Tetesi: Watu wa Mkuranga wanalalamika kupigwa na Polisi

Tetesi: Watu wa Mkuranga wanalalamika kupigwa na Polisi

Kama mbinu zenyewe ni hizo basi tatizo linakua na wanaokuza in Polisi wenyewe.
 
Enzi za mwl. kulikuwa na wizi wa ng'ombe sana kule Tarime. Kukaja na wazo kuwa, ukipigiwa kura ya wizi kuwa weye ni mwizi wa ng'ombe ulihamishwa na serekali wewe na familia yako ukapelekwa Mtwara au Nachingwea na ni marufuku kukanyaga Darisalama au Dodoma na sehemu za karibu na kwenu. Wizi ulipungua kama sio kwisha.
Wazo langu;
Tusiwapige raia wema, tuwahamishie Mbeya na vijiji vyao tuweke watu wengine watakao shirikiana na Mwingulu kumaliza tatizo hili. Hao jamaa wamejizatiti kweli kweli. Sio watu wa kubeza. Si unajua tena ni watu wa dini ileeee. Toa watu hapa peleka kulee leta wengine waje kukaa hapo. Kwani mbona vijiji vya ujamaa viliwezekana kuanzishwa?? Hao wenyeji ni wangapi?? Mbona tunaona mapori tuu??
 
Kufuatia kitendo cha jeshi la polisi kukumbwa na mfululizo wa mauji ya walinda amani wetu kwa uweledi wa hali ya juu kabisa wakazi wa barabara kati ya kibiti na Mkuranga wamechezea fimbo mchana kweupe.. na kulazimishwa kulala saa kumi na moja jioni

Wakazi hao na watanzania kiujumla hatujatangaziwa kwa nini mauaji haya yaendelee either kwa sababu za kiusalama au vinginevyo ila kinachoshangaza ni hii strategy ya kisasa kabisa yakuchezesha raia fimbo
Kwa mujibu wa shuhuda wa macho wanasema waliokua wanapigwa ni akina mama wenye watoto,vijana,na yeyote yule ambae alikua anakutwa na polisi etc, sababu iliyosababisha kukimbia vijiji kwa muda na walipohoji hawakupata majibu
Katika vipigo hivyo heavy inasemekana wengine imewalazumu kujiuguza maumivu ma hospitalini au ku survive na panadol(pain killers)
Kitu ambacho labda tunapaswa kujiuliza kwa mbinu hii je hawa raia wataleta tena ushirikiano wakutoa taarifa za siri kwa polisi? Perception yao itakuaje kwa jeshi la polisi?wataona utofauti wowote kati ya jeshi la polisi na hao wanajambazi wanaosakwa?au mbinu hii ya ku sideline moja kwa moja raia katika mapambano haya ndio imekua suluhisho pekee?

Ni muda sasa wa jeshi la polisi kufanyiwa reform kwani tumerithi mbinu za kikoloni katika utendaji kazi wake
Wachapwe Tu. Hakuna Namna - Ni JINO KWA JINO.....
 
Kama polisi anakuja anapiga RAIA asiyekuwa na hatia, ni bora kumsaidia jambazi ampige polisi anayepiga raia.
Sasa Kama raia hataki kuonesha ushirikiano kwa vyombo vya dola acha achapwe tu.
 
~AFRICAN INTELEGENCY;-
RAIA NDIYO INFORMER WA WAHALIFU NUMBER ONE...!,
•KUWA PIGA AU KUWASHURUTISHA KWA LOLOTE NI KUWAOGOFYA..!/
MUNGU TUPE HEKIMA NA BUSARA.
 
Sasa wao polisi walivamiwa usiku wa Giza, wao wanawavamia wananchi mchana kweupeee, ishi ndiyo nini sasa
 
Hao police wajichunguze matendo yao ka hao waliouawa walikuwa mabingwa wa rushwa ukipita tu na gari wanakukomalia uwape hela by force and now naona wamewageukia wananchi.
 
Majambazi wanasema hawana shida na raia shida yao ni viongozi na polisi sasa kama polisi unamuadhibu raia unafikiri atakupenda lazima ampende jambazi
 
Lile neno force liliwekwa kwa Maana ipi? Tambua hata jeshi la wananchi linaitwa TPDF, unajua hiyo F imesimama badala ya neno lipi?
TPDF - Tanzania people defending force" ungekuwa umeelewa maana hiyo hapo juu usingeniuliza , ila mungu akusamehe si kosa lako kutokwenda shule
 
Wabondwe sana mpaka waseme maana hao majambazi wanayafuga humo ndani piga sana.
 
Polisi wameuawa,wao wanashangilia!! Viongozi wa mitaa wamepigwa risasi hadi kupoteza maisha,wenyeji wanakenua meno tu.Nyambafu kabisa. Na wapigwe tu,pigeni hadi wapate akili.
 
Kama kweli kitu kama hicho kimetokea polisi wategemee sifuri kufanikisha zoezi lao hatuendi hivyo hata wakati wa vita tulifanikiwa kwa ushirikiano na wananchi wa Uganda ila tahadhari lazima iwepo kwa sababu unakuwa hujui mwema na msaliti
 
Raia wema wanapigwa hata bila huruma, wakati mwingine ni chuki binafsi tu, bibi kizee anapigwa kisa nn? Au ndio nchi ya viwanda
 
Ndiyo wakome kuwaficha majambazi na waharifu!!
 
Back
Top Bottom