Watu waliokataa Magufuli asiongezewe Miaka ndio haohao wanashadadia Mbowe aendelee kuongoza. Ndio haohao wanakapinga CCM isiendelee! Unafiki mtupu!

Mpo salama!

Watu wenye ndimi mbili. Watu wenye mawe mawili ya kupimia ni watu Hatari Sana popote walipo. Ni watu wanafiki na muda wowote wanaweza kukuuza.

Alipokuwepo Magufuli, Chawa wake walitoa maoni Yao kuwa Magufuli aongezewe Muda, Magufuli atawale milele, na kama Magufuli angekataa wapo walioapa wangemshikia kiboko kumlazimisha aendelee kutawala. Yalikuwa ni maoni Yao.

Sisi wengine maoni yetu tulikataa tukasema Hapana. Miaka yake ikiisha inatosha. Wengine tukasema Katiba hairuhusu lakini Katiba ni kitabu tuu tunaweza kukibadilisha sehemu ndogo (Constitution amendment) ili kuweka kipengele cha kuongeza Muda.

Haya walewale ambao waliwaka, walimkalia kooni JPM ambaye yeye mwenyewe hata hakuwahi kusema ataongeza Miaka zaidi ya yeye kutamka hataongeza Miaka. Leo hii kile walichokuwa hawakitaki kwa JPM wanakifanya kwenye chama Chao.

Mbowe hata angekuwa kiongozi mzuri kama Malaika, kumuongezea Miaka mingine juu ya ishirini sio Sawa.

Alafu Mbowe angetakiwa aonyeshe uzuri wake katika kuandaa viongozi wengine wazuri zaidi yake wa kumrithi.

Siongei kumtetea Lisu awe kiongozi nope! Anaweza kugombea mtu mwingine Nje ya Lisu na akawa kiongozi wa CHADEMA hii itaonyesha kuwa CHADEMA inaakiba ya kutosha ya viongozi.

Kama kuna watu wanaona Mbowe aendelee Basi wasishangae wale wanaoona CCM iendelee.

Wanasema Mbowe kaitoa CHADEMA Mbali.
Watu wanasema CCM imeitoa nchi Mbali.

Uongozi mzuri ni pamoja na kuweza kuachia nafasi wengine waongoze.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
CHADEMA ITAKUFA KIFO KIBAYA SANA KAMA MBOWE ASIPO ONDOLEWA KITINI HARAKA IWEZEKANAVYO .....NIKAMA CCM KAMA SAMIA ASIPO ONDOLEWA BASI NCHI INAKWENDA KUCHAFUKA
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
Hoja ya hovyo sana. Hata Tanzania ni ya wàtanzania. Sasa CHADEMA ikichukua nchi utasema Hivyo hivyo kwamba CHADEMA ni ya wanachadema.
 
Ndiyo, CHADEMA ikichukua nchi itaendelea kubaki ya wanachedema kama ambavyo CCM leo hii ni ya wanaCCM.
 
CHADEMA ITAKUFA KIFO KIBAYA SANA KAMA MBOWE ASIPO ONDOLEWA KITINI HARAKA IWEZEKANAVYO .....NIKAMA CCM KAMA SAMIA ASIPO ONDOLEWA BASI NCHI INAKWENDA KUCHAFUKA
CHADEMA ikifa maisha ya raia yataendelea kama kawaida tu, labda itakuwa hasara kwa wanachadema ila nchi ikichafuka maisha ya raia wote yataathirika vibaya.
 
Tatizo lipo hapo hili samia aondoke hili takiwa kuwe na upinzani makini utakao sababisha ccm na serikali yake kumwona samia hatoshi hivyo kumpiga chini uchaguzi ujao na kuteua mtu mwingine....hila kwa sasa samia anayo fursa ya kung'ang'ania uongozi kwa sababu ya upinzani kukosa nguvu hivyo HATARI YA PILI YA TAIFA KUCHAFUKA INATEGEMEANA NA UPINZANI KUWA DHAIFU.
 
Lisu ashinde au asishinde tunazingatia hoja zake.

CHADEMA inahitaji Mwenyekiti mpya
Yes gentleman,
Mwenyekiti mpya wa Chadema atapatikana rasmi kabla ya Pasaka2025, na atatokana na kura za wajumbe wa mkutano mkuu Taifa wa Chadema.

