Watu wa mijini wengi ni wagonjwa kwa sababu ya kuvaa viatu

Watu wa mijini wengi ni wagonjwa kwa sababu ya kuvaa viatu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Mwanadamu asili yake ni udongo.

Kuna connection kubwa sana kati ya udongo na mwanadamu. Hata neno Adam ambalo limeleta neno mwanadamu linatokana na neno "Adamah" la Kiebrania ambalo humaanisha udongo.

Katika kutuumba Mungu aliweka vitu katika viganja vya miguu na mikono ambayo vikikutana na Ardhi vina-trigger karibu kila kitu katika mwili wako na kukirudisha katika utendakazi wake sahihi.

Nimechelewa kujua leo kuna watu wanakuwa mamilionea kwa kufungua vituo vya tiba ambao kufanya massage za viganja vya mikono na miguu na watu wanapona visukari, figo, moyo, mapafu. Hadi hii ingefanywa vyema kama ungepiga pushup kwa viganja vikiwa wazi. Ungetembea peku muda mrefu kila siku.

Pia kwa sababu tuliumbwa uchi. Kuna connection Kubwa kati ya wewe kuwa uchi nje ya Nyumba yako ukiangalia anga. Kwa sababu Nyumba sio asili yetu, pata nafasi Mara mojamoja toka nje ya Nyumba yako uchi wa mnyama ukiwa peku, angalia anga, shika vitu vya asili utashangaa mambo yako yatakavyokunyookea. Hata kama ndoa yako nilikuwa shidani shida itaondoka.

Mtu anayeingia kazini akiwa peku, nenda shopping Kariakoo peku, hutajuta.

Wamegundua siri hii wachache, wajinga wanasrma ni uchawi.

Wako mapadri
Wako wachungaji, TB Joshua
Wako wasanii, Mpoto
Wako wengi anza sasa sio ushamba ni akili
 
Sawa ngoja tuishi humo
Tumia muda mwingi ikiwa unaikanyaga Ardhi mkuu, hutajuta.

Unaona hata Mungu alimwambia Musa na Yoshua nyakati tofauti wavue viatu alikuwa anazungumza nao mambo ya msingi.

Hata akili yako itachaji zaidi maana kuna creational connection kati yako na ardhi
 
sasa sisi tunasali tumevaa mikanzu na baibui, kumbe kuna vitu tunakosa
Hamuendi mbali sana kwa sababu huwa mnavua viatu na kukanyaga Adamah (udongo) ILS kosa ni kuweka tiles au mikeka mnapata manufaa hafifu kwa kuhusisha artificial soil. Mlitakiwa msiweke sakafu kama navii Musa alipoongea na Mungu.

Uchi ni special case unapotaka kuongea na Mungu katikati ya nature na kumshukuru kwa kukuumba hivyo ulivyo. Nakuhakikishia jaribu uone. Kesho yake tu unaweza kupewa barua ya kupanda cheo au ukapokea simu ya biashara itakayobadili maisha yako.

Don't underestimate the power of nature.
 
Unamaanisha hata chooni tuingie bila viatu?
Sijakusoma Mkuu
 
Unamaanisha hata chooni tuingie bila viatu?
Sijakusoma Mkuu
Namaanisha kanyaga Ardhi mkuu. Ya asili. Na utanufaika zaidi ukikanyaga juu ya kokoto.

Chooni kuna sakafu/tiles utapata manufaa hafifu kama ukikanyaga natural soil.

Mkwawa alikuwa na uwezo wa kuletea ligi Mzungu na asiyumbe kwa sababu alikuwa anatembea peku. Siku hizi unamtukana Mzungu kwenye media wakati kimyakimya unamuomba msaada
 
Nimeanza asubuhi hii hii, tena nimeizamisha kabisa.
Mkuu vipi kujizika kabisa kuna faida gani??
JPEG_20201113_094741_1105190237196000945.jpg


Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Sawa hayo mengine huwa nayafanya sana,ila hili la kutoka nje uchi ngojea mpaka nimalizie ukuta wa nyumba yangu ntalifanya sana mkuu,si unajua kuishi kutamu...
 
Ngoja nitoke nje Uchi sasa hivi nione km nikweli hayo unayosema
Kuna siku ilinyesha mvua ya mawe hatari . nikasema isinichezee, nikatoka nje uchi nikainyooshea Mkono nikaiambia ikome kama inataka inyeshe ILS sitaki kuna hayo mawe hatarishi.

Dakika TATU hazikupita ikakata ikaanza rasharsha.

Tatizo mnadanganywa sana makanisani. Mungu alipomuambia Adamu atavitawala na kuvitiisha Adamu hakuwa na Nguo wala viatu. Kuna mambo special kesi ikiwa uchi na peku nature utaitawala kama mtoto Mdogo au housegirl.

Sio uchawi Bali ni Mungu ndio alitoa hayo maelekezo. Kwa sababu ya ujinga Leo watu wanatawaliwa na baridi, joto, mvua etc wakati vyote ni vyao walipewa wavitawale
 
Sawa hayo mengine huwa nayafanya sana,ila hili la kutoka nje uchi ngojea mpaka nimalizie ukuta wa nyumba yangu ntalifanya sana mkuu,si unajua kuishi kutamu...
Big up mkuu.
Hata Alexander the great dogo aliyetawala ulaya hadi India alikuwa na ajili nyingi na uwezo Mkubwa maana alisoma kwa philosopher nguli Aristotle nadhani na walikuwa wanafundishwa wakiwa uchi utotoni.

Kuna mambo ukimfundisha mwanao akiwa uchi na peku kwenye Ardhi hatayaacha hata uzeeni
 
Namaanisha kanyaga Ardhi mkuu. Ya asili. Na utanufaika zaidi ukikanyaga juu ya kokoto.

Chooni kuna sakafu/tiles utapata manufaa hafifu kama ukikanyaga natural soil.


Mkwawa alikuwa na uwezo wa kuletea ligi Mzungu na asiyumbe kwa sababu alikuwa anatembea peku. Siku hizi unamtukana Mzungu kwenye media wakati kimyakimya unamuomba msaada
Basi sawa mkuu,,
 
Kwenda kariakoo peku c utard miguu ina vidonda??🙄🙄🙄
Mkuu vidonda ni siku ya kwanza tu, baadaye unakomaa. Licha utapata tija hafifu kwa sababu sehemu Kubwa ni pavings, lami na slabs. Ila utamzidi aliyeenda na viatu mkuu
 
Back
Top Bottom