Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa

Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa

Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa , ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilisema Jumatano, ikijibu maswali kutoka kwa askofu.

Idara hiyo, inayojulikana kama Dicastery of the Doctrine of the Faith, haikuwa wazi hata hivyo, katika kujibu swali la ikiwa wenzi wa jinsia moja wanaweza kuruhusiwa kupata ubatizo wa Kanisa kwa ajili ya mtoto aliyeasiliwa au ule uliopatikana kupitia mama mlezi.

Askofu Jose Negri wa Santo Amaro nchini Brazili alituma kwa ofisi ya mafundisho maswali sita mnamo Julai kuhusu watu wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia (LGBT ) na ushiriki wao katika sakramenti za ubatizo na ndoa.

Kurasa hizo tatu za maswali na majibu zilitiwa saini na mkuu wa idara hiyo, Kadinali wa Argentina Víctor Manuel Fernández, na kuidhinishwa na Papa Francis mnamo Oktoba 31.

Ziliwekwa kwenye tovuti ya idara hiyo Jumatano kwa kutumia neno la Kiitaliano "transsexuals".

Francis, mwenye umri wa miaka 86, amejaribu kulifanya Kanisa liwe na ukarimu zaidi kwa watu wa jumuiya ya LGBT bila kubadili mafundisho ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na msemo mmoja kwamba kuvutia watu wa jinsia moja si dhambi bali ni dhambi ni kitendo chenyewe cha kushiriki mapenzi ya jinsi moja.

Katika kujibu swali la kama watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa, ofisi ya mafundisho ilisema wanaweza kwa masharti fulani na mradi tu "hakuna hatari ya kusababisha kashfa ya umma au kuchanganyikiwa miongoni mwa waumini".

BBC

View attachment 2809066
Mark 2:17
[17]Yesu aliposikia aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi; sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi. Swali kuhusu Kufunga

TAKBIR[emoji110] YESU AKIBAR [emoji109]
 
Juzi nimeandika humu kuwa huyu mzee ni shoga nikalaaniwa kweli, haya sasa kweli mtu na akili zake awabatize mashoga nae hatokuwa shoga kweli.
Hata YESU Alilaumiwa na wa-Sharia!
[emoji116][emoji116]
Matthew 9:11-12
[11]Mafarisayo walipoona, waliwaambia wanafunzi wake, Mbona mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

[12]Naye aliposikia, aliwaambia, Wenye afya hawahitaji tabibu, bali walio hawawezi.
 
Nipo nimejibanza sehemu nakunywa kahawa nasubiri majibu…
Umenikumbusha zama hizo vikombe vya muuza kahawa anaviliza Kiaina! Kuna mlio wa Aina YAKE akiuza Gongo tupu, Kuna mlio akiuza kahawa tupu, Kuna mlio WA vikombe akiuza mix Gongo na kahawa
 
Kwani kuna shida gani hapo? Kama wezi, wazinzi, wasema uongo na wauaji wanaweza kubatizwa na kuwa Wakatoliki na kusimamia sakramenti mbalimbali, hao wa jinsia moja kwa nini wasibatizwe?
We jamaa hivyo vyote tabia za tamaa za mwanadamu lakini ushoga ni kinyume kabisa na uumbaji ya unamsahisha mungu.
 
We jamaa hivyo vyote tabia za tamaa za mwanadamu lakini ushoga ni kinyume kabisa na uumbaji ya unamsahisha mungu.
Mtu anayeshiriki ushirikina hawezi kubatizwa na kuwa hata kiongozi kanisani?
 
We jamaa hivyo vyote tabia za tamaa za mwanadamu lakini ushoga ni kinyume kabisa na uumbaji ya unamsahisha mungu.
Tuanze kwa amri kumi za Mungu tuone kama tamaa za mwanadamu zinakubalika
 
Tuanze kwa amri kumi za Mungu tuone kama tamaa za mwanadamu zinakubalika
Hazikubaliki ila zinaweza kufanywa Kwa namna flani ziwe sahihi Mfano tamaa za uzinzi unarusiwa kuoa, wizi unaruhusiwa Kuomba ukapewa. Sasa ushoga ni kinyume kabisa
 
In reality hakuna dhehebu lililoanzishwa na Mungu, ila dini ikiwa na maana ya njia ya kumwelekea huyo Mungu,,, haya mengine ni mafundofundo na "mafindofindo" 😂😂😂 ya binadamu kama mimi na wewe...
YESU mwenyewe alikuwa muumini wa Uyahudi, sasa kama sisi ni wa Kristo si ni tuwe Wayahudi sasa eti?? 😂😂😂
 
Yaani et mwanaume aliyebadili jinsi awe msimamizi wa ubatizo? Kwa kiswahili kingine awe baba wa kiroho kwa huyo mtoto anayebatizwa atamuongoza huyo mtoto kuelekea wapi?