Ni kweli,
ni muhimu sana kuzingatia hoja, historia, dhamira na misingi ya kuanzishwa kwa Chama Cha ha Demokrasia na Maendeleo.

Mwenyekiti mpya wa Chadema 2025-2030 atatoka kanda ya Chadema ya kiutawala ya Kaskazini 🐒
 
Tatizo lipo hapo hili samia aondoke hili takiwa kuwe na upinzani makini utakao sababisha ccm na serikali yake kumwona samia hatoshi hivyo kumpiga chini uchaguzi ujao na kuteua mtu mwingine....hila kwa sasa samia anayo fursa ya kung'ang'ania uongozi kwa sababu ya upinzani kukosa nguvu hivyo HATARI YA PILI YA TAIFA KUCHAFUKA INATEGEMEANA NA UPINZANI KUWA DHAIFU.
Kwa nini kama CHADEMA, ACT na vyama vingine vyote vya upinzani ni dhaifu msijichange mkaanzisha chama kingine cha upinzani kitakachokuwa imara kupambana na CCM??
 
Umeambiwa kama chadema ni mali ya wote wewe ccm nenda kachukue fomu ya kugombea nafasi ya uenyekit chadema
Narudia tena chadema ni Mali ya umma ndo maana Ipo chini ya msajili wa vyama vya siasa na inaishi Kwa kodi zetu na sio kikundi Cha kufa na kuzikana kama unaona chadema Ina wamiliki wataje wa miliki wote
 
Magufuli alikuwa Rais wa nchi, Mbowe ni mwenyekiti wa CHADEMA.
Nchi ni ya watu wote, wenye vyama na wasio na vyama, wenye dini, wasio na dini wapagani n.k
CHADEMA ni ya wanachadema
ukisikia wehu ndo huu uliouandika hapa
 
Narudia tena chadema ni Mali ya umma ndo maana Ipo chini ya msajili wa vyama vya siasa na inaishi Kwa kodi zetu na sio kikundi Cha kufa na kuzikana kama unaona chadema Ina wamiliki wataje wa miliki wote
NImekuambia wewe mwana ccm nenda kachukue fomu ya kugombea uenyekiti wa chadema si mali ya umma
 
Mpo salama!

Watu wenye ndimi mbili. Watu wenye mawe mawili ya kupimia ni watu Hatari Sana popote walipo. Ni watu wanafiki na muda wowote wanaweza kukuuza.

Alipokuwepo Magufuli, Chawa wake walitoa maoni Yao kuwa Magufuli aongezewe Muda, Magufuli atawale milele, na kama Magufuli angekataa wapo walioapa wangemshikia kiboko kumlazimisha aendelee kutawala. Yalikuwa ni maoni Yao.

Sisi wengine maoni yetu tulikataa tukasema Hapana. Miaka yake ikiisha inatosha. Wengine tukasema Katiba hairuhusu lakini Katiba ni kitabu tuu tunaweza kukibadilisha sehemu ndogo (Constitution amendment) ili kuweka kipengele cha kuongeza Muda.

Haya walewale ambao waliwaka, walimkalia kooni JPM ambaye yeye mwenyewe hata hakuwahi kusema ataongeza Miaka zaidi ya yeye kutamka hataongeza Miaka. Leo hii kile walichokuwa hawakitaki kwa JPM wanakifanya kwenye chama Chao.

Mbowe hata angekuwa kiongozi mzuri kama Malaika, kumuongezea Miaka mingine juu ya ishirini sio Sawa.

Alafu Mbowe angetakiwa aonyeshe uzuri wake katika kuandaa viongozi wengine wazuri zaidi yake wa kumrithi.

Siongei kumtetea Lisu awe kiongozi nope! Anaweza kugombea mtu mwingine Nje ya Lisu na akawa kiongozi wa CHADEMA hii itaonyesha kuwa CHADEMA inaakiba ya kutosha ya viongozi.

Kama kuna watu wanaona Mbowe aendelee Basi wasishangae wale wanaoona CCM iendelee.

Wanasema Mbowe kaitoa CHADEMA Mbali.
Watu wanasema CCM imeitoa nchi Mbali.

Uongozi mzuri ni pamoja na kuweza kuachia nafasi wengine waongoze.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Siasa ni sihasa🤣🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom