeya ni mikali zaid? Baridi na ubichi wote wa mbeya na iringa na njombe afu useme dar kuna hali ya unyevu unyevu kuliko kusini?
dadavua mkuu
Mbeya Kuna jua aisee hatua hupigi dar Kuna joto ila jua si Kali
 
Mnao jichubua na mikorogo ya mafungu, mnaitwa hukuu. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe ukienda Kyela hurudi. Hujawahi kutana na Black Beauty za Mbeya wewe.

Weusi ni rangi tu, achana na hizo nadharia za Melanin.

Nje ya mada: Kwa hiyo mtu mweusi mwenye mimba ya mtoto mweusi ukimpeleka Dar atazaa mtoto mweupe.
 
Kawaida ya sehemu zenye watu weusi kwa wingi hawajiamini,, hata Kagera ipo sana hiyo
 
Back
Top Bottom