Tetesi: Watu wa Mkuranga wanalalamika kupigwa na Polisi

Kama mbinu zenyewe ni hizo basi tatizo linakua na wanaokuza in Polisi wenyewe.
 
wale wenye Noah nyeusi waende na mbwembwe zao huko vichakani mkurunga wakawateke hawa mashetan walioua kikatili ndugu zetu polisi.
Mkuu Copenhagen naomba nije chemba kwako....!
 
Enzi za mwl. kulikuwa na wizi wa ng'ombe sana kule Tarime. Kukaja na wazo kuwa, ukipigiwa kura ya wizi kuwa weye ni mwizi wa ng'ombe ulihamishwa na serekali wewe na familia yako ukapelekwa Mtwara au Nachingwea na ni marufuku kukanyaga Darisalama au Dodoma na sehemu za karibu na kwenu. Wizi ulipungua kama sio kwisha.
Wazo langu;
Tusiwapige raia wema, tuwahamishie Mbeya na vijiji vyao tuweke watu wengine watakao shirikiana na Mwingulu kumaliza tatizo hili. Hao jamaa wamejizatiti kweli kweli. Sio watu wa kubeza. Si unajua tena ni watu wa dini ileeee. Toa watu hapa peleka kulee leta wengine waje kukaa hapo. Kwani mbona vijiji vya ujamaa viliwezekana kuanzishwa?? Hao wenyeji ni wangapi?? Mbona tunaona mapori tuu??
 
Wachapwe Tu. Hakuna Namna - Ni JINO KWA JINO.....
 
Kama polisi anakuja anapiga RAIA asiyekuwa na hatia, ni bora kumsaidia jambazi ampige polisi anayepiga raia.
Sasa Kama raia hataki kuonesha ushirikiano kwa vyombo vya dola acha achapwe tu.
 
~AFRICAN INTELEGENCY;-
RAIA NDIYO INFORMER WA WAHALIFU NUMBER ONE...!,
•KUWA PIGA AU KUWASHURUTISHA KWA LOLOTE NI KUWAOGOFYA..!/
MUNGU TUPE HEKIMA NA BUSARA.
 
Sasa wao polisi walivamiwa usiku wa Giza, wao wanawavamia wananchi mchana kweupeee, ishi ndiyo nini sasa
 
Hao police wajichunguze matendo yao ka hao waliouawa walikuwa mabingwa wa rushwa ukipita tu na gari wanakukomalia uwape hela by force and now naona wamewageukia wananchi.
 
Majambazi wanasema hawana shida na raia shida yao ni viongozi na polisi sasa kama polisi unamuadhibu raia unafikiri atakupenda lazima ampende jambazi
 
Lile neno force liliwekwa kwa Maana ipi? Tambua hata jeshi la wananchi linaitwa TPDF, unajua hiyo F imesimama badala ya neno lipi?
TPDF - Tanzania people defending force" ungekuwa umeelewa maana hiyo hapo juu usingeniuliza , ila mungu akusamehe si kosa lako kutokwenda shule
 
Wabondwe sana mpaka waseme maana hao majambazi wanayafuga humo ndani piga sana.
 
Polisi wameuawa,wao wanashangilia!! Viongozi wa mitaa wamepigwa risasi hadi kupoteza maisha,wenyeji wanakenua meno tu.Nyambafu kabisa. Na wapigwe tu,pigeni hadi wapate akili.
 
Kama kweli kitu kama hicho kimetokea polisi wategemee sifuri kufanikisha zoezi lao hatuendi hivyo hata wakati wa vita tulifanikiwa kwa ushirikiano na wananchi wa Uganda ila tahadhari lazima iwepo kwa sababu unakuwa hujui mwema na msaliti
 
Raia wema wanapigwa hata bila huruma, wakati mwingine ni chuki binafsi tu, bibi kizee anapigwa kisa nn? Au ndio nchi ya viwanda
 
Ndiyo wakome kuwaficha majambazi na waharifu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…