Watu wa mikoani tukienda Dar tunang'ara ndani ya muda mfupi,tukirudi makwetu tunapauka

Watu wa mikoani tukienda Dar tunang'ara ndani ya muda mfupi,tukirudi makwetu tunapauka

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Kuna dada wa kazi alienda huko daslam baada ya mwezi akarudi baada ya kupata msiba,siku anarudi ngozi kama mzungu.alikaa kuomboleza kwa wiki mblIi akafubaa tena.

Wenzetuhuko daslam maji yenu ya kuoga munawekaga nini

Nimemtaja huyo binti lakini mifano ninayo mingi tu
 
joto na maji ya chumvi vinaivisha ngozi vizuri sana, kingine Dar wanawake hawafanyi kazi ngumu kama mikoani ,ila mwanamke wa mikoani hata afanyaje ukitaka kummbaini mwanamke wa mkoani angali kiwiko cha mguu kwenda chini kwa walio wengi ni kweusi kumekomaa ila wanawake wa hapo hapo Dar miguu yao kuanzia kwenye kiwiko kwenda chini ni kulaini kumekaa kimayai mayai na hata baadhi ya wanaume wa Dar wanasifa sawa sawa na dada zao.
 
Mkuu ni Hali ya hewa ya joto, mm nimezaliwa na kukulia Dar unayoyasema ni kweli.
Ipo hivi Dar jua ni Kali Sana, na hivyo husababisha joto na kupitia joto mwili hutoa jasho Sana kiasi ambacho kama utakuwa unaoga mara kwa mara lazma ngozi itakate.

Kwa Dar ukipaka mafuta au lotion mwilini lazma iyeyuke mapema na hivyo husaidia mwili kutoa uchafu kupitia jasho tofauti na mikoani ambako ni baridi, Kule ukipaka lotion ni ngumu kuyeyuka sababi ya baridi.

Ila watu wa Dar Wana maisha magumu,wengi hawali wakashiba tofauti na wa mikoani.
 
hata ray kigosi yule wa bongo movie jiji la dar es lilimbadilisha rangi usikute hata huyo dada alikuwa mnywaji mzuri wa maji.
 
Yalee mataa yana mwanga fulani yanakufanya unaonekana umenawiri...

1741292336281.png

1741292482266.png
 
Naskia huko dar walimbwende wanatumia nishati safi ila wa huko mikoani mnatumia nishati chafu, yaani ngozi inazungukwa na moshi mpaka wanaonekana kama wazee
 
Hao wanajichubua tena ni jinsia zote! Hayo engine ni porojo tu!
 
Back
Top Bottom