Mpo salama!
Watu wenye ndimi mbili. Watu wenye mawe mawili ya kupimia ni watu Hatari Sana popote walipo. Ni watu wanafiki na muda wowote wanaweza kukuuza.
Alipokuwepo Magufuli, Chawa wake walitoa maoni Yao kuwa Magufuli aongezewe Muda, Magufuli atawale milele, na kama Magufuli angekataa wapo walioapa wangemshikia kiboko kumlazimisha aendelee kutawala. Yalikuwa ni maoni Yao.
Sisi wengine maoni yetu tulikataa tukasema Hapana. Miaka yake ikiisha inatosha. Wengine tukasema Katiba hairuhusu lakini Katiba ni kitabu tuu tunaweza kukibadilisha sehemu ndogo (Constitution amendment) ili kuweka kipengele cha kuongeza Muda.
Haya walewale ambao waliwaka, walimkalia kooni JPM ambaye yeye mwenyewe hata hakuwahi kusema ataongeza Miaka zaidi ya yeye kutamka hataongeza Miaka. Leo hii kile walichokuwa hawakitaki kwa JPM wanakifanya kwenye chama Chao.
Mbowe hata angekuwa kiongozi mzuri kama Malaika, kumuongezea Miaka mingine juu ya ishirini sio Sawa.
Alafu Mbowe angetakiwa aonyeshe uzuri wake katika kuandaa viongozi wengine wazuri zaidi yake wa kumrithi.
Siongei kumtetea Lisu awe kiongozi nope! Anaweza kugombea mtu mwingine Nje ya Lisu na akawa kiongozi wa CHADEMA hii itaonyesha kuwa CHADEMA inaakiba ya kutosha ya viongozi.
Kama kuna watu wanaona Mbowe aendelee Basi wasishangae wale wanaoona CCM iendelee.
Wanasema Mbowe kaitoa CHADEMA Mbali.
Watu wanasema CCM imeitoa nchi Mbali.
Uongozi mzuri ni pamoja na kuweza kuachia nafasi wengine waongoze.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Wewe ni mtu unayeheshimika sana, wengi tunaamini una uelewa mpana sana.
Chadema hakijawahi kushika dola, Kiko kwenye harakati za kupambana kushika dola. Kuongoza chama siyo SAWA na kuongoza nchi. Mashariki ya kati nchi ya Israel inaongoza kwa kuwa na demokrasia Bora kuliko wote ukanda ule, lakini huyu Netanyahu amekuwa waziri mkuu kwa muda gani?
Kama Chadema akiwemo Lisu mwenyewe waliondoa ukomo wa madaraka, na yeye amekiri alisimamia mapatano ya kuhakikisha waliojitokeza kuhoji au kubadilisha mfumo aliwashughulikia kama msimamizi mkuu wa nidhamu ndani ya chama, Kwa Nini tusisubiri mchakato mzima uanze na kuisha na siye tukosoe pale ambako hapakuwa sawa?
Ikiwa Kuna haja ya kuweka ukomo hilo si linawezekana kwenye vikao vya chama na ni rahisi tu!!
Tuhuma za chama cha ccm kuingilia uchaguzi hilo halikwepeki, Chadema ni tishio kwa ccm sana tu.
Sisi wengine ni watu wazima, tulishuhudia nguvu ya Mrema, 1995 na ukweli tushukuru sana uwepo wa Mwl. Nyerere ambaye alisaidia sana kuidhibiti serikali isiingilie kampeni za wagombea. Ilifikia hatua Mwalimu anahutubia huku magari yenye vipasa sauti vyenye sauti kubwa na mziki,vikikatiza kwenye mikutano yake ya kumnadi Mkapa na kusimamisha mkutano kwa muda, lakini Mwalimu hakupaniki bali aliwavumilia tu,je Hawa watawala na polisi tulionao sasa wanaweza kuvumilia na watadhibitiwa na nani?
Kama kweli tunataka mabadliko ni wananchi ndio wanayaanzisha, Mrema aliweza kwa kuwa alikuwa na mtaji wa watu ambao aliwapata akiwa waziri wa mambo ya ndani, japo kiuhalisia hakufaa kuwa Rais, kutokana na style yake ya kutoheshimu Sheria na haki za binadamu.
Tundu Lisu ni jasiri na ana uthubutu wa kufanya chochote bila kujali kitamgharimu nini, binafsi, ukweli tunaomsikia tunamuamini,hata hivyo wapo wanaofanya naye kazi kwa karibu kwenye ofisi Moja,ni viziri nao tuwasikilize wanamuonaje?
Amelalamikia kuhusu rushwa ndani ya Chadema, basi afanye kama alivyofanya Dr. Slaa Mwembechai, 2008/2010 kututajia hao waliopewa na Abdul.