Watu wajinga wanapopewa PhD za heshima!

Watu wajinga wanapopewa PhD za heshima!

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Suala la PhD (Doctor of Philosophy) zinazotolewa kama za heshima, sasa si tu linakera, bali sasa linarahisisha na kudharaulisha maana hasa ya elimu.

Kama PhD, a pinnacle of acchieved learning, research na contribution to natural understsnding, linaanza kuwa la kisiasa nchini, basi tumefikia our lowest stage of educational stupidity.

Kwamba hata wale wenye PhD za ukweli, zinazotokana na kuuliza, kujiuliza na kuandika research papers zenye mchango mkubwa kitaifa na kimataifa, halafu ukapata PhD za kina Babu Tale, na huku kina Prof Mkenda wako kimya, basi hata higher learning nchi hii haina maana yoyote.

Dr Babu Tale, Dr Msukuma, na kwa bahati mbaya kabisa wanaingizwa kina wanasiasa mashuhuri , kuwa kitaaluma wako sawa na Dr Ndulu, Dr Ng'wandu na Prof Mawenya, Prof Rweyemamu, Pro Mazengo, basi hatuna haja ya kuwa na vyuo vya elimu ya juu.

Yaani kama Msukuma, ukijulikana tu, basi unapewa PhD ya heshima.

Tukumbuke, mtu mjinga si yule aliyeelimika.
 
Suala la PhD(Doctor of Philosophy) zinazotolewa kama za heshima, sasa si tu linakera, bali sasa linarahisisha na kudharaulisha maana hasa ya elimu...
Wote wanaozitoa (kuziuza) kuzinunua hawajui maana ya PhD. Hawa vilaza wetu wanatapeliwa sana na wajinga wengine. Sitashangaa kusikia Kenya na Nigeria wameanzisha vyuo hivi ili kuwaibia hawa vilaza walioogopa umande na wasiojua kitu.

Iisitoshe ukiwa CCM unaweza kuwa Daktari, mtume, askofu, mchungaji hata kama ni tapeli. Ukiwa upinzani utaambiwa dini na siasa havichanganyiki. Tumegeuka taifa la hovyo. Walianza mchezo huu mchafu akina Jakaya Kikwete.
 
Suala la PhD(Doctor of Philosophy) zinazotolewa kama za heshima, sasa si tu linakera, bali sasa linarahisisha na kudharaulisha maana hasa ya elimu...
Wanaotoa ndio wanakosea; digirii za heshima huwa haziitwi Ph.D. kwani zinatolewa bila kuwapo Thesis wala viva voce; hizo zinaitwa Honoris Causa Doctor of Something; kwa mfano Doctor of Humane Letters, Doctor Of Humanities, Doctor of Literature, Doctor of Laws, Doctor of Leadership, Doctor of Divinity, Doctor of Arts, Doctor of Philosophy (D.Phil siyo Ph.D.), n.k. Nilishangaa hata UDSM eti walitoa Ph.D. kwa Mama. Watu hawa ambao walimpa Nyerere Honorary Doctor of Literature Honoris Causa akiwa ameandika vitabu zaidi ya 30 leo hii wanaota Ph.D. kwa mtu ambaye hajaandika chochote.
 
Suala la PhD(Doctor of Philosophy) zinazotolewa kama za heshima, sasa si tu linakera, bali sasa linarahisisha na kudharaulisha maana hasa ya elimu...

Ujinga ni mawazo yako tu. Kikwete kafanya biashara kuliko Msukuma? Unajua jamii na kaya za kule kwao kazisaidia vipi?

Hivyo tusiwe wepesi wa kujadili mafanikio ambayo huyajui. Lakini hizi PhD mbona wanapewa waimbaji kibao na wasanii huko US ingawa tofauti watu hawaoni ni kitu cha ajabu🤔 ni sisi tu tunafikiri kuitwa Dr ni kitu kikubwa
 
Acha wivu Mkuu
Babutale kafanya Mambo Makubwa kuzidi prof lipumba
 
Acha wivu Mkuu
Babutale kafanya Mambo Makubwa kuzidi prof lipumba
Hujui usemalo vingine wewe ndiye huyu Tale. Unadhani kumpromoti muuaji wa maadili kama Nasib ni deal kwa taifa? Kama wewe ni wale wanaoweza hata dada na mama zao kwa vile wanapewa dola, hili ni dili kubwa tu
 
Ni kiwango cha juu cha upumbafu Nyerere alikuwa nazo kama nne hivi lakini hakuwahi kujiita Dokta , kuja viwatu vimenunua hizo pHd feki kwenye vyuo vya mchongo ole wako isimuite dokta kitaumana, hii yote ni sababu ya kudhani kwamba kila kitu ni shortcut, tunatakiwa kujitafakari sana mbona China Malaysia etc hawaendekezi huu upuuzi? eti babu tale naye analazimisha tena bungeni aitwe dokta Stupid kabisa darasa la saba kichwani mweupe kisa ana kiubunge cha mchongo anafokea watu.
 
Mjiinga(mtu asiyesoma) Dr Babu Tale.
 
Suala la PhD (Doctor of Philosophy) zinazotolewa kama za heshima, sasa si tu linakera, bali sasa linarahisisha na kudharaulisha maana hasa ya elimu...
Hakika, ujinga si kitu cha kuheshimiwa halikadhalika na wajinga pia. Ukimtunuku mtu mjinga kitu chochote zaidi ya kumfundisha, ni kuutusi uerevu pamoja na kuwatusi werevu.
 
Acha wivu boss kua mbunge sio kitu cha mchezo watu ............Dr tale tale ni zaidi ya PHD alionayo ni true hustler kama unaona rahis jaribu uone sizani kwenye ukoo wenu kuna hata mkuu wa wllaya........uyo lipumba hadi leo tabora ajasaidia chochote just mpuuzi tu
 
Huyo mtu ni mfano wa ujinga mwingi. Kwa bahati mbaya riziki haibagui wajinga au werevu
 
Huyo mtu ni mfano wa ujinga mwingi. Kwa bahati mbaya riziki haibagui wajinga au werevu
Sawa boss ila heshimu struggle za wenzio hata kama umewazid kiacademic wao wamekuzid kiuchumi na kijamii pia........
 
Sawa boss ila heshimu struggle za wenzio hata kama umewazid kiacademic wao wamekuzid kiuchumi na kijamii pia........
Ku-struggle ni jambo moja na ku-acquire academic credentials ni jambo lingine. Tusilazimishe eti kwasababu mtu amefanikiwa kiuchumi au kimaisha basi apewe academic rewards. Huo ni ujinga mwingi
 
Back
Top Bottom