Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Watu wa Musoma tukumbushane stori za Musoma kuanzia 2000-2010

Nimewahi kunywa uji pale Mara dishes,

Kuzuri sana,

Kile kituo Cha matumaini ya vijana,

Vingekuwwpo Kila wilaya Nchi nzima tungekuwa mbali mno,

Palikuwa na walimu wa VIPAJI vingi chini ya mfadhili Toka nje Italy.
 
Marehemu Barongo alijenga nyumba na kuzungushia ukuta ukiwa na mfanano wa meli ya MV. BUkoba kama kumbukumbu ya kumpoteza mke wake katika ajali hiyo mwaka 1996....
Du kweli aise ila siku izi ukipaona, pamechoka mbaya wakati ndo ilikuwa nyumba kali maeneo hayo.
 
Alikuwa anaitwa Mutalagala kama sijakosea alifariki 2007 nyumbani kwake nasikia walikuwa wakiweka vibao kama kapumzika, au hayupo, n.k
Sio kusikia, ndivyo ilivyokuwq, mwamba alikuwa mtata sana. Aliiuwa na cheo kikubwa tu CCM,

Ukikuta kibao kimeandikwa kapumzika hapo itabidi ukae usubiri mpaka aamke.
 
Mgasa, Kinche, Bonny Weed, Ally Bega, Duchu, Maromaro (R.I.P). List ni ndefu sana kwa wanangu wa Jamaica Mockers.

Mbio za vijiti unakutana na akina Jigga, Jira, Chui, Mapacha (jamaica pia walikua na mapacha).

Huku West Lawama unakutana na wakongwe akina Majani.

Yale maisha yamefanya tukawa tough sana. Kusurvive katikati ya gangs kama zile inahitaji roho ngumu. Bahati nzuri nilikua muhuni mpenda shule, hiyo ndio ponapona yangu. Othrerwise ningekua either jela au kaburini.
Jamaica Mockers na Mbio za vijiti wametusumbua sana Musoma Tech
 
Back
Top Bottom