Kuna wadada wapo huko kipindi bado mdogo wakaja na mazawad masimu makubwa surual wamesuka manywele marefu wakasema wanafanya kazi Posta Red onion hotel
Sasa mwaka jana nikatimba huko nikaenda bar moja inaitwa Fair way kama unaenda Bunju katikati ya Tegeta na Boko eeeh nikakuta ni wahudumu wa Bar
Cha ajabu watoto wao wamewaacha mkoani ikabid waniambie nitunze siri nikawaambia nataka nije mnapokaa lahaulaaaaaa
Chumba kimoja wanakaa watu 9 Ila siku wakirudi mkoani huwa tunakoma watoto weupeee Demiss miye mpaka nataman nipake Mkorogo wa Maimartha wa Jesse nifanane nao.
Na yale manywele wanayarusha kama wakorea nywele mpaka gutako zinafika hapo Demiss nimesuka twende kilioni.
Wadada wa dar mna dhambi kama kaka zenu
Hawa ndo wanatuharibu sisi wa mkoani