Kuna mchangiaji et amesema Mungu aliumba mashonga hivi hajui Mungu aliwaangamiza kwa moto hao sodoma na gomora kwa uovu huo huo? Huyo Papa amekengeuka hajui anachopaswa kukisimamia labda ameingia kwenywe ushawishi ili kanisa liruhusu huo uchafu
Tulia usukumiwe HOGO LA KINYEO
 
Kanisa ni kwa ajili ya wenye dhambi. Waitwe kwa wingi na waende zaidi mataifa yaliyoruhusu ushoga, waende kuwabatiza kwa jina la Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu.

Ndio maana siku hizi makanisa hayakemei dhambi, wenye dhambi (walevi, malaya, wachawi nk) wanatengwa na kusimangwa badala ya kuwekwa pamoja.

Kanisa Takatifu la Mitume limefanya kitu sahihi, bila shaka hao mashoga watapata mafunzo kabla ya ubatizo na kumkiri Kristo na kuachana na ushoga.
UZURI wa hizi dini na madhehebu yetu ni kuwa huwezi kosa shimo la kupitia hata ukibanwa na Kontena la futi 80...
 
Yaani et mwanaume aliyebadili jinsi awe msimamizi wa ubatizo? Kwa kiswahili kingine awe baba wa kiroho kwa huyo mtoto anayebatizwa atamuongoza huyo mtoto kuelekea wapi?
Hiyo habari mngeomba mtafsiriwe kwa Kiswahili halafu ndio muanze kutoa maoni, vinginevyo mtaendelea kubeba tafsiri kila mmoja anavyojisikia. Mbona sijaona ukizungumzia suala la kubatizwa wakati habari yenyewe ya kiingereza imelitaja? Ni kama vile umerukia aya uliyoielewa bila kujali kuwa kuna aya nyingine zilitangulia
 
Unajua amri kuu za mungu zipo Kwa ajili ya binadamu Ila unapoamua kuo shoga unakua unaza kujitoha katika Hali ya binadamu.
Nina maana yangu kukuuliza hivyo, kwani naona unakubali kuwabatiza waliokiuka amri kumi za Mungu (kuiba, kuua, kuzini, kusema uongo, kutamani mwanamke asiye mke wako, etc), halafu unashangaa kuwabatiza wanaofanya ushoga!
 
Mathayo 24 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³² Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
³³ nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
 
Napata Ukakasi Tena Zaidi ya Sana Na Hii Dini Tuliyokaririshwa na West. Kubadili Jinsia Ni Kumkufuru Muumba Wako, Kukufuru Kusudio Lako Ulikotoka Hapa Ulipo na Huko Uendako. Sasa huyu mzee namna gani asee
 
Mathayo 24 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
³² Basi kwa mtini jifunzeni mfano; tawi lake likiisha kuchipuka na kuchanua majani, mwatambua ya kuwa wakati wa mavuno u karibu;
³³ nanyi kadhalika, myaonapo hayo yote, tambueni ya kuwa yu karibu, milangoni.
Inafikirisha sana mkuu. Ukiunganisha dots na yanayotokea hapo middle east yawezekana ule muda uu karibu kuwadia japo sio Leo kesho wala keshokutwa
 
Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo katika Kanisa Katoliki, mashahidi katika harusi za kidini na kubatizwa , ofisi ya mafundisho ya Vatikani ilisema Jumatano, ikijibu maswali kutoka kwa askofu.

Idara hiyo, inayojulikana kama Dicastery of the Doctrine of the Faith, haikuwa wazi hata hivyo, katika kujibu swali la ikiwa wenzi wa jinsia moja wanaweza kuruhusiwa kupata ubatizo wa Kanisa kwa ajili ya mtoto aliyeasiliwa au ule uliopatikana kupitia mama mlezi.

Askofu Jose Negri wa Santo Amaro nchini Brazili alituma kwa ofisi ya mafundisho maswali sita mnamo Julai kuhusu watu wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia (LGBT ) na ushiriki wao katika sakramenti za ubatizo na ndoa.

Kurasa hizo tatu za maswali na majibu zilitiwa saini na mkuu wa idara hiyo, Kadinali wa Argentina Víctor Manuel Fernández, na kuidhinishwa na Papa Francis mnamo Oktoba 31.

Ziliwekwa kwenye tovuti ya idara hiyo Jumatano kwa kutumia neno la Kiitaliano "transsexuals".

Francis, mwenye umri wa miaka 86, amejaribu kulifanya Kanisa liwe na ukarimu zaidi kwa watu wa jumuiya ya LGBT bila kubadili mafundisho ya Kanisa, ikiwa ni pamoja na msemo mmoja kwamba kuvutia watu wa jinsia moja si dhambi bali ni dhambi ni kitendo chenyewe cha kushiriki mapenzi ya jinsi moja.

Katika kujibu swali la kama watu waliobadili jinsia wanaweza kubatizwa, ofisi ya mafundisho ilisema wanaweza kwa masharti fulani na mradi tu "hakuna hatari ya kusababisha kashfa ya umma au kuchanganyikiwa miongoni mwa waumini".

BBC

View attachment 2809066
Ipo siku huyu papa atapigiwa kura ya kutokuwa na imani naye
 
Back
Top Bottom